Huko vijijini unadhani ni kaburini mpaka ufe ndio uingie? Sio kwenda tu, hayo ni maisha yetu ya kawaida, na mitazamo iko wazi. Wale wajinga mliokuwa mnasema hawajui lolote kwa sasa wengi wanajua ukweli, ila kinachofanyika huko vijijini ni kuongozwa kwa kutishiwa maana wengi hawajui haki zao. Watu wanajua mbivu na mbichi, na isitoshe hatumlazimishi mtu yoyote kutuunga mkono, zaidi ya kumshawishi maana sisi sio kikundi cha kijeshi au kigaidi, hivyo tunatumia ushawishi wa hoja za kisiasa.
Kuna watu wengi sana wameulewa upinzani na wanaukubali, ndio maana unaona, ccm inatumia nguvu ya vyombo vya dola kuendelea kuzuia huo moto wa upinzani, unaosambaa kama moto wa petroli kwenye nyasi kavu usiendelee kusambaa. Mama yangu mzazi ana miaka 62 yuko Lushoto huko milimani, anaijua cdm na anaikubali sana, na sio yeye tu, wapo wengine wa umri wake, na vijana wengi wanaikubali cdm. Sasa sijui ni vijiji gani unataka kututishia.