Vita ya serikali na kanisa; je, Tanzania ina cha kujifunza kutoka Uingereza

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Tarehe Mei 28 hadi Juni 2, 1982 itakumbukwa kwa Papa John Poul II, kuwa Papa wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutembelea taifa la Uingereza tangu mgawanyiko wa Reformation 1530, uliosababisha kuundwa kwa Kanisa la Anglikana, yaani Church of England.

Mojawapo ya matukio muhimu katika ziara hiyo ilikuwa ni mkutano wa kihistoria kati ya Papa John Poul II, mkuu wa kanisa katoliki duniani na Robert Runcie Askofu mkuu wa kanisa kuu la Canterbury, ambalo ndilo kitovu cha Kanisa la Anglikana duniani, ambapo kwa pamoja walitembelea na kufanya sala mbele ya kaburi la Thomas Becket aliyeuliwa Disemba 29, 1170 na askari wa mfalme Henry II.

Kwanini Papa na Askofu Robert Runcie, walitembelea na kusali mbele ya kaburi hilo? Thomas Becket alikuwa Askofu Mkuu wa Canterbury mwaka 1164-1170, kipindi ambacho Uingereza ilikuwa bado ikifuata imani ya Kikatoliki na ilikuwa chini ya utawala wa Henry II (1154–1189). Mwaka 1163, wawili hawa waliingia kwenye mgogoro mkali wa kisiasa, kisheria, na kidini ulioishia kwa mauaji ya Becket mwaka 1170. Kiini cha mgogoro huu ilikuwa ni kama ifuatavyo:

MOJA: Mfalme Henry alitaka kanisa liwe chini ya sheria za kifalme, kuzuia rufaa kwa Papa, na kudhibiti uteuzi wa maafisa wa kanisa kupitia Katiba ya Clarendon (1164). Becket alikataa, akisimamia "uhuru wa kanisa".

MBILI; Henry alitaka makasisi waliotuhumiwa kwa uhalifu wa kiraia kuhukumiwa na korti za kifalme kupitia sheria ya Criminous Clerks. Becket alipinga, akisema kanisa pekee ndilo lililokuwa na mamlaka ya kuwahukumu.

TATU: Becket alipinga kodi za kifalme kwa makasisi

Baada ya kuona Askofu Thomas Becket amekuwa kero kwake, Mfalme II aliwaambia askari wake "Will no one rid me of this turbulent priest?" Desemba 29, 1170, askari wanne walikwenda Canterbury na kumuua Becket kwa upanga ndani ya kanisa wakati ibada ya jioni inafanyika. Thomas Becket Alitangazwa mtakatifu na Papa Alexander III mwaka 1173.

Mwaka 1174 baada shinikizo kubwa kutoka kwa Papa Alexander III na umma wa Kikristo, Henry II alisafiri hadi Canterbury Cathedral, mahali ambapo Becket aliuawa, akiwa mguu peku, akiwa na mavazi ya toba ya kanzu ya kitawa, na alikubali kupigwa mijeledi na watawa kama ishara ya kutubu. Aidha Henry alikubali kuachana na baadhi ya mamlaka yake dhidi ya Kanisa, na kuruhusu baadhi ya haki za kanisa ambazo alikuwa akizizuia kabla ya mauaji ya Becket.

Msimamo wa Injili juu ya uhusiano wa kanisa na serikali ni "Mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu" (Mathayo 22:21). Katika Napoleonic Code 1804 tunasoma "Faith is beyond the reach of the law. It is the most personal possession of man, and no one has the right to demand an account for it."
 
Najua wenye Nia mbaya na huyu mama Kuna jambo kuuubwa mnajaribu Kila Hali kumtengenezea Ili akwame......mtashindwa mara bilioni kama mlivyomshindwa mpaka Sasa. Baada ya nrne yenu kukwama Sasa mnageukia kwa Kasi kwenye udini na huko mmeona mumchonganishe na kanisa (Wakristo wote).
Tanzania hakuna vita yoyote kati ya kanisa na serikali. Poleni sana.
 
