Vita ya Uganda sawa.....Rwanda hapana...Kagera tunasema hapana

Vita ya Uganda sawa.....Rwanda hapana...Kagera tunasema hapana

Mkuu nadhamiria tu kuwaonya hao Mashabiki wa Vita, wanamtuhumu Kagame kuwa anapenda Vita wakati wao ndo kwa maneno yao wanaishangilia. Watanzania tuwe makini na watu hawa, wasije kuwa wanatumika kuwarainisha viongozi wetu. Kuivamia nchi ya Mwenzio ni Makosa kisheria lazima tuelewe hivyo.

Hakuna kielelezo cha msingi kinacho thibitisha Rwanda kuivamia Tanzanai, Tanzania kuna kundi linalo pambiza vita Tena linaendela kukua Kila kukicha. Mimi ninawalaani sana na maandishi yao yatabaki uthibitisho siku itakapo fika. Wanaodhani vita ni mchezo wa kuigiza waendelee. Historia itasomwa
 
Khaa!! wewe ndiyo umepotea kabisa. Utawezaje kufanya yote hayo kama hakuna hakuna amani? Amani ni jambo pana sana. Unataka hawa wahamiaji haramu wajazane nchini kwetu hadi baadaye waanze kudai haki za uwenyeji kama inavyosemwa?? au na wewe ni mmoja wao??

Umesoma ukaelewa maoni ya mleta hoja? maelezo yako yanaonesha hujasoma wala hujamuelewa. Hebu rudia kuyasoma kwasababu amefafanua vizuri zaidi na kwa upana kuhusiana na madhara ya hiyo vita na kwamba hakuna sababu za msingi
wala manufaa yoyote, bado hujaelewa mpiga debe?
 
Rohombaya, Nikusahihishe najulikana kama FOR 2015. Pole kwa roho yako mbaya. Nimeshauri hakuna haja ya Serikali kuwasikiliza watu wenye roho mbaya kama yako ikaingia Mkenge na kuingia vitani maana hakuna sababu ya Msingi ya kufanya hivyo kwa sasa. Nataka kukumbusha mfano wa Mwalimu alioutoa akiwa anamtania Sir George Kahama kuhusu Umimi (EGOISM) alionao Mwanadamu. Ndege ilipopata Hitilafu Sir akasema My God, hali ilipoendelea kuwa mbaya akasema Mungu Wangu, ilipokaribia kudondoka akasema MUNGU WANGE,,,huyo kajirudia zake Bukoba kuna lugha tatu hapo. Mwalimu alitaka kuonesha umuhimu wa kuwa Wazalendo. Tatizo wewe na roho mbaya yako unadhani Uzalendo ni kwa Utanzania tu, HAPANA unatakiwa kuwa Mzalendo na kwa Kabila lako. Ndio maana tunaambiwa tukajenge kwetu au mtu akifariki watu wanaanza kuuliza Mnasafirisha au...

Ni ukweli usiofichika kuwa leo hii ninyi mnaohimiza vita mnajua kwa namna yoyote HAITAWAATHIRI. Majibu mabaya ya PK kwa JK hayawi sababu tosha ya Kuanzia Goma na Kuishia Kigali. Hizo ni chuki binafsi na habari ndo hiyo. Yaani unadhani Vita ikiianza wataoathirika ni Chunya, Mafia au Bariadi,,,wala ni Kagera...Sisi tunasema YA UGANDA SAWA... RWANDA HAPANA...Peleka kule roho mbaya yako
Khaa!! Safari ya kuelekea kwenye UTANZANIA bado sana. Anyway hata jamaa zako wanasema Mama Salma ni Mhutu :bored:
 
Wala serikali ya Tz haijatangaza vita na Rwanda! Acha woga ndugu yangu! Kama itabidi Rwanda tutaidunda! Pia ni dhana potofu kufikiri kuwa ni wahaya pekee ndo walikufa katika vita ya Kagera! Ni Watanzania wote walishiriki katika vita hiyo! Acha woga!

