Vita ya Uganda sawa.....Rwanda hapana...Kagera tunasema hapana



Hakuna kielelezo cha msingi kinacho thibitisha Rwanda kuivamia Tanzanai, Tanzania kuna kundi linalo pambiza vita Tena linaendela kukua Kila kukicha. Mimi ninawalaani sana na maandishi yao yatabaki uthibitisho siku itakapo fika. Wanaodhani vita ni mchezo wa kuigiza waendelee. Historia itasomwa
 

Umesoma ukaelewa maoni ya mleta hoja? maelezo yako yanaonesha hujasoma wala hujamuelewa. Hebu rudia kuyasoma kwasababu amefafanua vizuri zaidi na kwa upana kuhusiana na madhara ya hiyo vita na kwamba hakuna sababu za msingi
wala manufaa yoyote, bado hujaelewa mpiga debe?
 
Khaa!! Safari ya kuelekea kwenye UTANZANIA bado sana. Anyway hata jamaa zako wanasema Mama Salma ni Mhutu :bored:
 
Wala serikali ya Tz haijatangaza vita na Rwanda! Acha woga ndugu yangu! Kama itabidi Rwanda tutaidunda! Pia ni dhana potofu kufikiri kuwa ni wahaya pekee ndo walikufa katika vita ya Kagera! Ni Watanzania wote walishiriki katika vita hiyo! Acha woga!

Nsabhi, Ni kweli kabisa kuwa Tanzania haijatangaza vita ila hizi Chokochoko za watu waroho wa Damu za Watu, ambao kila kukicha ni kuitia Kiburi Serikali ione Umuhimu wa kuingia Vitani ndo zinanitia Hofu na Mashaka. Hatuna sababu kabisa kwa vyovyote ya kuidunda Rwanda kwa sasa. Watanzania wengi walikufa wakati wa Vita na Uganda lakini Ukweli unabaki kuwa waliokufa wengi ni Wahaya, walioharibiwa mali zao ni wahaya, walikiombia makazi yao ni wahaya. Hii nayo kama waroho wa damu za watu watakavyo ikitokea ni hukohuko kwa Wahaya. Kagera imewakosea nini? tunauliza tu?

Nitaendelea kuwa Muoga mpaka hawa Blood Suckers watakapoahamisha Mada na kuanza kutuletea habari za Maendeleo ya nchi yetu na namna ya kukabiliana na hali duni ya Maisha.
 
Siku hizi vita zinapiganiwa kwenye mitandao mkuu, wala usifikiri kuna kunguru wa kupigana karne hii, ukiona nchi inaingia vitani ujue kuna serious case not this one from PK and JK. Kwa hiyo maoni yangu ni kuwa, nawewe unaendeleza vita kati ya Rwanda na Tanzania. Kanusha kama ni uongo mkuu FOR 2015.
 
Khaa!! wewe ndiyo hujamuelewa. hakuna cha zaidi alichokieleza zaidi ya kuuweka mbele Uhaya mbele kuliko Utaifa. Kwa akili yako unadhani mbadala ya tatizo kati ya Rwanda na Tanzania ni kutengeneza katiba nzuri na kupeleka huduma za maendeleo vijijini?? Hivi nyie ni watu wa wapi hasa??
 
Tanzania hawana mpango wowote wa kupigana na Rwanda wala hakuna anaetaka Tz ivamie Rwanda.Aliye tufikisha hapa ni Kagame.Chokochoko zote zinaletelezwa na Kagame usingekuwa upuuzi wa Kagame majeshi yetu yasinge pelekwa Kongo hata wewe mwenyewe usingethubutu kuandika hiki ulicho kiandika Jk naye hangetoa ushauri ule alioutoa kwa Kagame hata wale wanao onekana kuwa na mtazamo wa kivita na Rwanda ni Kagame ndiye kasababisha mtazamo huo.Vita ya Uganda na Tz haikuibuka ghafula tu zilianza chokochoko kidogokidogo kama alivyoanza Kagame hatimaye Id amini akaivamia Tz.Na kuifanya Tz kupigana vita ambavyo haikutegemea kupigana.Kagame naye kaanza kutishia kumpiga Jk na anaposema kuwa atamchapa haina maana kwamba ataruka moja kwa moja mpaka magogoni kwa Jk ni lazima kwanza ataanza kuishambulia nchi yetu kwa kupitia Ngara,B'mlo,Karagwe au anaweza akatumia mbinu nyingine yoyote ile ya kutimiza malengo yeke.Amini alipigwa kwa sababu aliivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera na ni ukweli usiyopingika kuwa mkoa wa Kagera uliathirika sana na vita hivyo pamoja na watanzania wote kwa ujumla.Kagame tayari ameshaonyesha nia tayari ya kuichapa Tz.Je atakapo ivamia Tz kwa kupitia mkoa wa Kagera asipigwe kwa sababu wahaya wa Kagera na mkoa wa Kagera kwa ujumla wao wataathirika?au tusubiri auchukuwe mkoa wa Kagera apite Mwanza,Shinyanga na Majeshi yetu yamsubiri mikoa ya kati ndipo waanze kupambana naye ili kuepusha athari kwa mkoa wa Kagera?au pengine uvamizi wake hauta kuwa na athari yote kwa mkoa wa Kagera labda akiachwa Kagera risasi zake zitakuwa haziuwi pengine mabomu na risasi za wtz ndizo zitakazo kuwa zinaua peke yake.
 