Acha kusingzia,hakuna anayemkwamisha.Anajikwamisha mwenyewe akisaidiwa na wanafiki kama wewe
 
Najua wenye Nia mbaya na huyu mama Kuna jambo kuuubwa mnajaribu Kila Hali kumtengenezea Ili akwame......mtashindwa mara bilioni kama mlivyomshindwa mpaka Sasa. Baada ya nrne yenu kukwama Sasa mnageukia kwa Kasi kwenye udini na huko mmeona mumchonganishe na kanisa (Wakristo wote).
Tanzania hakuna vita yoyote kati ya kanisa na serikali. Poleni sana.
Chapisho hili ni historia ya kweli kuhusu kilichotokea uingereza karne ya 12, kwanini ww unalipokea kama ni shambulizi dhidi ya Rais wetu? Tujifunze kuyajadili mambo kwa uhalisia wake bila chachu za kiitikadi. Rais Samia sio tu ni Rais wangu, pia ni mwenyekiti wangu na nimgombea wangu wa Urais. Lakini hilo halinifanyi kuwa mfungwa wa fikra kiasi cha kupoteza uhuru wakushiriki mijadala ya kijamii.
 
Najua wenye Nia mbaya na huyu mama Kuna jambo kuuubwa mnajaribu Kila Hali kumtengenezea Ili akwame......mtashindwa mara bilioni kama mlivyomshindwa mpaka Sasa. Baada ya nrne yenu kukwama Sasa mnageukia kwa Kasi kwenye udini na huko mmeona mumchonganishe na kanisa (Wakristo wote).
Tanzania hakuna vita yoyote kati ya kanisa na serikali. Poleni sana.
Sisi watu wa Mbeya tumemkosea nn Samia, kwa nn tunazuiwa kwenda kuabudu? Askofu anayeendesha ibada hapa kanisani kwetu sio Gwajima, Speech mbili alizozitoa, moja aliifanya mbele ya waandishi wa habari (kukemea utekaji), ya pili aliifanya kwenye kanisa lililopo Dar ( akifafanua zaidi kile alichokisema kwenye press). Sasa sisi waumini huku Mbeya kosa letu ni lipi? Mbona misikiti haifungwi wakati kila mara tunawasikia viongozi wa kiislamu wakiongelea siasa misikitini?
 
Chapisho hili ni historia ya kweli kuhusu kilichotokea uingereza karne ya 12, kwanini ww unalipokea kama ni shambulizi dhidi ya Rais wetu? Tujifunze kuyajadili mambo kwa uhalisia wake bila chachu za kiitikadi. Rais Samia sio tu ni Rais wangu, pia ni mwenyekiti wangu, nimgombea wangu. Lakini hilo halinifanyi kuwa mfungwa wa fikra kiasi cha kupoteza uhuru wakushiriki mijadala ya kijamii.
Hata Gwajima alisema hivyohivyo, lakini haikusaidia kuzuia mashambulizi toka kwa mwenyekiti wake huyo.

Jihadhari.
 
Usituletee stori za 19 kweusi
Gwajima ni tapeli anaedanganya kufufua watu
 
Sisi watu wa Mbeya tumemkosea nn Samia, kwa nn tunazuiwa kwenda kuabudu? Askofu anayeendesha ibada hapa kanisani kwetu sio Gwajima, Speech mbili alizozitoa, moja aliifanya mbele ya waandishi wa habari (kukemea utekaji), ya pili aliifanya kwenye kanisa lililopo Dar ( akifafanua zaidi kile alichokisema kwenye press). Sasa sisi waumini huku Mbeya kosa letu ni lipi? Mbona misikiti haifungwi wakati kila mara tunawasikia viongozi wa kiislamu wakiongelea siasa misikitini?
Watu wa Mbeya ni wacha Mungu sana, kwavyovyote vile, hatua ya Serikali kufunga kanisa lenu, isingeacha kuwaumiza. Wito wangu kwenu, huu ndio wakati wa kuirejelea sala maarufu ya "Lord, open the King of England's eyes" ya William Tyndale October 1536. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho(Waefeso 6:12)
 
Kama Askofu mwenye makanisa zaidi ya 2000, Mbunge wa JMT, Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ni muhuni, nchini kwetu hapa nani atapona kuitwa Muhuni?
Hata wahuni wana watu dogo. Hujui hilo? Ahahahahaha! Hata kusema ana makanisa 2000 ni uhuni ndio maana anashughulikiwa. Na kumbuka hili, makanisa HAYAWEZI kuwepo kwenye nchi isiyo na ustawi na amani. Hivyo, anayeondoa ustawi huo ni mhuni kama Gwajima and should be treated as such!
 
