Vita ya nafasi ya pili imepamba moto haswa

Vita ya nafasi ya pili imepamba moto haswa

Hii imetokea kwa bahati mbaya ama? wapinzani wa mwishoni kwa Azam na kwa Simba wanafanana. Wapinzani wa Azam ndio wapinzani hao hao kwa Simba kumalizia ligi.

KMC
JKT
Geita na
Kagera
 
Mtoto wa mama kutengenezewa njia mtaona Kila ngozi aka 5
 
Azam akishinda hiyo game, nafasi ya pili yake.
Ila hii timu ilivyo ya kizwazwa isiyo na hamasa si ajabu ikatandikwa.
 
Mechi baina ya Simba dhidi ya Azam ndio itakayotoa mwanga ni timu ipi inaweza kucheza klabu bingwa msimu ujao.
Azam wakiwa wameshuka dimbani mara 25 wakijikusanyia alama 57 wanapigana vita dhidi ya Simba ambayo imecheza michezo 24 wakiwa na point 53.
Timu hizo zitakutana wenyewe kwa wenyewe tarehe 9 huku Simba wakihitaji zaidi ushindi ili kukaa nafasi ya pili mapema kabisa.

Hizi hapa ni mechi 4 za Azam baada ya kumalizana na Simba tarehe 9
1) vs KMC- Chamazi
2) vs JKT Tanzania- Isamuhyo
3) vs Kagera- Chamazi
4)vs Geita- Nyankumbu

Hizi ni mechi tano za Simba baada ya mechi dhidi ya Azam
1) Vs Kagera- Kaitaba
2) vs Dodoma- Jamuhuri
3) vs Geita- Chamazi
4) vs KMC- Chamazi
5) vs JKT Tanzania- Chamazi

Je kati ya Azam na Simba ni yupi mwenye ratiba ngumu hapo? Ni yupi ataweza kupambana kucheza champions league msimu ujao?
Naomba Mungu Simba yetu isipate nafasi ya pili.
 
Mmiliki wa AZAM ni shabiki wa Simba over.

Siongezi wala kupunguza neno.
Ila Azam kupaa kwenye soka ndo dream yake , hivyo kesho ushabiki utabaki mfukoni na ataruhusu vijana wafungue boosters waikande Simba. Azam kushinda kutamletea mabilioni, ataangazia kwenye ugali kwanza!! Hata ungekuwa wewe ungeikanda Simba maana huyu tunae sasa ni Simba mzee hana makali yoyote.
 
Back
Top Bottom