Vita ya Uganda sawa.....Rwanda hapana...Kagera tunasema hapana


Mkuu Mutakyamirwa, Naamini kwa dhati hawa mashabiki, wapambe wa vita wataisikia Sauti hii ya Watanzania. Binafsi nilifanya hivyo pia kumbe ulikuwa ni mwanya wa hawa jamaa kuendelea na UASI na UCHOCHEZI wao. Kamwe Serikali isiingie Mkenge. Wana Ajenda yao hao. Wana Kagera wanataka kuchapa kazi. Majanga ya Mv. Bukoba, Vita na Uganda, UKIMWI vyote vilihusisha vifo na hivyo kupunguza Nguvu kazi ya Taifa na Mkoa wa Kagera kwa Ujumla. Sasa nyie Blood Suckers mnataka nini tena jamani? Mbona yako mengi ya kuandika? Wagonjwa wanakufa mahospitalini, watoto wanasomea chini ya miti? hakuna walimu wa kutosha?bidhaa muhimu bei juu, Wauza Madawa ya kulevya kibao? Utoroshaji wa fedha nje ya nchi ndo usiseme? yaani mmeona KUCHAGIZA vita tu. HAKIKA NI WA KUPUUZWA
 
Ni kweli hata mie sipendi vita kabisa. Ila PK na watu wake wanaropoka ovyo, wako provocative sana.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
halafu kule Rwanda ili ujue yuko kivita zaidi kimaandalizi nasikia kila jengo refu keshaweka vifaa vya kutungulia ndege, njia zote za kwenda nyumbani kwake zimewekwa miiba. Sasa hivi mtanzania ukipata shida bahati mbaya imekukutia Rwanda usitegemee kabisa kupata msaada unaohitajika hata kama utakwenda polisi sanasana watakuchania hato document zako watakazohitaji kama vielelezo. Ndio ujue mioyo ya watu wa visasi ilivyo migumu hata akikuchekea.
 

WAKABAMBEE, Hiyo kitu nilishaisoma siku nyingi mno. I have it in ma head. Strongly nasema Nduli Idd Amin 'Dada' alivamia Ardhi ya Tanzania na hilo andiko linasema. Hilo ndio lilikuwa kosa lake, aliingizwa katika Mtego akategeka na hivyo akachakazwa, Ilikuwa ni haki ya Mwalimu kumuondoa na kisha kumuadhibu, hata hivyo the Story is Contrary to this Issue and I take it as History. Hoja yangu nimeijenga kwa wapenda vita ingawa wewe kimsingi pia hukupenda Uchokozi wa Tanzania kwa Uganda that time. Na mimi sipendi tuwe wachokozi
 

Nakuunga mkono. Vita na Rwanda haikubaliki ng'o. Tushughulike na kuinua uchumi na elimu ya watoto wetu na siyo vita. Vita huwa havina mshindi. Hata kama tukisema tulimshinda Nduli Idd Amin Dada bado tuliathirika sana kiuchumi na sidhani kama tumesha-stabilize tangu wakati ule. Tukatae vita kwa sababu yo yote ile.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Rubi, Hicho ndicho kinachotuponza Watanzania na pengine Wanyarwanda walio nchini mwao, KUSIKIA...Kuna Wanyarwanda pia wanaamini Wanyarwanda wakija Tanzania wananyanyaswa. Sasa wewe Rubi kama Mtanzania hebu tujadili hapa umesikia wapi kesi ya Mnyarwanda kunyanyaswa hapa Tanzania?. Kama hakuna then It is the same Story kwa Watanzania huko Rwanda. Yaani ni kukuza tuu mambo mradi wafanikishe mambo yao.

Kuongea ni Hulka ya Mtu ndio maana Wakenya wakienda Dukani wanasema NATAKA kilo moja ya Sukari wakati Mtanzania akienda atasema Naomba Kilo moja ya Sukari, ila wote wanachotaka ni kuhudumiwa. Tuache UMIMI, Tuache UBINAFSI
 
Ni kweli hata mie sipendi vita kabisa. Ila PK na watu wake wanaropoka ovyo, wako provocative sana.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

mbona hueleweki so kama wanaropoka ndo wanyaamazishwe kwa vita? nyani wale wadogo wakiona msitu unaungua hukaa juu ya mawe ng'ambo na kuchekelea bila kujua kama hayo ni makazi yao.....roho zenu za chki zishindwe kwa jina la yesu...we nani kumchukia binadam mwenzako...kagame na wanyarwanda walifanya nini hadi uwachukie hivo?unapoteza muda kushabikia ujinga wakati ni mlala hoi wa kawaida tu utakachoambulia ni njaa,hakuna madawa,shule ndo hivo mwisho za kata ila manufaa ya vita kama yapo hutanusa ng'o.....vita unayostahili kupigana kwa gharama yoyote ni ile ya madawa ya kulevya ufisadi na civic education...hiyo ndo vita ya mtz
 