Nsabhi, Ni kweli kabisa kuwa Tanzania haijatangaza vita ila hizi Chokochoko za watu waroho wa Damu za Watu, ambao kila kukicha ni kuitia Kiburi Serikali ione Umuhimu wa kuingia Vitani ndo zinanitia Hofu na Mashaka. Hatuna sababu kabisa kwa vyovyote ya kuidunda Rwanda kwa sasa. Watanzania wengi walikufa wakati wa Vita na Uganda lakini Ukweli unabaki kuwa waliokufa wengi ni Wahaya, walioharibiwa mali zao ni wahaya, walikiombia makazi yao ni wahaya. Hii nayo kama waroho wa damu za watu watakavyo ikitokea ni hukohuko kwa Wahaya. Kagera imewakosea nini? tunauliza tu?

Nitaendelea kuwa Muoga mpaka hawa Blood Suckers watakapoahamisha Mada na kuanza kutuletea habari za Maendeleo ya nchi yetu na namna ya kukabiliana na hali duni ya Maisha.
 
Siku hizi vita zinapiganiwa kwenye mitandao mkuu, wala usifikiri kuna kunguru wa kupigana karne hii, ukiona nchi inaingia vitani ujue kuna serious case not this one from PK and JK. Kwa hiyo maoni yangu ni kuwa, nawewe unaendeleza vita kati ya Rwanda na Tanzania. Kanusha kama ni uongo mkuu FOR 2015.
 
Umesoma ukaelewa maoni ya mleta hoja? maelezo yako yanaonesha hujasoma wala hujamuelewa. Hebu rudia kuyasoma kwasababu amefafanua vizuri zaidi na kwa upana kuhusiana na madhara ya hiyo vita na kwamba hakuna sababu za msingi
wala manufaa yoyote, bado hujaelewa mpiga debe?
Khaa!! wewe ndiyo hujamuelewa. hakuna cha zaidi alichokieleza zaidi ya kuuweka mbele Uhaya mbele kuliko Utaifa. Kwa akili yako unadhani mbadala ya tatizo kati ya Rwanda na Tanzania ni kutengeneza katiba nzuri na kupeleka huduma za maendeleo vijijini?? Hivi nyie ni watu wa wapi hasa??
 
Tanzania hawana mpango wowote wa kupigana na Rwanda wala hakuna anaetaka Tz ivamie Rwanda.Aliye tufikisha hapa ni Kagame.Chokochoko zote zinaletelezwa na Kagame usingekuwa upuuzi wa Kagame majeshi yetu yasinge pelekwa Kongo hata wewe mwenyewe usingethubutu kuandika hiki ulicho kiandika Jk naye hangetoa ushauri ule alioutoa kwa Kagame hata wale wanao onekana kuwa na mtazamo wa kivita na Rwanda ni Kagame ndiye kasababisha mtazamo huo.Vita ya Uganda na Tz haikuibuka ghafula tu zilianza chokochoko kidogokidogo kama alivyoanza Kagame hatimaye Id amini akaivamia Tz.Na kuifanya Tz kupigana vita ambavyo haikutegemea kupigana.Kagame naye kaanza kutishia kumpiga Jk na anaposema kuwa atamchapa haina maana kwamba ataruka moja kwa moja mpaka magogoni kwa Jk ni lazima kwanza ataanza kuishambulia nchi yetu kwa kupitia Ngara,B'mlo,Karagwe au anaweza akatumia mbinu nyingine yoyote ile ya kutimiza malengo yeke.Amini alipigwa kwa sababu aliivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera na ni ukweli usiyopingika kuwa mkoa wa Kagera uliathirika sana na vita hivyo pamoja na watanzania wote kwa ujumla.Kagame tayari ameshaonyesha nia tayari ya kuichapa Tz.Je atakapo ivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera asipigwe kwa sababu wahaya wa Kagera na mkoa wa Kagera kwa ujumla wao wataathirika?au tusubiri auchukuwe mkoa wa Kagera apite Mwanza,Shinyanga na Majeshi yetu yamsubiri mikoa ya kati ndipo waanze kupambana naye ili kuepusha athari kwa mkoa wa Kagera?au pengine uvamizi wake hauta kuwa na athari yote kwa mkoa wa Kagera labda akiachwa Kagera risasi zake zitakuwa haziuwi pengine mabomu na risasi za wtz ndizo zitakazo kuwa zinaua peke yake.
 
