Vita ya Uganda sawa.....Rwanda hapana...Kagera tunasema hapana

Huna point wewe


 
Kama itatokea Rwanda atatandikwa basi atatandikwa na majeshi ya UN na sio Tanzania.
 

Mkuu WA-UKENYENGE, Sikupenda kabisa kuanzisha hii mada, imenibidi baada ya kuona kila uchao kuna Watanzania wenzetu wachache wanachagiza ili tuone Umuhimu wa Vita. This is Crazy, nikaona ni vema nitoe ya Moyoni wasije wakadhani tuko nyuma yao. Sure ni lazima tuwe na sababu za kutosha kuingia vitani. Ni upuuzi usiokuwa kifani Kuanza kujadili habari za Bahima na kuchomekea habari za kutaka vita.

Binafsi naamini sana katika kukaa kimya hasa katika masuala kama haya maana kuyaongea ndo kunaongeza zaidi Attention na wakati mwingine katika kuongea mtu usipokuwa makini unajichanganya. To be Frank after this I won't talk anymore on this issue. Ila ujumbe umewafikia wote Wachombezaji, wapenda vita wasiokuwa na Ndugu. Na nawaambia kamwe hila zao hazitafanikiwa. WE ARE FED UP. Wanaandika ili vita ikianza walipoti na hivyo kupata Faida katika kuuza habari. VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA
 
Mkuu safi sana,nimefurahi sana.vita vya maendeleo tumeshapigwa 10-0 hadi sasa hivi.eti tuingie kwenye vita.uchumi wetu ni dhaifu.Sina maana hatuna resources hapana.lakini nchi haina pesa kwani pesa inaingia kwa mafisadi wachache alafu tunataka vita.vita ni gharama .kwanini hiyo bajeti ya vita hisiende kwenye mashuleni,afya na kwenye miundo mbinu.Nakupongeza mkuu wewe ni mtu wa amani .GOD BLESS YOU
 
VITA HAIKUBALIKI. Lazima kila juhudi ifanyike kuepuka vita na kama ipo iwe ni "last last last resort" na kwa sababu ya msingi sio hili la MIPASHO BAINA YA MARAISI. Ila Ndg. FOR2105 rekebisha kidogo waliokufa kwenye mapambano ya Kagera siyo wahaya peke yao bali hata wawakilishi wa makabila mengine mengi yaliyoshiriki kwenye vita moja kwa moja. Kuna ndugu zetu wengi sana wamekufa mstari wa mbele wakipambana kumng'oa nduli Amini na ushahidi mpaka leo upo pale kwenye makaburi ya mashujaa ya kambi ya Kaboya. Ila nakubaliana na wewe kuwa Wahaya waliathirika zaidi na mimi ni mmoja wa waathirika wengi na vita kwani nilikuwa Bukoba wakati Amini akileta ndege zake kuja kulipua sehemu mbalimbali Bukoba na lilishuhudia mabomu yakidondoshwa mpaka hospitali na kuathiri wagonjwa wasiokuwa na hatia. Kwa ufupi ni kuwa Kagame siyo adui wa watanzania na HATUTAKI VITA NAYE. Serikali ielekeze kuvu zake zote kwenye mapambano na maadui zetu wa jadi ambao ni UJINGA, MARADHI NA UMASKINI. na hawa wapya ambao ni UFISADI na UHALIFU WA KIMATAIFA ikiwepo na BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA.
 
Kama itatokea Rwanda atatandikwa basi atatandikwa na majeshi ya UN na sio Tanzania.

Ndibalema, That will be more good na bila shaka watakuwa na sababu kwa wakati huo. Tusiihusishe kabisa Tanzania na watu wetu wasihusike. Na kama ikitokea Uwanja wa vita uwe hukohuko watakaoamua wenyewe. Tanzania Hapana
 

Tata, Nimekubali na nilikiri kabisa kuwa Walio-athirika wengi walikuwa Wahaya. Tushirikiane ku - discourage hawa watu wachache wapenda vita. Pole kwa masaibu ya Vita ya Kagera, una kumbukumbu nzuri, unaweza kuwa mfano bora
 

