Vita ya kumaliza kesi ya Lissu katika giza la kufungiwa kwa CHADEMA

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Heche kahama.jpg

Wakati CHADEMA ikianza operesheni ya “Katiba Mpya Free Lissu” katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, tayari hofu imeshatanda serikalini, ambapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeiandikia baria ikitaka ijieleze kwa nini isifungiwe au kutozwa faini.
Chadema kahama.jpg

Miongoni mwa makossa wanayotakiwa kujieleza ni kauli ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche aliyetangaza kufanyika maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu aliyekaa gerezani kwa Zaidi ya mwaka mzima akishitakiwa kwa makossa ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Geita Mei 17, 2026, Heche amesema wameanza ikutano ya operesheni ili kuwaandaa wananchi na maandamano makubwa ambayo pamoja na mengine yatakuwa ni ya kushinikiza Lissu aachiliwe huru.

Kwa mujibu wa Heche, Lissu anapitia mateso makali gerezani na hata kuhofia afya yake, akibainisha kuwa hivi karibuni aligua tumbo baada ya kupewa matunda na maofisa wa Megereza.

Awali katika mkutano wa kuzindua operesheni hiyo uliofanyika katika mji wa Katoro mkoani Geita, Katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika alisema kuna njia mbili za kumwachilia Lissu ambazo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuifuta kesi hiyo kwa Nolle Proseque au Mahakama kuharakisha kesi hiyo iliyokwama katika Mahakama ya Rufani Februari 24, 2026.

Kitendawili

Hata hivyo, suala la kuachiliwa kwa Lissu linaonekana kuwa kitendawili kigumu kilichoshindwa kuteguliwa na Mahakama kwa sababu haieleweki sababu za kuchelewesha kesi yake mpaka sasa.

Kwa upande mwingine Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kutia mguu chini kupinga madai ya CHADEMA kutaka Lissu aachiliwe huru kama sharti la chama hicho kuingia kwenye mazungumzo ya maridhiano.

View attachment 3591036
Wakati CHADEMA ikianza operesheni ya “Katiba Mpya Free Lissu” katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, tayari hofu imeshatanda serikalini, ambapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeiandikia baria ikitaka ijieleze kwa nini isifungiwe au kutozwa faini.
View attachment 3591045
Miongoni mwa makossa wanayotakiwa kujieleza ni kauli ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche aliyetangaza kufanyika maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu aliyekaa gerezani kwa Zaidi ya mwaka mzima akishitakiwa kwa makossa ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Geita Mei 17, 2026, Heche amesema wameanza ikutano ya operesheni ili kuwaandaa wananchi na maandamano makubwa ambayo pamoja na mengine yatakuwa ni ya kushinikiza Lissu aachiliwe huru.

View attachment 3591037

Kwa mujibu wa Heche, Lissu anapitia mateso makali gerezani na hata kuhofia afya yake, akibainisha kuwa hivi karibuni aligua tumbo baada ya kupewa matunda na maofisa wa Megereza.

View attachment 3591038

Awali katika mkutano wa kuzindua operesheni hiyo uliofanyika katika mji wa Katoro mkoani Geita, Katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika alisema kuna njia mbili za kumwachilia Lissu ambazo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuifuta kesi hiyo kwa Nolle Proseque au Mahakama kuharakisha kesi hiyo iliyokwama katika Mahakama ya Rufani Februari 24, 2026.

Kitendawili

Hata hivyo, suala la kuachiliwa kwa Lissu linaonekana kuwa kitendawili kigumu kilichoshindwa kuteguliwa na Mahakama kwa sababu haieleweki sababu za kuchelewesha kesi yake mpaka sasa.

Kwa upande mwingine Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kutia mguu chini kupinga madai ya CHADEMA kutaka Lissu aachiliwe huru kama sharti la chama hicho kuingia kwenye mazungumzo ya maridhiano.

View attachment 3591042
kwa wakati muafaka taasisi hiyo itashikishwa adabu kwa mujibu wa sheria za nchi 🐒
 
Hata hivyo, suala la kuachiliwa kwa Lissu linaonekana kuwa kitendawili kigumu kilichoshindwa kuteguliwa na Mahakama kwa sababu haieleweki sababu za kuchelewesha kesi yake mpaka sasa.
 
Lisu ni shujaa watamuua lakini ukweli utabaki
Hafi ng'oo kwa matakwa yao ya kibinadamu, wala kwa hila zao, wala kwa uchawi na uganga wao kwa Jina la Yesu KRISTO!!

Atakufa pale tu atakapokuwa amelitimiza kusudi la Mungu lililomleta hapa duniani na ktk nchi ya Tanganyika..!!
 
Back
Top Bottom