Vita ya Urusi na Ukraine: Akili na malengo ya Putin nchini Ukraine

Wengi wameziamini Propoganda dhaifu za Putin.

Urusi imepakana na nchi 5 sio 2 za NATO kwenye mpaka wa nchi kavu na Uturuki katika Black Sea.
 
Wengi wameziamini Propoganda dhaifu za Putin.

Urusi imepakana na nchi 5 sio 2 za NATO kwenye mpaka wa nchi kavu na Uturuki katika Black Sea.
Anza kuusoma Uzi kuanzia mwanzo, maswali unayouliza au hoja unazozitoa zimejibiwa juu.

Kuuleta wakati uliyopita kwa wakati wa sasa ilihali kwa uliyopita ramani yake ilishawekwa wazi hayo ni mapungufu. Uhalali wa kuyaibua yaliyopita kwa nyakati ya sasa ni kuhoji ili fafanuzi zitolewe zaidi.

Usiturudishe nyuma tafadhali.
 
Wengi wameziamini Propoganda dhaifu za Putin.

Urusi imepakana na nchi 5 sio 2 za NATO kwenye mpaka wa nchi kavu na Uturuki katika Black Sea.
Sio kweli, hizo nchi zingine 3 za Nato zilizopakana na Russia nchi kavu ni zipi.
 
Nchi 6 zinazopakana na Russia ambazo tayari ziko NATO ni Norway, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Uturuki.
Sio kweli, hizo nchi zingine 3 za Nato zilizopakana na Russia nchi kavu ni zipi.
 
Uturuki imepakana na Urusi kwenye Black Sea.

Kama Russia haitaki kuikali Ukraine lengo la mwisho la uvamizi wao ni nini?

Mwisho wa uvamizi wao ili uhasibike umefanikiwa wanataka watimize nini ndio waondoe majeshi yao Ukraine?
Ni kweli wana-share bahari, pia wana-share bahari na Ujerumani na Denmark.

Malengo yao yako wazi tu, wanataka Katiba ya Ukraine ibadilishwe ikubali na kuitambua Crimea ni sehemu ya Urusi, wanataka jamhuri za Donetsk na Lugansk kutambuliwa na Ukraine kuwa nchi huru, pia Ukraine ijitangaze kuwa nchi Neutral . Hayo yakitimia tutaona Urusi wanarudi nyumbani. Ila binafsi natilia shaka kama wataondoka maeneo ya kusini kwenye miji ya Mariupol, Berdyansk, Melitopol na Kherson.
 
Nijuze mkuu mipaka ya bahari huwekwa wapi?
Hapo sikukutajia kuwa wamepakana na Japan na Marekani kwa bahari.
Wamepakana wapi? Unajua mipaka ya bahari kati ya nchi inapowekwa?
 
Inasikitisha Sana mtu anaandika upupu na watu wanamshabikia anyway , mda utatupa majibu sahihi kama huyo Putin atawatisha NATO au watamfurumusha...!!
 
Kama ni hivo kwanini marekani anaweka kambi ya kijeshi kila nchi??
 

Ndio, Marekani(Jimbo la Alaska) limepakana na Russia kwa sababu umbali kati yao ni maili 55 tu na kwenye eneo la maji dogo kama hilo(maziwa na mito pia) mpaka unakuwa katikati ya maji. Huu mpaka wa Alaska na Russia hauzungumziwi sana kwa sababu ukiacha bahari bado kuna eneo kubwa la barafu lisilopitika na pia Alaska ni jimbo lilo mbali na lisilopakana kwa ardhi na jimbo lingine lolote la Marekani.

Russia imepakana na Japan bahrini na wamekuwa na migogoro ya kugombania visiwa kadhaa kati yao kwa muda mrefu.
Nijuze mkuu mipaka ya bahari huwekwa wapi?
Hapo sikukutajia kuwa wamepakana na Japan na Marekani kwa bahari.
 
Tuelewane kidogo hii vita ni kama covid yaani dunia nzima tunateseka, kiufupi ni mwanzo wa anguko la marekani, Itafika hatua mkate utauzwa 5000 hapo watu tutasema kwa kejeli tu marekani kama super power huna msaada kwetu tupishe ndipo tutakapompokea Israel kwa shangwe atupoze.
 
Umeeleza uzuri mkuu yoda, ila kama ingewezekana kueleza lwa mujibu wa sheria za kimataifa ingekuwa nzuri sana.
 
Mkuu mbona kuna kitu umekiacha kutolea ufafanuzi Zelensky anasema kufeli kwa mazungumzo basi vita hii itakuwa ya 3 ya dunia, Ni kwa vipi hiyo vita itatokea? nani yuko nyuma ya Ukraine kwa hiyo vita? lakini Biden kasema vita ya 3 itapigwa katika ardhi ya urusi na sio Ukraine., hemu tiririka hapa icho kitendawili kikoje?