Mkuu Environmental, Ahsante sana. Inauma sana sana hasa ukienda pale Mkoani Kagera kujionea madhara ya Vita ile afu leo mtu anakuambia Peleka nchi vitani, tena Eneo la Mapambano ni lilelile, hivi inaingia akilini kweli. Mimi Hapana. Tuwaambie hawa wanaoshabikia vita HAPANA. Serikali iwe makini na watu hawa ni hatari kwa Ustawi wa Taifa letu
 
Watu wa Mkoawa Kagera nafikir kwa sasa hawahitaj Vita,napenda pia kuwataarifu watu wengine kuwa hata huo ukimwi uliathiri kikamirifu Mkoa huo kiuchumi,chanzo chake ni vita hivyo,kwana Wanajeshi ndiyo waliyouingiza Tanzania(Wanajeshi wa Tanzania waliyokuwa vitani),sijui kama mnajua hilo?Kwa sasa mkoa unajipanga ki Uchumi.Pili lazima magazeti yazingatie kuandika mambo yasiyokuwa ya kichochezi,vita si vizuri.Tatu angalia nchi tunazozita ndugu kama Kenya inachukua nafasi ya kuendesha siasa za Biashara kwa kupitisha maneno na kukoleza mgogoro ili Rwanda itumie bandari yake.
 
Gulit, Inawezekana kuwa hujaiona Point kwa sababu hujatembea ndani ya Mistari ya Mada au pengine sijaandika kwa namna inayokufurahisha wewe na pengine wewe ni Mmojawao Marafiki wa Mashaka. Ila kwa kifupi ni kuwa VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA. Njoo na hoja
 

duh, kama unafamilia ina kaz kwel.
Leo hii Watanzania tunakosa huduma muhimu tukiwa na aman sasa tukiingia vitan itakuwaje? Vita ni very expensive interms of social and economic sectors. Unavyo onekana hili hulijui.
Vita ya kagera imechangia sana kutuporomosha kiuchumi na hadi sasa hatujarecover hayo majeraha wewe na wapuuz wenzako mnawaza vita.

Kagame hajatuvamia na hakituvamia tuna haki ya kumpiga ila kwa sasa hamna sababu ya kuingia vitan na kagame.

Kagame tushamjua ni mwendawazimu jibu zur ni kumpuuza na kulinda mipaka yetu ila huku kuendelea kujibizana nae ni sawa na kupiga sarakas tukiwa tumejifunga taulo ukilinganisha na status ya Tz dunian.

We rohombaya na blood sucker wenzako kama Jk alitoa ushaur kwa moyo mmoja kwa kagame aongee na waasi ili aman ipatikane why don't exercise that strategy with Rwanda so as to keep peace in our region?
 
Bila shaka wewe ni muhamiaji haramu......Rais kasema hatuna mpango wa kuivamia nchi yeyote kwa hiyo Rwanda wakiingia kwetu tucheke nao tu.....au hii operation ya kuwarudisha kwenu inawachanganya.....????
 
Mkuu unafaa kuwa kiongozi kabisaaaaaaa.wewe una hekima na busara.wewe ukiona mtu anaangalia matokeo ya vita.Hujue huyu mtu ana busara.vita sio ya siku moja kama tunavyofikiri.tumeona kule iraq,vietnam.Jamani siku hizi watu ni technology kama mkuu alivyoeleza hapo juu.Tujifunze kujenga na sio kuchochea kwa manufaa ya watoto wetu wanaokuja.Chuki tunayopandikiza sasa inaota miziz kwa kasi ya ajabu sana kwa hawa ndugu zetu,majirani wetu Rwanda.Jamani kweli watu wazima mkuu wapo hapa great thinkers website na wanaongea wana mtazamo mfupi ki akili.Vita kama unavyosema mkuu tunacheza na maisha ya ndugu zetu [wazee,watoto,akina mama].wengine kutembea hawawezi na vitu vya kuwabeba na kuwahamisha hamisha hakuna ,kwani kila mtu atakuwa anaokoa roho yake tu.Mungu hatuepushe na hili shetani la vita ambalo watu wachache wanalipenda.
 

