Nimesononeshwa sana na matokeo ya mitihani Kidato cha Nne ya Mwaka huu. Ni dhahiri kwamba kila mwaka kunakuwa na wanafunzi wanaofeli, lakini hili la 66% ya watahiniwa kufeli (kupata Division Zero) limeniuma sana.
Kuna sababu nyingi.....
kuanzia migomo ya walimu, watumishi wa umma kutishiwa nyau na serikali dhaifu, kiasi hata wengine kung'olewa meno. siasa kwenye elimu, hasa mijadala ya kishabiki ya wabunge wa ccm wanapokuwa bungeni kwa kuwa na tabia ya kusifia kila kitu kwa kauli za kijuha za 'kiwango cha ufaulu kimeongezeka ...tunaipongeza serikali' mambo yote ya namna hiyo.
lakini baya zaidi ni hili la utitiri wa vitabu vya rejea.
wakati siye tukisoma O'Level kulikuwa na vitabu dizaini moja tu. Vitabu vya Taasisi zetu adhimu...Taasisi ya Elimu Tanzania na Taasisi ya Kukuza Mitaala Tanzania. baada ya utandawazi na ubinafsishaji na nyonyaji na soko huria kumeibuka makanjanja wanaojifanya wanaandika vitabu vya maswali na majibu...moja wapo ni huyu jamaa anajiita Nyambari Nyangwine. Namshukuru Mungu sikuwahi kusoma vitabu vyake na hakika sitakuja kumshauri mtu avinunuwe. Haiwezekani kitabu kikawa na maswali na majibu tu halafu ukategemea kikusaidie kufaulu. hata kama utafaulu utakuwa bogazi tu kwa sababu huna maarifa kichwani.
Kwa kuwa waTZ tupo kama tumerogwa, basi hatuna budi tuchezee madini, tuchezee oembe za ndovu, tuchezee kila kitu, lakini TUSICHEZEE ELIMU.
vitabu vya Nyambari na makanjanja wenzake vipigwe marufuku. Walimu wapewe staha zao. Turudi kwenye mstari. Vinginevyo tunatia aibu, dunia ya leo kuwa kuzalisha wahitimu ambapo idadi ya waliofeli ni kubwa kuliko waliofaulu.
Nilishangaa sana niliposkia vitabu vya shaaban Robert vimefutwa Kusadikika na vyengine vimefutwa. Nikajiuliza kulikon? Nikawahi kuuliza ndugu wanafunzi jee Song of Lawino and Ocol- wakanijib hawakijui hicho kitabu. Nikamuuliza ndugu yangu ambae siishi nae pamoja ambae alikuwa form IV, hebu niambie umesoma vitabu vingapi na kuhakiki kwa upand wa kiswahili na kiingereza. Jibu alilonipa nilishangaa sana! yaani hajui hata kitabu kimoja. Alinivunja moyo sana kwani nilikuwa nikimlipia mpaka tuition. Kwa bahati nzuri kuna siku nikamfuma na vitabu, nikamuuliza kitbu gani hicho akanijibu Nyambari, kutizama ndani nakuta majibu matupu ya historia.
Mimi nimuumini wa Physics chem, Math na Biology tangu nasoma Form I-IV na FIV PCM ndio masomo yangu mama lakini vitbu vyote ambavo tuliambiwa tusome o-level tulisoma na mpaka leo vingine navikumbuka kama Mfame juha,Malenga wapya, kusadikika, mashairi ya kandoro-japokuwa kilifutwa lakini nilikuwa nacho na nakisoma. Vya english navyo tulisoma- No longer it easy, beautiful one not born yet, Great Ponds, Lawino and Okol nk.
Wanafunzi wa leo ni wavivu ile mbaya, mtu akichukua masomo ya art eti ya sayansi hayataki na wa sayansi eti wa art hayataki, huu ni upumbavu wa hali ya juu. Matokeo yake ukiwa umefanya masomo 4 na yule aliefanya 7 kiwiano anaibuka kidedea aliefanya 7 na hapo ndio chanzo cha kufeli watoto wengi. Utashangaa mtu anafanyia mtihani masomo 3 tu lakini kila mwaka anafeli.
Siku hizi kuna mtandao na facebook, kila mwanafunzi utamkuta yupo huko ni kuchat tuu, akirudi nyumbani TV hana mda.
USHAURI KWA SERIKALI
1. Vitabu ivipige marufuku na tuje na sera mpya ya elimu
2. Serikali itangaze zawadi nono kwa wanafunzi ili iwafichue wezi wa mitihani pamoja na wale wa mtandao wizari ambao wanawatengenezea vyeti vya credit kwa wanafunzi waliofeli ili watu wapige dili. Huu mtandao upo na ndalichako na wenzake wanaujua.
3. Ijenge vyuo vya amali ili waliofeli waweze kujiendeleza zaid