FOR 2015
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 538
- 221
Ndugu wana JF. Salaam kwenu
....'Tumevamiwa; Mwendawazimu ametuvamia, sasa tutampiga. Nia ya kumpiga tunayo, Uwezo wa kumpiga tunao na sababu ya kumpiga tunayo'.
Ndugu, hayo yalikuwa ni maneno mazito ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa tayari kuingia vitani dhidi ya Nduli Iddi Amin 'Dada'. Nimeikumbuka kauli hii baada ya takribani siku kadhaa kuwa zimepita tunaendelea kusikia Chokochoko za Wasioitakia mema Tanzania kutaka Vita na Rwanda. Hili kwa mtazamo wangu halikubaliki kwa sababu zifuatazo;
Mosi; Tanzania haina sababu hata moja ya kuivamia Rwanda, hata moja nasisitiza. Hoja za walio wengi zimelenga katika CHUKI BINAFSI dhidi ya Kagame,,basi,,hakuna sababu nyingine. Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa ushauri kwa Kagame na Kagame akajibu mbovu, basi. Inaishia hapo, sio sababu tosha ya kutufanya tuingie vitani. VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.
Mbili; Wengi na hasa wanaoshabikia Tanzania kutaka kuingia Vitani ni watu baki, hawana maslahi hata Chembe na Mkoa wa Kagera na hawajui hata Makaburi ya Wahaya waliofariki miaka ya 1978-1980 wakati wa Vita ya Kagera yakoje. Hawakuwahi KULIA hawa; hawakuwahi kumlilia mtu aliyekufa kwa risasi, wamezoea kulilia watu wanaokufa kwa magonjwa ya kawaida. Kabla hawajaanza kushabikia mimi naita UWENDAWAZIMU huu watembee Makaburi ya Wahaya waliokufa katika Vita ya Kagera, hakika wataacha ushabiki usiokuwa na msingi. VITA YA UGANDA SAWA...VITA NA RWANDA HAPANA.
Tatu; Kiuchumi moja kati ya Mikoa iliyokuwa inaendelea kwa kasi ya ajabu baada ya kupata Uhuru ilikuwa ni Mkoa wa Kagera, baada ya Vita ya Uganda kila kitu kilienda SHAGHALABAGHALA. Unajua kwa nini? Sababu nguvu kazi kubwa (Vijana) iliuawa katika vita na wengine kukimbia makazi yao. Wala Serikali haikuwahi kufanya Juhudi Binafsi kuupa kipaumbele Mkoa wa Kagera kwa sababu ya madhara yaliyopatikana kutokana na vita hiyo. Katika vita hiyo kulikuwa na kujitolea kwingi lakini kwa sababu ya Vita yenyewe uwanja wa vita ilikuwa ni Kagera, Wahaya wengi ndio waliojitokeza. Maana ya hili ni kwamba, Endapo Serikali itataka kukidhi MIHEMKO ya WAJINGA wachache wanaopenda vita, bado Uwanja wa Vita Utakuwa Kagera. VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.
Nne, Vifo,,Enyi mashabiki wa vita na Rwanda, jamani mnataka tena Bibi, Babu, Kaka, Dada, Shangazi, Wajomba na wadogo zetu wauawe?. Ndiyo furaha yenu? Tuambieni? Msitukumbushe mbali, msitukumbushe vilio, Simanzi na majonzi. Hapana, tunasema HAPANA. Nyie waandishi msiokuwa na Ndugu huko Bukoba mtuachie Ndugu zetu waishi maana nao wanayo haki ya kuishi kama mlivyo nyie katika maofisi yenu huko Dar es Salaam. Yaani mnaamini kuwa itakuwa ni sisi kuua tu bila kuuawa? Wahaya tunasema VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.
Tano, Mgawanyiko, ukijaribu kufuatilia kwa karibu unagundua kuwa kuna mgawanyiko Mkubwa sana kati ya wanaotaka vita na Rwanda na wale wasioitaka ambapo mimi naangukia katika kundi la pili. Hii kitu katika medani za vita, haiwezi kuifanya Tanzania kushinda Vita hiyo kama tunavyojitia moyo. Hakika tunajidanganya, tunafanya Propaganda za kitoto, tunacheza ngoma tukiwa uchi, tuache Ujinga. Tuache kabisa kuwaogopesha Wananchi wetu kwa maslahi ya Damu za Wahaya, Hapana hatutakubali. Wahaya kwa mara nyingine tunasema na kusisitiza VITA YA UGANDA SAWA,,VITA NA RWANDA HAPANA.
Mwisho, Sababu kubwa iliyotufanya tuingie Vitani na Uganda wakati huo ni Uvamizi wa Ghafla uliokuwa umefanywa na Iddi Amin kwa Tanzania akitaka kuichukua Ardhi ya Kagera. Naamini hii ni sababu kubwa sana ndio maana Mwalimu alimuita Iddi Amin MWENDAWAZIMU maana ni Mwendawazimu pekee anayeweza kuingia Nyumbani kwako, akataka kuingia hadi jikoni na hatimaye Chumbani baadaye kabatini na uvunguni. Je Rwanda na Kagame wamefanya nini?.. Kuichukua Ardhi ya Kagera kulimaanisha kuwafanya Wahaya wawe Sehemu ya Uganda, Kufanya Visiwa karibu 27 vilivyo Ziwa Victoria upande wa Kagera viwe Upande wa Uganda, Ndizi nzuri zote unazozijua Tanzania ziwe Upande wa Uganda; kiukweli hili lilikuwa halikubaliki, ndio maana tukatengeneza NIA na SABABU baada ya kuongezewa UWEZO kutoka RUSSIA. Kwa sasa Rwanda na Kagame wao hawajatukosea kitu na kwa hiyo tunasema VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.
Ushauri, Wale wote wanaoshabikia vita na Rwanda hasa kwa wakati huu, wangejikita zaidi katika kuhakikisha Tunajenga Uzalendo miongoni mwa Watanzania ili kuwa na Maendeleo endelevu na pia kuipenda nchi yao. Tumshauri Mheshimiwa Rais atimize wajibu wake wa Kuwaletea Watanzania Maendeleo badala ya kuja na WISH WASH ideas. Tujikite katika kuhakikisha tunakuwa na Katiba bora itakayotupa Mwelekeo Mzuri wa Taifa letu. Tumwambie Mheshimiwa Rais na washauri wake Wapeleke Huduma za Jamii kama Hospitali, Shule, Maji, Barabara kule vijijini ambapo hawajui hata Mpaka wa Tanzania na Rwanda ukoje. Tuwaambie Wabunge wajali maslahi ya Wananchi, watimize ahadi zao. Tukifanya hivyo hakika tutafika.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI KAGERA (BUKOBA)