Mimi hujanitaja,nakuja mwenyewe...they ve' heard ur call hasa manyerere naona ana speed up kuja upande huu.lol
 
Last edited by a moderator:

UHAYAN kuna msemo "eibala libi liita nyinalyo" maana yake jina baya umuua mwenye nalo ={ GIVE THE DOG A BAD NAME AND KILL }
kwel wewe ni roho mbaya kwan kimjazacho mtu ndo kimtokacho

kwa akil yako ndogo unafikir vita na rwanda waathirika wakubwa na wa kwanza watakuwa wapi?
Ukikaa karibu na ua la warid lazima utanukia uwarid.vita ya kipuuz na rwanda waathirika wa kwanza ni wana Kagera.

Leo hii kagera kuna wajane,wagane,yatima,vilema, watu wamekuwa maskin wa kupindukia kwa sababu walipoteza kilakitu kwenye vita na Uganda ambayo kwel ililenga kuwa komboa kutoka kwa nduli Amin Dada.hiyo vita sawa lakin kupigana na rwanda kwa sababu hizi zilizopo ni uendawazimu.

Jk ulimshaur Pk aongee na waasi nasi WANAKAGERA tunakutaka Jk ukaongee na Pk mu yamalize,wana kagera tunataka maji,barabara,umeme,shule,hospitals na maisha bora kama ulivyo tuahid 2005 na si vita.

Wale wapenda vita refer watu wa dar walivyo haha ktk mabomu ya mbagala na gongo la mboto na hadi leo watu wanalala nje na wamepoteza mwelekeo wa maisha sasa fikir ikiwa vita je?

VITA NA UGANDA SAWA LAKIN VITA NA RWANDA HAPANA!
 

Sidhani kama Tanzania itaanzisha vita na Rwanda. Lakini Rwanda itavamia Tanzania, bila shaka lazima ijibiwe hilo halikwepeki
 
khaa!! kumbe akili yako fupi sana. Vita huwa na sababu. Kwa akili yako unataka hata kama Rwanda wakituhit (kwani hadi sasa wanasubiria wapate fursa ya kulitekeleza hilo) basi tukae tu tukiwaimbia "eibala libi liita nyinalyo" huku tukiwapigia makofi na kuwashangilia?? Hili jingine angalau unajua kama waathirika wa kwanza wa uhamiaji haramu ni watu wa Kagera. JK hana cha kuzungumza na PK alitoa ushauri wake tu basi kuufuata au kuuacha ni haki yake PK :bored:
 

You are very right Herod Masud no Proof, no Reasons to guarentee the War with Rwanda. Just Few War Lovers always exaggerrating things and Issues. We should in one Voice as Tanzania Family SAY NO TO THEM. TANZANIANS DON'T WANT WAR WITH RWANDA
 
kuna watu wanashabikia vita wakat vita vikianza mtaanza kula ugali wa dona,vita si nzuri asa kwa uchumi wetu ulivyo chini,watanzania ni masikin sana,sio wakat muafaka wa vita
 
Sobonike, Exactly....Kuigusa Ardhi ya Tanzania huo utakuwa ni UWENDAWAZIMU uliopitiliza. Hata mimi hutaniona kamwe nikiwa Against hawa Mashabiki wa vita. Kwa sasa hakuna sababu na kweli hakuna sababu
 
kuna watu wanashabikia vita wakat vita vikianza mtaanza kula ugali wa dona,vita si nzuri asa kwa uchumi wetu ulivyo chini,watanzania ni masikin sana,sio wakat muafaka wa vita

Money Stunna, Si tu Ugali wa dona hata maji ya kuoga watayakosa, vikwapa vitawanuka siku zote za vita na mbaya zaidi Harufu ya Damu itawafuata kokote watakakokwenda. TUWAKEMEE KWA NGUVU ZOTE
 
Money Stunna, Si tu Ugali wa dona hata maji ya kuoga watayakosa, vikwapa vitawanuka siku zote za vita na mbaya zaidi Harufu ya Damu itawafuata kokote watakakokwenda. TUWAKEMEE KWA NGUVU ZOTE

vita ya tanzania na uganda,tanzania ilitumia zaidi ya trillion 1,ebu fikiria kwa mwaka 1978 pesa ilivyokuwa na thamani harafu tukatumia pesa zote hizo,na mbaya zaidi nchi za ulaya zitatukopesha pesa kwa riba kubwa sana kwa sababu ya mahitaj tutakopa hizo siraha,nchi ni masikin sana hii,bajet yetu kwa miaka 2 aifikii ata pesa za mmiliki wa chelsea
 

Tukundane, Ni kweli Tanzani haina Mpango na Vita na hata Rwanda haina Mpango wa vita. Hapa tunawakemea Blood Suckers wanaopenda kuona Vita ikipiganwa tena Tanzania ikiwa ndio Mchokozi. Haiingii akilini Mtu analeta Mihemko kwa Serikali ili ione haja ya kuingia katika vita. Kama tuko Wise Enough tungempuuza huyo PK. Mbona Mheshiwa Rais aliongea vizuri wakati wa hotuba yake kuhusu Rwanda, kwa nini Individuals wanataka kujifanya wako faasta sana katika hili suala. Diplomasia iko wapi. VITA HAPANA
 

Mutahappy, Tena hawa wanaochagiza Serikali ya Tanzania iingie vitani kwa sababu wengi kama sio wote wanaishi Dar, vema wakakumbuka tu Hemwahemwa ya Mbagala na Gongo la Mboto. Sasa iweje wafurahie Wenzao wa Kagera. NO PLEASE, GIVE US A BREAK. Hizo damu mnazozitamani kachinje Ng'ombe, Mbuzi, Kuku hata Kondoo mnywe. Msiichochee Serikali. Haka ka Amani tuliki nako kanatosha. Tuache Tupumue
 
asante mkuu.JF ni sehemu ya great thinkers kama wewe mkuu.Kuna watu wanlifikiri hapa kuna watu wasio ona mbali.Mkuu asante sana kwa kuwa kati ya wana amani wazuri hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…