Tanzania inahitaji wazando wa aina ya FOR 2015, tunahitaji kuangalia miundombinu yetu kwa ujumla wake ilikuijenga tanazania bora yenye matumain hasa kwa siku zijazo.

Ngoja niwaite washabiki wa vita ambao kwao ufedhuli wa propaganda imeathili mishipa yao ya akili nakusahau madhara kama hayo hapo juu.

Manyerere Jackton , Alumbwagweumutwa , Manyerere Jackton, Mauza uza , Tambala , kidole007 , stroke , mokala1989 , [MENTION]NattyDread[/MENTION], Mwamakula , makoye78 , Lilambo , thatha , Rutunga M

Mimi hujanitaja,nakuja mwenyewe...they ve' heard ur call hasa manyerere naona ana speed up kuja upande huu.lol
 
Last edited by a moderator:
Khaa!! FOR 2013 yaani wewe ni kunguru kweli. Nani katangaza vita? Unalialia tu bure. Unamaaana hata kama PK akimhit JK kama alivyoahidi basi tumuangalie tu?? Hivi kipi bora kwako kati ya Kagera kuwa sehemu ya Rwanda au Kagera kuwa battlefield ili iokolewe? Usiwe mjinga kwa kutanguliza UHAYA mbele kuliko UTANZANIA. Hata hivyo kwa akili yako kama ikitokea vita kati ya Rwanda na Tanzania unadhani itapiganiwa Mafia au Chunya au Bariadi??

UHAYAN kuna msemo "eibala libi liita nyinalyo" maana yake jina baya umuua mwenye nalo ={ GIVE THE DOG A BAD NAME AND KILL }
kwel wewe ni roho mbaya kwan kimjazacho mtu ndo kimtokacho

kwa akil yako ndogo unafikir vita na rwanda waathirika wakubwa na wa kwanza watakuwa wapi?
Ukikaa karibu na ua la warid lazima utanukia uwarid.vita ya kipuuz na rwanda waathirika wa kwanza ni wana Kagera.

Leo hii kagera kuna wajane,wagane,yatima,vilema, watu wamekuwa maskin wa kupindukia kwa sababu walipoteza kilakitu kwenye vita na Uganda ambayo kwel ililenga kuwa komboa kutoka kwa nduli Amin Dada.hiyo vita sawa lakin kupigana na rwanda kwa sababu hizi zilizopo ni uendawazimu.

Jk ulimshaur Pk aongee na waasi nasi WANAKAGERA tunakutaka Jk ukaongee na Pk mu yamalize,wana kagera tunataka maji,barabara,umeme,shule,hospitals na maisha bora kama ulivyo tuahid 2005 na si vita.

Wale wapenda vita refer watu wa dar walivyo haha ktk mabomu ya mbagala na gongo la mboto na hadi leo watu wanalala nje na wamepoteza mwelekeo wa maisha sasa fikir ikiwa vita je?

VITA NA UGANDA SAWA LAKIN VITA NA RWANDA HAPANA!
 
Ndugu wana JF. Salaam kwenu

....'Tumevamiwa; Mwendawazimu ametuvamia, sasa tutampiga. Nia ya kumpiga tunayo, Uwezo wa kumpiga tunao na sababu ya kumpiga tunayo'.

Ndugu, hayo yalikuwa ni maneno mazito ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa tayari kuingia vitani dhidi ya Nduli Iddi Amin 'Dada'. Nimeikumbuka kauli hii baada ya takribani siku kadhaa kuwa zimepita tunaendelea kusikia Chokochoko za Wasioitakia mema Tanzania kutaka Vita na Rwanda. Hili kwa mtazamo wangu halikubaliki kwa sababu zifuatazo;

Mosi; Tanzania haina sababu hata moja ya kuivamia Rwanda, hata moja nasisitiza. Hoja za walio wengi zimelenga katika CHUKI BINAFSI dhidi ya Kagame,,basi,,hakuna sababu nyingine. Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa ushauri kwa Kagame na Kagame akajibu mbovu, basi. Inaishia hapo, sio sababu tosha ya kutufanya tuingie vitani. VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.