MTU WA NJIA HII, Ni kweli kabisa watu wa Mkoa wa Kagera hawapendi vita ila kuna watu wachache nje ya Mkoa wa Kagera ambao wangependa kuona Mkoa ukianza tena kudidimia kwa kuondokewa na Nguvu kazi, maana ndio utakuwa uwanja wa Vita. Eti wanajivika Kilemba Cha Uzalendo, Uzalendo gani kwa kuwaona wenzako wanakufa na wewe Ukiwa Katika Runinga unaangalia Makombora yanavyorushwa na kuua Raia?..Hawa ndio tunaowambia kuwa VITA YA UGANDA SAWA,,,VITA NA RWANDA HAPANA
 
Bila shaka wewe ni muhamiaji haramu......Rais kasema hatuna mpango wa kuivamia nchi yeyote kwa hiyo Rwanda wakiingia kwetu tucheke nao tu.....au hii operation ya kuwarudisha kwenu inawachanganya.....????

Chisango, Natambua kuwa Mheshiwa Rais keshasema hivyo, na andishi langu halikumlenga Mheshimiwa Rais, linajaribu kuwaonesha watu wanaoendelea KUCHAGIZA vita, hata baada ya Mheshimiwa Rais kusema kuwa hatuna sababu ya kuwa na Vita sio kitu cha kushabikia kama wafanyavyo hao wapenda vita pengine labda na wewe ni miongoni mwao. Hata Tamko la Mkuu wa Nchi bado wanaendelea kulijadiri tena kwa namna ya hatari. Mkuu inawezekana mimi nikawa raia mzuri tu pengine kukuzidi wewe unayekimbilia kutaka kuniita Mkimbizi. No matter what, vita hapana Chisango
 

Mkuu,

Mjadara huu ulipoanza nilikasilishwa na mods na nikajifungia siku 10. Nilikuwa nimechukia sana nilipogundua watu wanashabikia vita kwa mwanvuri wa 'uzalendo'. Nilipojifungua ni kakuta mjadara ndo umepamba moto zaidi. Nimejitahidi kuwaeleza kama ulivyofanya, na ninafikiri watake wasitake wakuu wa nchi hii waiskilize sauti ya waishio Kagera. Kinyume na hapo vita ipelekwe huko waishiko sio Kagera.
 
je ni kweli Amini alikuwa wa kwanza kuvamia Tanzania? soma hapa chini ujue kile wengi hamjui
 
Kweli kabisa ndugu! Vita vya kiuchumi vinatutesa sasa vya bunduki si itakuwa majanga!hapana kabisa!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wala serikali ya Tz haijatangaza vita na Rwanda! Acha woga ndugu yangu! Kama itabidi Rwanda tutaidunda! Pia ni dhana potofu kufikiri kuwa ni wahaya pekee ndo walikufa katika vita ya Kagera! Ni Watanzania wote walishiriki katika vita hiyo! Acha woga!

Jaribu kumwelewa mleta mada. He must be right.
 
[h=2]Events leading to the war[edit source | editbeta][/h]Relations between Tanzania and Uganda had been strained for several years before the war started. After Amin seized power in a military coup in 1971, the Tanzanian leader Julius Nyerere offered sanctuary to Uganda's ousted president, Milton Obote. Obote was joined by 20,000 refugees fleeing Amin's attempts to wipe out opposition. A year later, a group of exiles based in Tanzania attempted, unsuccessfully, to invade Uganda and remove Amin. Amin blamed Nyerere for backing and arming his enemies. The relationship between Uganda and Tanzania remained strained for many years.In early October 1978, dissident troops ambushed Amin at the presidential lodge in Kampala, but he escaped with his family in a helicopter.[SUP][3][/SUP] This was during a period when the number of Amin's close associates had shrunk significantly, and he faced increasing dissent from within Uganda. When General Mustafa Adrisi, Amin's Vice President, was injured in a suspicious car accident, troops loyal to Adrisi (and other soldiers who were disgruntled for other reasons) mutinied. Amin sent troops against the mutineers (which included members of the elite Simba Battalion), some of whom had fled across the Tanzanian border.[SUP][1][/SUP][SUP][3][/SUP] The rebellion spilled over into Tanzania, where Tanzania-based anti-Amin exiles joined the fighting against Amin's troops.Uganda declared a state of war against Tanzania, and sent troops to invade and annex part of the Kagera region of Tanzania, which Amin claimed belonged to Uganda.

JE NI KWELI KUWA AMINI ALIANZISHA VITA? TAFUTA KUJUA ZAIDI , MITANDAO IKO WAZI KWA WOTE , HII NI SEHEMU NDOGO TU YA HABARI YENYEWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…