Mkuu Kinauche, Nakushukuru, huu ni muda wa kuijenga nchi yetu sio Propaganda zisizo kuwa na kichwa wala miguu. Hao wapenda vita tuwashauri wabadili muelekeo. VITA HAILIPI kwa Tanzania. It only pays to US,UK,France, Russia na ni kwa sababu wanapata mwanya wa kuuza siraha na kamwe wasingependa itokee katika nchi zao. Blood Suckers andikeni Articles za Kuhusu Katiba Mpya ya Kuwasaidia Watanzania miaka 50 au pengine hata 100 ijayo sio kushabikia vita.
 
Wanaotaka vita hivi ni CCM ili wapate kisingizio kuwa tumeshindwa kuwapa maisha bora kwa kila Mtanzania kwa sababu tulichokozwa tukapigana vita. Hivyo hakuna kitu tena tuna kofia na khanga na wali mkavu tu. Tuchagueni tena muone furaha ya kushinda vita jamanie.....???
 

Ruzibiza, Wasamehe bure ila naamini Serikali pia watu wanaoichochea inawaona. Watu hawa ni ajabu kwelikweli they like Human Blood, sijui kwa nini. Ingawa naamini ni kwa sababu Ndugu, Jamaa na Marafiki zao hawataathirika kwa namna yoyote. TUWAKEMEE, na vyombo vya dola viwaonye
 

mgt software. Vita ikianza hakuna CCM, hakuna CHADEMA, hakuna CUF wala baba yake na NCCR, TLP wala UDP. Na kwa taarifa sio kwamba tutakuwa na uhakika wa kushinda. Ni vema kama kuna hizo NOTIONS basi vyama vyote bila kujali Itikadi vikakemea hawa watu wachache wasituingize katika Vita isiyo na kiuno wala kiwiliwili. HATUTAKI
 
na mie sitaki vita kabisa maana nguvu ilitumika Kagera iliharibu kila kitu, wenye magari makubwa kama Kugis, na wengine waliathilika sana maana magari yao yalikuwa yakikamatwa na kuamlisha kupeleka vikozi uwanja wa vita, wahindi wote waliondoka na mali nyingi, BCU ilifilisika kutokana na kugawa magari na pesa kwa ajiri ya vita. Kiwanda cha sukari na majani ya chai yaliaribiwa. Mifugo ilikosa madawa ikafa. Kwa kweli kilikuwa kilio cha kusaga meno na pia ndio ulikuwa mwisho wa usomi kwa wahaya, maana shule nyingi zilifungwa walimu walipelekwa kupigana.
 
Its true kwamba vita sio nzuri hata mimi sikubalian nalo ila rais anapaswa kuwa makini katka maamuz juu ya hili,maana siku zoye anaemaliza huwa anaonekana sie alienza!
 
Hivi kwa historia ya mtu kama Kagame akikuambia ataku-hit, unadhani anamaanisha nini?
 
Wacha uwoga kwanza waliokufa siyo wahaya tu kwa taarifa yako, yale makaburi 619 yaliyopo Kaboya sijui Kyaka ni ya Watanzania kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.Tukichokozwa tutampiga PK maana nia ya kumpiga tutakuwa nayo, sababu ya kumpiga tutakuwa nayo na uwezo wa kumpiga mpaka navosema sasa hivi saa tano usiku huu tunao tena kwa 100%
 
ndugu jaribu kutembelea rwanda uone kama hujawahi fika uone ili uamini uambiwacho. siku hizi si za zamni au jaribu kutafuta waTZ waliotoka rwanda hivi karibuni upate yanayojiri kivitendo sio kimacho.
 
Ushauri alioutoa JK kwa PK unaonyesha wazi jinsi rais wetu asivyopenda limwagike hata tone moja la damu ya mhanga mwingine wa ukanda wa maziwa makuu! Aliutoa ushauri huo ikiwa tayari askari wetu wakiwa tayari Kongo kuitikia wito wa UN. Aliutoa ushauri huo kama ni sehemu ya kuwajibika kwake kulinda maisha ya askari wetu na vilevile kuwapa nafasi wadau wengine (wanaojifichaficha) kusaidia ku'diffuse tense atmosphere' iliyokuwepo wakati huo! Rais wetu aliwajibika kikamilifu lakini wapenda vita wakaona KUTUTISHIA NYAU ni solution! Hamna mtu anaetaka vita Tanzania na wapenda vita halisi wameumbuka na wanaona haya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…