Mbili; Wengi na hasa wanaoshabikia Tanzania kutaka kuingia Vitani ni watu baki, hawana maslahi hata Chembe na Mkoa wa Kagera na hawajui hata Makaburi ya Wahaya waliofariki miaka ya 1978-1980 wakati wa Vita ya Kagera yakoje. Hawakuwahi KULIA hawa; hawakuwahi kumlilia mtu aliyekufa kwa risasi, wamezoea kulilia watu wanaokufa kwa magonjwa ya kawaida. Kabla hawajaanza kushabikia mimi naita UWENDAWAZIMU huu watembee Makaburi ya Wahaya waliokufa katika Vita ya Kagera, hakika wataacha ushabiki usiokuwa na msingi. VITA YA UGANDA SAWA...VITA NA RWANDA HAPANA.

Tatu; Kiuchumi moja kati ya Mikoa iliyokuwa inaendelea kwa kasi ya ajabu baada ya kupata Uhuru ilikuwa ni Mkoa wa Kagera, baada ya Vita ya Uganda kila kitu kilienda SHAGHALABAGHALA. Unajua kwa nini? Sababu nguvu kazi kubwa (Vijana) iliuawa katika vita na wengine kukimbia makazi yao. Wala Serikali haikuwahi kufanya Juhudi Binafsi kuupa kipaumbele Mkoa wa Kagera kwa sababu ya madhara yaliyopatikana kutokana na vita hiyo. Katika vita hiyo kulikuwa na kujitolea kwingi lakini kwa sababu ya Vita yenyewe uwanja wa vita ilikuwa ni Kagera, Wahaya wengi ndio waliojitokeza. Maana ya hili ni kwamba, Endapo Serikali itataka kukidhi MIHEMKO ya WAJINGA wachache wanaopenda vita, bado Uwanja wa Vita Utakuwa Kagera. VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.

Nne, Vifo,,Enyi mashabiki wa vita na Rwanda, jamani mnataka tena Bibi, Babu, Kaka, Dada, Shangazi, Wajomba na wadogo zetu wauawe?. Ndiyo furaha yenu? Tuambieni? Msitukumbushe mbali, msitukumbushe vilio, Simanzi na majonzi. Hapana, tunasema HAPANA. Nyie waandishi msiokuwa na Ndugu huko Bukoba mtuachie Ndugu zetu waishi maana nao wanayo haki ya kuishi kama mlivyo nyie katika maofisi yenu huko Dar es Salaam. Yaani mnaamini kuwa itakuwa ni sisi kuua tu bila kuuawa? Wahaya tunasema VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.

Tano, Mgawanyiko, ukijaribu kufuatilia kwa karibu unagundua kuwa kuna mgawanyiko Mkubwa sana kati ya wanaotaka vita na Rwanda na wale wasioitaka ambapo mimi naangukia katika kundi la pili. Hii kitu katika medani za vita, haiwezi kuifanya Tanzania kushinda Vita hiyo kama tunavyojitia moyo. Hakika tunajidanganya, tunafanya Propaganda za kitoto, tunacheza ngoma tukiwa uchi, tuache Ujinga. Tuache kabisa kuwaogopesha Wananchi wetu kwa maslahi ya Damu za Wahaya, Hapana hatutakubali. Wahaya kwa mara nyingine tunasema na kusisitiza VITA YA UGANDA SAWA,,VITA NA RWANDA HAPANA.

