Kile kile kilichomfanya USA akatae makombora ya wasovieti yasiwekwe CUBA ndio hiko hiko kinachomfanya Russia akatae Ukraine kujiunga na NATO.
Ile nguvu ya USA kuhisi anaweza kuyapangia mataifa mengine (Cuba) ya nini cha kufanya ndio nguvu hiyo hiyo Russia anaitumia kumpangia Ukraine nini cha kufanya!
Kwenye hii dunia ya leo ni aiza uwe na nguvu au ukubali kupangiwa cha kufanya. Hakuna option nyingine! Haiwezekani uwe huna nguvu alafu ujipangie cha kufanya. Mataifa yote duniani yamegawanyika pande hizo. Kuna yenye nguvu (yanayopanga mataifa mengine yafanye nini) na kuna yasiyo na nguvu (yanayopngiwa na mtaifa mengine yafanye nini).
Ukraine na Cuba wako kwenye upande wa wasio na nguvu. Russia na USA wapo kwenye upande wa walio na nguvu.
Kuhusu nini threat ya NATO kwa Russia. Simple logic tu ni kwa nn hiyo NATO inalazimisha sana kumove east!? Why not south or north!?
Kuhusu kwa nini UKraine kwa sababu 1. Strategic position ya Ukraine kwa Russia (kuliko hao wengine uliowataja) 2. Size ya Ukraine 3. Uwepo wa warusi waukraine nchini Ukr (Russian speaking UKRnians) 4. Sasa hv Russia wana nguvu ya kuzuia NATO asijitanue zaidi
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app