Hata wahuni wana watu dogo. Hujui hilo? Ahahahahaha! Hata kusema ana makanisa 2000 ni uhuni ndio maana anashughulikiwa. Na kumbuka hili, makanisa HAYAWEZI kuwepo kwenye nchi isiyo na ustawi na amani. Hivyo, anayeondoa ustawi huo ni mhuni kama Gwajima and should be treated as such!
Sisi watu wa Mbeya tumemkosea nn Samia, kwa nn tunazuiwa kwenda kuabudu? Askofu anayeendesha ibada hapa kanisani kwetu sio Gwajima, Speech mbili alizozitoa, moja aliifanya mbele ya waandishi wa habari (kukemea utekaji), ya pili aliifanya kwenye kanisa lililopo Dar ( akifafanua zaidi kile alichokisema kwenye press). Sasa sisi waumini huku Mbeya kosa letu ni lipi? Mbona misikiti haifungwi wakati kila mara tunawasikia viongozi wa kiislamu wakiongelea siasa misikitini?
 
basi ashitakiwe Kwa utapeli,lkn akisema watu wasitekwe nyie mnao mpinga mnasema watekwe? kosa lake hapa ni Nini?
Hivi kuna sehemu serikali imesema Gwajima anatafutwa? au kaamua kujificha tu mwenyewe....
Kuhusu kufutwa kwa kanisa hilo anatakiwa akapambane mahakamani na hakuna anayemkataza kufungua madai ya kufutiwa kanisa lake, na nasema kanisa lake sababu kaliaanzisha mwenyewe kama shughuli zake za kipato.
 
Sisi watu wa Mbeya tumemkosea nn Samia, kwa nn tunazuiwa kwenda kuabudu? Askofu anayeendesha ibada hapa kanisani kwetu sio Gwajima, Speech mbili alizozitoa, moja aliifanya mbele ya waandishi wa habari (kukemea utekaji), ya pili aliifanya kwenye kanisa lililopo Dar ( akifafanua zaidi kile alichokisema kwenye press). Sasa sisi waumini huku Mbeya kosa letu ni lipi? Mbona misikiti haifungwi wakati kila mara tunawasikia viongozi wa kiislamu wakiongelea siasa misikitini?
Mna bahati mbaya ya kuwa na Kiongozi mhuni kama Gwajima. Hiyo misikiti inafungwa kwa kosa gani?
 
Usituletee stori za 19 kweusi
Gwajima ni tapeli anaedanganya kufufua watu
Mambo ya imani ni magumu sana. Mfano, ufufuo ni miongoni mwa mafundisho makuu kwenye imani ya kikristo. Katika 1Wafalme17:17-24 Elia amfufua mtoto wa mjane wa Zarephath, 2Wafalme4:32-37 Elisha alimfufua mtoto wa mwanamke mshunani, 2Wafalme13:20-21 Mfupa wa Elisha ulimfufua mfu, Matendo9:36-42 petro anamfufua Thabitha, Matendo20:7-12 Paulo anamfufua Eutiko, Luka7:11–17 Yesu amfufua kijana wa mjane wa Naini, Luka8:49–56 Yesu amfufua binti wa mkuu wa Synagoge na Yohana11:1–44 Yesu anamfufua Lazaro. Kwa mafungu hayo utapeli wa Gwajima katika kuombea watu wafufuke unatoka wapi? Approach ya Bishop Gwajima ilikuwa na mapungufu, lakini kwakumpuuza serikali ingenufaika zaidi kuliko kupambana naye.
Katika Napoleonic Code 1804 tunasoma "Faith is beyond the reach of the law. It is the most personal possession of man, and no one has the right to demand an account for it."
 