Mwisho, Sababu kubwa iliyotufanya tuingie Vitani na Uganda wakati huo ni Uvamizi wa Ghafla uliokuwa umefanywa na Iddi Amin kwa Tanzania akitaka kuichukua Ardhi ya Kagera. Naamini hii ni sababu kubwa sana ndio maana Mwalimu alimuita Iddi Amin MWENDAWAZIMU maana ni Mwendawazimu pekee anayeweza kuingia Nyumbani kwako, akataka kuingia hadi jikoni na hatimaye Chumbani baadaye kabatini na uvunguni. Je Rwanda na Kagame wamefanya nini?.. Kuichukua Ardhi ya Kagera kulimaanisha kuwafanya Wahaya wawe Sehemu ya Uganda, Kufanya Visiwa karibu 27 vilivyo Ziwa Victoria upande wa Kagera viwe Upande wa Uganda, Ndizi nzuri zote unazozijua Tanzania ziwe Upande wa Uganda; kiukweli hili lilikuwa halikubaliki, ndio maana tukatengeneza NIA na SABABU baada ya kuongezewa UWEZO kutoka RUSSIA. Kwa sasa Rwanda na Kagame wao hawajatukosea kitu na kwa hiyo tunasema VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA.

Ushauri, Wale wote wanaoshabikia vita na Rwanda hasa kwa wakati huu, wangejikita zaidi katika kuhakikisha Tunajenga Uzalendo miongoni mwa Watanzania ili kuwa na Maendeleo endelevu na pia kuipenda nchi yao. Tumshauri Mheshimiwa Rais atimize wajibu wake wa Kuwaletea Watanzania Maendeleo badala ya kuja na WISH WASH ideas. Tujikite katika kuhakikisha tunakuwa na Katiba bora itakayotupa Mwelekeo Mzuri wa Taifa letu. Tumwambie Mheshimiwa Rais na washauri wake Wapeleke Huduma za Jamii kama Hospitali, Shule, Maji, Barabara kule vijijini ambapo hawajui hata Mpaka wa Tanzania na Rwanda ukoje. Tuwaambie Wabunge wajali maslahi ya Wananchi, watimize ahadi zao. Tukifanya hivyo hakika tutafika.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI KAGERA (BUKOBA)

Sidhani kama Tanzania itaanzisha vita na Rwanda. Lakini Rwanda itavamia Tanzania, bila shaka lazima ijibiwe hilo halikwepeki
 
UHAYAN kuna msemo "eibala libi liita nyinalyo" maana yake jina baya umuua mwenye nalo ={ GIVE THE DOG A BAD NAME AND KILL }
kwel wewe ni roho mbaya kwan kimjazacho mtu ndo kimtokacho

kwa akil yako ndogo unafikir vita na rwanda waathirika wakubwa na wa kwanza watakuwa wapi?
Ukikaa karibu na ua la warid lazima utanukia uwarid.vita ya kipuuz na rwanda waathirika wa kwanza ni wana Kagera.

Leo hii kagera kuna wajane,wagane,yatima,vilema, watu wamekuwa maskin wa kupindukia kwa sababu walipoteza kilakitu kwenye vita na Uganda ambayo kwel ililenga kuwa komboa kutoka kwa nduli Amin Dada.hiyo vita sawa lakin kupigana na rwanda kwa sababu hizi zilizopo ni uendawazimu.

Jk ulimshaur Pk aongee na waasi nasi WANAKAGERA tunakutaka Jk ukaongee na Pk mu yamalize,wana kagera tunataka maji,barabara,umeme,shule,hospitals na maisha bora kama ulivyo tuahid 2005 na si vita.

Wale wapenda vita refer watu wa dar walivyo haha ktk mabomu ya mbagala na gongo la mboto na hadi leo watu wanalala nje na wamepoteza mwelekeo wa maisha sasa fikir ikiwa vita je?

