Vita ya Intaneti Tanzania: Faiba vs Ruta za mchongo

halotel mpeni miaka mitano kutoka mwaka jana 2025,mpaka mwaka 2030 soko la fiber ataliteka
 
Sababu zao zipii? Si waliambiwa waweke ofisi Tanzania wakakataa je hiyo ndio sababu?
Jamuhuri janja janja nyingi.

Sheria ya Tanzania inamnyima muendeshaji wa satellite kuuza intaneti moja kwa moja kwa mtumiaji wa mwisho . Ni lazima wauze kupitia makampuni ya ndani au wasajili kampuni tanzu nchini

Musk akakataa kufanya biasha na madalali kama kina RA. Amefungua iyo kampuni tanzu STARLINK SATELLITE TANZANIA LIMITED na Tangu 2024 adi sasa hawajampa leseni.

Starlink hajakataa kuweka ofisi. Na iyo kampuni tanzu alishafungua tangu tangu 2024 na TCRA alitoa tangazo eti anakusanya maoni ya wananchi tukiridhia ndo watoe leseni, very stupid πŸ˜‚.
Mbona bandari hawakutushikisha ?

Mbona picha liko wazi mkuu. Yaleyale ya SGR NO SEAT AVAILABLE.
 
Una bahati, kwa wengine inaweza kuchukua muda mrefu kukufungia. Kama mdau alivyokupa tahadhari, siku ukipata changamoto unaweza kushangazwa. Kubwa zaidi wana staff wachache sana kuweza kutatua changamoto yako kwa wakati. Ila vifurusho vyao na speed ni vizuri.
 
Mkuu TTCL wakishaweka miundombinu yao, kukufungia naona ni haraka. Mimi nina watu kadhaa hapa mtaani, walivyolipia tu, siku hiyo hiyo walikuja kufungiwa. Labda inategemea na maeneo.
 
TTCL wanajikongoja. Kuna hawa wanajiita Savanna, bwana we wanasambaza nyaya kama hawana akili.
Shida ni kwamba wakati fiber wanaanza sambaza nyaya walikuwa wamelenga maeneo ya biashara na ya kishua ila kwa sasa internet ni kama king'amuzi hata nyumba za kupanga uswazi watu wanachanga
 
Hao Savanna kinondoni wana credit nzuri sana, watu wanaisifu service yao kuwa stable. Mimi kwa sasa TTCL naiona inaupiga mwingi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…