Vita ya Urusi na Ukraine: Putin aonya “Yeyote atakayeingilia atapata pigo la kihistoria”

Vita ya Urusi na Ukraine: Putin aonya “Yeyote atakayeingilia atapata pigo la kihistoria”

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
1645700034916.png

Rais wa Urusi, Vladimir Putin mara baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, ametoa onyo kwa mataifa ya Magharibi kuwa yeyote ambaye atajaribu kuingilia kinachoendelea baina ya mataifa hayo mawili atakutana na kitu ambacho hajawahi kukutana nacho.

Milipuko ilisikika Mji Mkuu wa Ukraine, Kiev ambapo Putin akanukuliwa akisema: “Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia.

Baraza la Usala la Umoja wa Mataifa liliitisha kikao cha dharura Jumatano Februari 23, 2022 mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi.

======

After Russian President Vladimir Putin announced he had ordered military action in Ukraine early Thursday, he threatened "those who may be tempted to intervene" on Ukraine's behalf. "Now a few important, very important words for those who may be tempted to intervene in ongoing events from the outside," Putin said.

"Whoever tries to interfere with us, and even more so to create threats to our country, to our people, should know that Russia's response will be immediate and will lead you to such consequences as you have never experienced in your history. We are ready for any development of events. All necessary decisions in this regard have been made. I hope that I will be heard."

The President of the European Council and the President of the European Commission issued a joint statement Thursday condemning Russian military action in Ukraine "in the strongest possible terms."

"Russia is grossly violating international law and undermining European and global security and stability," European Council President Charles Michel and European Commission President Ursula von der Leyen said in the statement.

Source: CNN
 
Putin amerukwa na akili....

Ni wakati muafaka kwa raia wa kawaida wa Urusi kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili..

Huyu jamaa ataiharibu zaidi nchi yake kiuchumi, kijamii huku akiipaka matope nchi yake mbele ya ulimwengu.

Ni lazima dunia iungane kuzuia Vita ya kibabe huko Ukraine.
 
Putin amerukwa na akili....

Ni wakati muafaka kwa raia wa kawaida wa Urusi kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili....
Putin ni tishio kwa dunia,

Ndio maana wakati wote hataki kuondoka madarakani, Ila wa Russia wote ni ndezi tu, mtu mmoja anakuwaje na nguvu namna hiyo? Yaani hata alipompa madaraka ya urais Medvedev ulikuwa ni uhuni tu, bado yeye ndio alikuwa mtawala.
 
Kuna watu waridhani Putin anaiogopa NATO na waliomba avamie sasa kavamia, sijui mtapitaje hapa.

Kwa kifupi media zilizo Africa, Ulaya na america taarifa mnazipata moja kwa moja kwa kingereza au kifaransa muda mwingine hata kwa kiswahili.

Ila nauhakika kuna watu hawajui kama china alishatangaza yupo na urus, pamoja na north korea wapo pamoja kwa shida na raha.

Na moja kubwa kuna makampuni ya marekani yamewekewa vikwazo china ni siku tatu nne nyuma ila watu hawajui kama wanachaguliwa taarifa za kusikia.

"Mwisho russia sababu anazo, nguvu anayo na uwezo anao ".

Mpaka putin kaamua ndio mjue marekani wamevunja mikataba kupitiliza zaidi ya miaka kumi russia kavumilia na marekani anajifanya superpower kwa superpower mwenzake wakati ile ni ardhi ya mrusi subir muone hlf bado madude ya kiduku.

Kwa asiyejua na anaesikiliza media za magharibi lazima amchukie Putin na amuone dictator ila ukimfatilia unajua dunia bila yeye dunia itafika mwisho haraka sana.

Long live Vladimir Putin Chuma.
 
Putin ni tishio kwa dunia,
Ndio maana wakati wote hataki kuondoka madarakani, Ila wa Russia wote ni ndezi tu, mtu mmoja anakuwaje na nguvu namna hiyo? Yaani hata alipompa madaraka ya urais Medvedev ulikuwa ni uhuni tu, bado yeye ndio alikuwa mtawala.
Hata akitawala dunia utamfanya nini? Kuna mambo hayaelezeki na mengine binadamu huyaweza mengine huwa ya Mungu mwenyewe.
 
hata akitawala dunia utamfanya nini ? kuna mambo hayaelezeki na mengine binadamu huyaweza mengine huwa ya Mungu mwenyewe.
Hana uwezo wa kutawala dunia, Yeye kama Superpower amefanya nini alipowekewa vikwazo?

Putin amefanya nini kwa ustawi wa dunia? Dunia ya wastaarabu hawapendi vita ndio maana wanamuona kama kichaa mmoja, Unafikiri US na NATO wakiingia nini kitatokea? Vita ya Dunia ya 3.
 
Safi wapigwe maana wao NAto ndio wamefikisha vita hapo. Walikua na room ya kuzuia njia yoyote ya ukraine kutaka kujiunga kwao.

Uzuri vita ya sasa itakua ni mabomu tuu.

Madalali wa magomeni tujiandae kupangisha wazungu kina rambo[emoji3]
Nina nyumba ya urithi apo magomeni, nitawapangisha kwa £400 kwa Mwezi
 
Putin amerukwa na akili....

Ni wakati muafaka kwa raia wa kawaida wa Urusi kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili..

Huyu jamaa ataiharibu zaidi nchi yake kiuchumi, kijamii huku akiipaka matope nchi yake mbele ya ulimwengu.

Ni lazima dunia iungane kuzuia Vita ya kibabe huko Ukraine.
Wangapi wamepigwa kibabe? Marekani alienda kumkanda mlibya kule, america kawakanda wangapi kwa uonevu? Hapa Urusi anafanya uonevu, lakini hao pro America wakae kimya, wakiligalambua dunia haitokalika
 
Back
Top Bottom