VITA NA UGANDA SAWA LAKIN VITA NA RWANDA HAPANA!
khaa!! kumbe akili yako fupi sana. Vita huwa na sababu. Kwa akili yako unataka hata kama Rwanda wakituhit (kwani hadi sasa wanasubiria wapate fursa ya kulitekeleza hilo) basi tukae tu tukiwaimbia "eibala libi liita nyinalyo" huku tukiwapigia makofi na kuwashangilia?? Hili jingine angalau unajua kama waathirika wa kwanza wa uhamiaji haramu ni watu wa Kagera. JK hana cha kuzungumza na PK alitoa ushauri wake tu basi kuufuata au kuuacha ni haki yake PK :bored:
 
Hakuna kielelezo cha msingi kinacho thibitisha Rwanda kuivamia Tanzanai, Tanzania kuna kundi linalo pambiza vita Tena linaendela kukua Kila kukicha. Mimi ninawalaani sana na maandishi yao yatabaki uthibitisho siku itakapo fika. Wanaodhani vita ni mchezo wa kuigiza waendelee. Historia itasomwa

You are very right Herod Masud no Proof, no Reasons to guarentee the War with Rwanda. Just Few War Lovers always exaggerrating things and Issues. We should in one Voice as Tanzania Family SAY NO TO THEM. TANZANIANS DON'T WANT WAR WITH RWANDA
 
kuna watu wanashabikia vita wakat vita vikianza mtaanza kula ugali wa dona,vita si nzuri asa kwa uchumi wetu ulivyo chini,watanzania ni masikin sana,sio wakat muafaka wa vita
 
Sobonike, Exactly....Kuigusa Ardhi ya Tanzania huo utakuwa ni UWENDAWAZIMU uliopitiliza. Hata mimi hutaniona kamwe nikiwa Against hawa Mashabiki wa vita. Kwa sasa hakuna sababu na kweli hakuna sababu
 
kuna watu wanashabikia vita wakat vita vikianza mtaanza kula ugali wa dona,vita si nzuri asa kwa uchumi wetu ulivyo chini,watanzania ni masikin sana,sio wakat muafaka wa vita

Money Stunna, Si tu Ugali wa dona hata maji ya kuoga watayakosa, vikwapa vitawanuka siku zote za vita na mbaya zaidi Harufu ya Damu itawafuata kokote watakakokwenda. TUWAKEMEE KWA NGUVU ZOTE
 
Money Stunna, Si tu Ugali wa dona hata maji ya kuoga watayakosa, vikwapa vitawanuka siku zote za vita na mbaya zaidi Harufu ya Damu itawafuata kokote watakakokwenda. TUWAKEMEE KWA NGUVU ZOTE

vita ya tanzania na uganda,tanzania ilitumia zaidi ya trillion 1,ebu fikiria kwa mwaka 1978 pesa ilivyokuwa na thamani harafu tukatumia pesa zote hizo,na mbaya zaidi nchi za ulaya zitatukopesha pesa kwa riba kubwa sana kwa sababu ya mahitaj tutakopa hizo siraha,nchi ni masikin sana hii,bajet yetu kwa miaka 2 aifikii ata pesa za mmiliki wa chelsea
 
Tanzania hawana mpango wowote wa kupigana na Rwanda wala hakuna anaetaka Tz ivamie Rwanda.Aliye tufikisha hapa ni Kagame.Chokochoko zote zinaletelezwa na Kagame usingekuwa upuuzi wa Kagame majeshi yetu yasinge pelekwa Kongo hata wewe mwenyewe usingethubutu kuandika hiki ulicho kiandika Jk naye hangetoa ushauri ule alioutoa kwa Kagame hata wale wanao onekana kuwa na mtazamo wa kivita na Rwanda ni Kagame ndiye kasababisha mtazamo huo.Vita ya Uganda na Tz haikuibuka ghafula tu zilianza chokochoko kidogokidogo kama alivyoanza Kagame hatimaye Id amini akaivamia Tz.Na kuifanya Tz kupigana vita ambavyo haikutegemea kupigana.Kagame naye kaanza kutishia kumpiga Jk na anaposema kuwa atamchapa haina maana kwamba ataruka moja kwa moja mpaka magogoni kwa Jk ni lazima kwanza ataanza kuishambulia nchi yetu kwa kupitia Ngara,B'mlo,Karagwe au anaweza akatumia mbinu nyingine yoyote ile ya kutimiza malengo yeke.Amini alipigwa kwa sababu aliivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera na ni ukweli usiyopingika kuwa mkoa wa Kagera uliathirika sana na vita hivyo pamoja na watanzania wote kwa ujumla.Kagame tayari ameshaonyesha nia tayari ya kuichapa Tz.Je atakapo ivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera asipigwe kwa sababu wahaya wa Kagera na mkoa wa Kagera kwa ujumla wao wataathirika?au tusubiri auchukuwe mkoa wa Kagera apite Mwanza,Shinyanga na Majeshi yetu yamsubiri mikoa ya kati ndipo waanze kupambana naye ili kuepusha athari kwa mkoa wa Kagera?au pengine uvamizi wake hauta kuwa na athari yote kwa mkoa wa Kagera labda akiachwa Kagera risasi zake zitakuwa haziuwi pengine mabomu na risasi za wtz ndizo zitakazo kuwa zinaua peke yake.