B
Tarehe Mei 28 hadi Juni 2, 1982 itakumbukwa kwa Papa John Poul II, kuwa Papa wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutembelea taifa la Uingereza tangu mgawanyiko wa Reformation 1530, uliosababisha kuundwa kwa Kanisa la Anglikana (Church of England).

Mojawapo ya matukio muhimu katika ziara hiyo ilikuwa ni Mkutano wa kihistoria kati ya Papa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Robert Runcie, katika Kanisa Kuu la Canterbury ambalo ndio kitovu cha Kanisa la Anglikana, ambapo kwa pamoja walitembelea na kufanya sala mbele ya kaburi la Thomas Becket aliyeuliwa Disemba 29, 1170 na askari wa mfalme Henry II.

Kwanini Papa na Askofu Robert Runcie, walitembelea na kusali mbele ya kaburi hilo? Thomas Becket alikuwa Askofu Mkuu wa Canterbury mwaka 1164-1170, kipindi ambacho Uingereza ilikuwa bado ikifuata imani ya Kikatoliki na ilikuwa chini ya utawala wa Henry II (1154–1189). Mwaka 1163, wawili hawa waliingia kwenye mgogoro mkali wa kisiasa, kisheria, na kidini ulioishia kwa mauaji ya Becket mwaka 1170. Kiini cha mgogoro huu ilikuwa ni kama ifuatavyo:

MOJA: Mfalme Henry alitaka kanisa liwe chini ya sheria za kifalme, kuzuia rufaa kwa Papa, na kudhibiti uteuzi wa maafisa wa kanisa kupitia Katiba ya Clarendon (1164). Becket alikataa, akisimamia kwa "uhuru wa kanisa".

MBILI; Henry alitaka makasisi waliotuhumiwa kwa uhalifu wa kiraia kuhukumiwa na korti za kifalme kupitia sheria ya Criminous Clerks. Becket alipinga, akisema kanisa pekee ndilo lililokuwa na mamlaka ya kuwahukumu.

TATU: Becket alipinga kodi za kifalme kwa makasisi

Baada ya kuona Askofu Thomas Becket amekuwa kero kwake, Mfalme II aliwaambia askari wake "Will no one rid me of this turbulent priest?" Desemba 29, 1170, askari wanne walikwenda Canterbury na kumuua Becket kwa upanga ndani ya kanisa wakati ibada ya jioni inafanyika. Thomas Becket Alitangazwa mtakatifu na Papa Alexander III mwaka 1173.

Mwaka 1174 baada shinikizo kubwa kutoka kwa Papa Alexander III na umma wa Kikristo, Henry II alisafiri hadi kanisa kuu la Canterbury Cathedral (mahali ambapo Becket aliuawa) akiwa mguu peku, akiwa na mavazi ya toba ya kanzu ya kitawa, na alikubali kupigwa mijeledi na watawa kama ishara ya kutubu. Aidha Henry alikubali kuachana na baadhi ya mamlaka yake dhidi ya Kanisa, na kuruhusu baadhi ya haki za kanisa ambazo alikuwa akizizuia kabla ya mauaji ya Becket.

Msimamo wa Injili juu uhusiano wa kanisa na serikali ni "Mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu" (Mathayo 22:21) .
Nani atuondolee Askofu msumbufu?
Kanisa wakati huo lilikuwa na nguvu kubwa tungefananisha na CCM hapa ila siyo hivyo vikanisha njaa vya siku hizi
 
Najua wenye Nia mbaya na huyu mama Kuna jambo kuuubwa mnajaribu Kila Hali kumtengenezea Ili akwame......mtashindwa mara bilioni kama mlivyomshindwa mpaka Sasa. Baada ya nrne yenu kukwama Sasa mnageukia kwa Kasi kwenye udini na huko mmeona mumchonganishe na kanisa (Wakristo wote).
Tanzania hakuna vita yoyote kati ya kanisa na serikali. Poleni sana.
Mjinga mkubwa wewe. Unafikiri kila vita lazima iwe na milio ya bunduki?
 
Back
Top Bottom