Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Kama upo uwezekano wa Mtanganyika kugombea ubunge Zanzibar au kuongoza nchi ya watu wa Zanzibar bila vizingiti vya kusheria muungano ungeeleweka.

Kama Mtanganyika angeweza kununua ardhi kama raia wa Tanzania huu muungano tusingeupigia kelele.
Usijitoe ufahamu, structure ya Muungano ilivyowekwa ni kuwabembeleza Wazanzibar ambao hawajawahi uhitaji huo Muungano Bali Bara so ulisema hamtaki wawe Marais ni nonsense.
 
Na tufanye haraka kugawana fito kwani mkoloni anakasi ya ajabu kuuza urithi wa vizazi vijavyo vya Watanganyika.
Nyie Machadema ndio mnaongea hayo ila CCM kamwe wasingetaka Muungano uvunjike Kwa maslahi mapana ya Nchi ambayo wanayajua wao.

Je nyie Machadema mnaona hakuna haja ya Muungano?

Acha ujinga
 
..Ccm walikuwa wanakataa serikali 3 kipindi kile Raisi wa muungano ni Mtanganyika.

..baada ya Samia kuwa Raisi, Ccm wameona madhara ya serikali 2 na kuwa na Rais toka Zanzibar.

..Tanganyika ingekuwa na serikali yake malalamiko dhidi ya Raisi Mzanzibari yasingekuwa na mantiki.
 
Mbovu Kwa muktadha wa nani? Ndio maana nimesema nyie Machadema ndio mnaona ni mbovu,Je ccm wanaona ni mbovu?
Mwl wako wa Civic form 2 alipata shida sana.

Hivi wewe unaona ni sawa raia wa upande mmoja wa muungano kuwa na haki zote za kuchagua na kuchaguliwa huku raia wa upande wa pili wakinyimwa haki hizo !.

Ni sawa na ni haki mzanzibar kumiliki ardhi Tanganyika lakini ni haramu mtanganyika kumiliki ardhi Zanzibar!.

Ni sawa na ni haki Mzanzibar kutawala huku Tanganyika lakini ni haramu Mtanganyika kutawala Zanzibar !.

Ni sawa Mzanzibar kuongoza wizara ambazo si za Muungano lakini ni haramu kwa Mtanganyika.

Ni halali kuajiriwa huku Tanganyika katika taasisi ambazo si za muungano lakini ni haramu kwa Mtanganyika kuajitiwa mamlaka ya bandari huko Zanzibar?.

Huu ujinga wote bado unajaribu kuwaingiza CDM.
 
Kazi ipo
 
Nyie Machadema ndio mnaongea hayo ila CCM kamwe wasingetaka Muungano uvunjike Kwa maslahi mapana ya Nchi ambayo wanayajua wao.

Je nyie Machadema mnaona hakuna haja ya Muungano?

Acha ujinga
Wewe ndiye mpumbavu kabisa,sisi tunaongelea maslahi ya Tanganyika ndani ya huu muungano wa mchongo wewe unaongelea mambo ya CCM. Sisi tunataka muundo wa muungano urekebishwe kwa maslahi mapana ya Tanganyika na kama hilo lisipofanyika ndiyo tunaona bora uvunjike.
 
Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili tofauti kila moja ina Rais wake, jeshi lake, bendera yake, wimbo wa Taifa lake, benki kuu yake , passport yake, je bado tu hamuelewi?
 
Mataifa mawili yaliyoungana yanaongozwa na Raia wa Zanzibar.

Kero za muungano zinatatuliwa na Wazanzibar wawili.Huu ni upuuzi wa kiwango cha kutisha.
so what! Mbona watanganyika waliongoza nchi hii kwa muda wa miaka 57, sasa mzanzibari ndiyo imekuwa kesi.
 
Hivi wewe unaona ni sawa raia wa upande mmoja wa muungano kuwa na haki zote za kuchagua na kuchaguliwa huku raia wa upande wa pili wakinyimwa haki hizo !.
hivi wewe umekosa haki gani ya kuchagua na kuchaguliwa hapo ulipo, au ulitaka uchague diwani wa zanzibar wakati wewe unaishi tanganyika?
 
Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili tofauti kila moja ina Rais wake, jeshi lake, bendera yake, wimbo wa Taifa lake, benki kuu yake , passport yake, je bado tu hamuelewi?
Hapo patamu Rais wa Zanzibar ni Mzanzibar,Rais wa Tanganyika ni Mzanzibar !.

Nchi mbili zote zinaongozwa na Raia kutoka nchi moja ya Zanzibar.Tanganyika hakuna watu wa kuongoza Tanganyika.

Hapa tatizo ni katiba mbovu ambayo imeizika Tanganyika.
 
hivi wewe umekosa haki gani ya kuchagua na kuchaguliwa hapo ulipo, au ulitaka uchague diwani wa zanzibar wakati wewe unaishi tanganyika?
Haki ya kuchagua Rais wa Zanzibar au Mtanganyika kugombea uRais wa Zanzibar. Mzanzibar anaweza kugombea ubunge wa Temeke au Kinondoni bila vikwazo vya kisheria.

Mtanganyika hawezi kugombea ubunge au uwakilishi wa jimbo lolote nchi ya Zanzibar.
 
Nyerere vipi, mmepelekea habari airudishe Tanganyika?
 
Hapo patamu Rais wa Zanzibar ni Mzanzibar,Rais wa Tanganyika ni Mzanzibar !.

Nchi mbili zote zinaongozwa na Raia kutoka nchi moja ya Zanzibar.Tanganyika hakuna watu wa kuongoza Tanganyika.

Hapa tatizo ni katiba mbovu ambayo imeizika Tanganyika.
Ndiyo maana hatutaki huu muungano fake, uvunjwe haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…