Tukundane, Ni kweli Tanzani haina Mpango na Vita na hata Rwanda haina Mpango wa vita. Hapa tunawakemea Blood Suckers wanaopenda kuona Vita ikipiganwa tena Tanzania ikiwa ndio Mchokozi. Haiingii akilini Mtu analeta Mihemko kwa Serikali ili ione haja ya kuingia katika vita. Kama tuko Wise Enough tungempuuza huyo PK. Mbona Mheshiwa Rais aliongea vizuri wakati wa hotuba yake kuhusu Rwanda, kwa nini Individuals wanataka kujifanya wako faasta sana katika hili suala. Diplomasia iko wapi. VITA HAPANA
 
UHAYAN kuna msemo "eibala libi liita nyinalyo" maana yake jina baya umuua mwenye nalo ={ GIVE THE DOG A BAD NAME AND KILL }
kwel wewe ni roho mbaya kwan kimjazacho mtu ndo kimtokacho

kwa akil yako ndogo unafikir vita na rwanda waathirika wakubwa na wa kwanza watakuwa wapi?
Ukikaa karibu na ua la warid lazima utanukia uwarid.vita ya kipuuz na rwanda waathirika wa kwanza ni wana Kagera.

Leo hii kagera kuna wajane,wagane,yatima,vilema, watu wamekuwa maskin wa kupindukia kwa sababu walipoteza kilakitu kwenye vita na Uganda ambayo kwel ililenga kuwa komboa kutoka kwa nduli Amin Dada.hiyo vita sawa lakin kupigana na rwanda kwa sababu hizi zilizopo ni uendawazimu.

Jk ulimshaur Pk aongee na waasi nasi WANAKAGERA tunakutaka Jk ukaongee na Pk mu yamalize,wana kagera tunataka maji,barabara,umeme,shule,hospitals na maisha bora kama ulivyo tuahid 2005 na si vita.

Wale wapenda vita refer watu wa dar walivyo haha ktk mabomu ya mbagala na gongo la mboto na hadi leo watu wanalala nje na wamepoteza mwelekeo wa maisha sasa fikir ikiwa vita je?

VITA NA UGANDA SAWA LAKIN VITA NA RWANDA HAPANA!

Mutahappy, Tena hawa wanaochagiza Serikali ya Tanzania iingie vitani kwa sababu wengi kama sio wote wanaishi Dar, vema wakakumbuka tu Hemwahemwa ya Mbagala na Gongo la Mboto. Sasa iweje wafurahie Wenzao wa Kagera. NO PLEASE, GIVE US A BREAK. Hizo damu mnazozitamani kachinje Ng'ombe, Mbuzi, Kuku hata Kondoo mnywe. Msiichochee Serikali. Haka ka Amani tuliki nako kanatosha. Tuache Tupumue
 
asante mkuu.JF ni sehemu ya great thinkers kama wewe mkuu.Kuna watu wanlifikiri hapa kuna watu wasio ona mbali.Mkuu asante sana kwa kuwa kati ya wana amani wazuri hapa JF.
 
Back
Top Bottom