Lakini Jana Russia ametoa masaa ili Ukraine aweze ku-surrender lakini Ukraine wamekataa jambo lenye mfano huo, tiririka hapa ni kitu gani hii hasa hawa Ukraine wanategemea kwenye hii vita? Ivi NATO tayari wapo Ukraine kwenye vita lakini hawajaonyesha baya kwenye medias kwamba wapo mzigoni?
 
Umeeleza uzuri mkuu yoda, ila kama ingewezekana kueleza lwa mujibu wa sheria za kimataifa ingekuwa nzuri sana.
Kuhusu mipaka baharini kujua umbali na mamlaka ya nchi katika maeneo hayo ya bahari inatumika United Convection Law of the Sea (UNCLOS, 1994).

Kwenye hii Convection au makubaliano ya kimataifa yamegawanya sehemu za maji na bahari kama hivi
1.Inland waters
Haya ni maji ya mito na maziwa katika nchi.

2.Territory water
Hapa nchi inatakiwa imiliki maili zisizopungua 12 kuanzia Baseline ya maji.

3.Contigious Zone
Hapa nchi uchukua eneo la maji ya bahari kuanzia Baseline na livuke territory water na lisizidi umbali wa mile 24.

4.Economic Exclusive Zone (EEZ).
Ni eneo la bahari ambalo nchi umiliki mpaka umbali usiozidi mile 200.

5. Continental Shelf
Ni eneo baada ya mile 200 kutoka usawa wa mwanzo wa maji (Baseline) ambapo nchi iliyo karibu na bahari inaweza ikatumia eneo hili kwa tafiti za kisayansi au shughuli za utumiaji wa rasilimali katika miamba.

6.High Sea
Hii ni eneo la bahari kuu na hakuna mmiliki wa eneo hili.
Huku hata nchi ambayo haijazungukwa na bahari wanaweza wakafanya shughuli zao zozote bila kusumbuliwa.

Baseline ni eneo ambalo maji yakitoka au kupwa au maji mafu(Low Tide) huanzia ndipo huo umbali au mstari huanzia.

Kutokana na makubaliano ya Umoja wa mataifa kuhusu bahari (UNCLOS) nchi sio lazima ichukue maili zote 12 za territory water na Contigious zone. Kama nchi haina uwezo wa kusimamia inaweza ikachukua hata maili 3 na kama ina uwezo ichukue hata zote 12.
 
Inasikitisha Sana mtu anaandika upupu na watu wanamshabikia anyway , mda utatupa majibu sahihi kama huyo Putin atawatisha NATO au watamfurumusha...!!
Ungekuja na hoja tungekuwa na mjadala unaojenga.
 
Nakubaliana nawe mia fil’ mia.

Mpaka wa Urusi na Uturuki ulokuwa ukieleza ni matokeo ya makubaliano ya nchi zote mbili mwaka 1978. Sababu ya makubaliano hayo ni kuwa haki za umiliki wa bahari kwa Uturuki kwenye EEZ zinafikia mpaka maji ya Urusi, wakaona wakae chini wakubaliane.

BTW umeeleza vizuri.
 
Mkuu vita ya tatu ya dunia itahusisha wakubwa wa Dunia kijeshi Urusi, NATO (kama itaendelea kuwepo) na China. Nani atakua na nani dhidi ya nani hilo tulipe muda. Ila kwa hakika litakua janga kubwa sana kuwahi kutokea (Mungu atuepushe).
Kusema itapigwa kwenye ardhi ya Urusi si sawa, naamini itapiganwa Kote huku mapambano makali yakiwa Urusi, Ulaya, Marekani na China.

Ndiyo, Urusi walitoa ultimatum wakiitaka Ukraine kuisalimisha Mariupol ili Urusi wawaache wananchi na askari wa Ukraine waondoke Mariupol, Ukraine wamekataa matakwa hayo wamechagua kuendelea kupigana.

NATO hawajaingia kwenye hii vita ila wanawaunga mkono Ukraine kwa kuwatumia fedha na silaha hatari. Jeuri ya Ukraine inatoka kwa nchi za Magharibi zinazoifadhili kwa kuwapa silaha.
Matumaini waliyonayo Ukraine ni kwamba kwakuwa Urusi imewekewa vikwazo vya kiuchumi wanakadiria mpaka mwezi wa tano Urusi watakuwa wameshaishiwa rasilimali za kuendelea kufadhili hii vita hivyo itawalazimu kufikia makubaliano ya amani rahisi kwa Ukraine kuliko yalivyo sasa.
Kwahiyo wanafanya kila wanachoweza kuhakikisha wanachelewesha ushindi wa Urusi kwa kadri wanavyoweza mkuu.
 
Kwa namna nyingine una-sound kwamba:, makombora ya Urusi yanaaweza fika kokote kule aliko adui ila makombora ya US hayawezi fika Moscow bila kuwa ndani ya UKRAINE ndiyo maana US anaitaka Ukraine😂😂.
Una MAHABA japo unakata wengine wawe neutral.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…