Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu

Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu

Nimesononeshwa sana na matokeo ya mitihani Kidato cha Nne ya Mwaka huu. Ni dhahiri kwamba kila mwaka kunakuwa na wanafunzi wanaofeli, lakini hili la 66% ya watahiniwa kufeli (kupata Division Zero) limeniuma sana.

Kuna sababu nyingi.....

kuanzia migomo ya walimu, watumishi wa umma kutishiwa nyau na serikali dhaifu, kiasi hata wengine kung'olewa meno. siasa kwenye elimu, hasa mijadala ya kishabiki ya wabunge wa ccm wanapokuwa bungeni kwa kuwa na tabia ya kusifia kila kitu kwa kauli za kijuha za 'kiwango cha ufaulu kimeongezeka ...tunaipongeza serikali' mambo yote ya namna hiyo.

lakini baya zaidi ni hili la utitiri wa vitabu vya rejea.

wakati siye tukisoma O'Level kulikuwa na vitabu dizaini moja tu. Vitabu vya Taasisi zetu adhimu...Taasisi ya Elimu Tanzania na Taasisi ya Kukuza Mitaala Tanzania. baada ya utandawazi na ubinafsishaji na nyonyaji na soko huria kumeibuka makanjanja wanaojifanya wanaandika vitabu vya maswali na majibu...moja wapo ni huyu jamaa anajiita Nyambari Nyangwine. Namshukuru Mungu sikuwahi kusoma vitabu vyake na hakika sitakuja kumshauri mtu avinunuwe. Haiwezekani kitabu kikawa na maswali na majibu tu halafu ukategemea kikusaidie kufaulu. hata kama utafaulu utakuwa bogazi tu kwa sababu huna maarifa kichwani.

Kwa kuwa waTZ tupo kama tumerogwa, basi hatuna budi tuchezee madini, tuchezee oembe za ndovu, tuchezee kila kitu, lakini TUSICHEZEE ELIMU.

vitabu vya Nyambari na makanjanja wenzake vipigwe marufuku. Walimu wapewe staha zao. Turudi kwenye mstari. Vinginevyo tunatia aibu, dunia ya leo kuwa kuzalisha wahitimu ambapo idadi ya waliofeli ni kubwa kuliko waliofaulu.

Ngw'anangwa ninaongeza moja kwenye hivyo vitabu vya maswali na majibu, majibu yaliyowekwa mengi yamekosewa. Hivi vitabu vipigwa marufuku immediately.

Nimesikia Mh Waziri TBC akisema wanaenda retreat kutafuta majibu. Nitafarijika ikiwa kuna mtu atamshahuri asihangaike na retreat anatuingiza gharama ya bure (maana najua watalipana posho kubwa). Sababu zinaeleweka na wala hazihitaji retreat. Lakini la kushangaza ni kwa nini alipinga hoja ya Mbatia ambayo ilikuwa inaomba kutafuta majibu ya matatizo haya na sasa anakuja na retreat. At least akiwa muungwana awaombe radhi watanzania.
 
actually nina ku award gt's honorable award for the year.

Mkuu watu anasema mengi sana lakini wanasahahu kwamba hakuna elimu kama hakuna valid reference. Ukiangalia kwa makini utagunda kwamba nyambari nyangwine baadhi ya vitabu vyake vinapotosha sana sana tena vinahadaa kabisa. Upataji wa maarifa ni pamoja na kupata correct and proper knowledge of the subject matter.

Sasa most of his books correctness of the subject matter ni ishu kubwa sana sana. Angalia vitabu vyake vya litrature na english structure angalia vya biology ni uongo mtakatifu.

Kule kwenye maswali na majibu ni uongo mtupu, sintosahau eti swali linasema ""name the vein which transports blood from the liver to the stomach"" jamani jamani kweli hii ni sahihi?? Ukienda kwenye majibu unakuta jibu ni hepatic portal vein.

Nilichowaambia wanafunzi wangu n kwamba wao wabaki wakariri majibu ya uongo na maarifa potofu huku wakidharau mafunzo ya waalimu wao.

kama hiyo picha kwenye avatar ni ya kwako basi umezawadiwa kiuno kizuri sana
 
actually nina ku award GT's honorable award for the year.

mkuu watu anasema mengi sana lakini wanasahahu kwamba hakuna elimu kama hakuna valid reference. Ukiangalia kwa makini utagunda kwamba Nyambari Nyangwine baadhi ya vitabu vyake vinapotosha sana sana tena vinahadaa kabisa. Upataji wa maarifa ni pamoja na kupata correct and proper knowledge of the subject matter.

sasa most of his books correctness of the subject matter ni ishu kubwa sana sana. angalia vitabu vyake vya litrature na english structure angalia vya biology ni uongo mtakatifu.

kule kwenye maswali na majibu ni uongo mtupu, sintosahau eti swali linasema ""name the vein which transports blood from the liver to the stomach"" jamani jamani kweli hii ni sahihi?? ukienda kwenye majibu unakuta jibu ni hepatic portal vein.

nilichowaambia wanafunzi wangu n kwamba wao wabaki wakariri majibu ya uongo na maarifa potofu huku wakidharau mafunzo ya waalimu wao.

Naungana na hoja yako, kwani hata mimi kuna baadhi ya mada nimejaribu kuzichunguza kwa makini katika masomo ya lugha na kugundua makosa yasiyosameheka, kunawakati katika kusomasoma kwangu nikagundua hawa jamaa hawatumii vichwa vyao katika utunzi wa vitabu bali wanacopy sana na kupaste kiasi wakati mwingine katika kufanya hivyo huwa hawafanyi analysis ya kina kwa kile wanachokicopy na kukipaste na kuishia kuandika makosa katika kazi zao.
 
"Vitabu vya Nyangwine"(vitabu vya maswali na majibu) havimfanyi mwanafunzi kushindwa mtihani. Mwanafunzi anashindwa mtihani kwa kiasi kikubwa kutokana na maandalizi aliyonayo. Mwanafunzi akihudhuria darasani, akamsikiliza mwalimu, akaandika notes, akafanya mazoezi na majaribio yote, akasoma vitabu vya kiada(text book) kisha akija kupata "vitabu vya Nyangwine" atafanya vizuri kwenye mitihani.

Kwa hiyo ni upotoshaji kusema kuwa vitabu vya maswali na majibu ni janga kielimu, janga na maandalizi mabovu kwa mwanafunzi.

Mkuu aina hii ya usomaji ( maswali na majibu bila kuwa na ziada yeyote) ni janga .Tatizo lilikuwa linakua taratibu nadhani sasa limefikia kilele watu wanashtuka. Mwanafunzi ahimizwe na azoeshwe kutafuta maarifa kwanza kupitia vitabu si maswali na majibu kuanzia form I! Nilifaulu kirahisi sana O-level kwa kusoma NELKON,ABOTT,TITCOMB and the like
 
Vitabu vyake ni bomu lakini vinapata ithibati. Wizara ya elimu ni ngoma nzito haichezeki!
 
Acheni kumsingizia Nyambari hizo shule zenyewe nyingi hata ukiwaulizia vitabu vya huyo mwandishi
hawavijui,kwani hawana vitabu kabisa,na kwa taarifa yako uliza shule zilizofanya vizuri watakuambia
wanatumia vitabu hivyohivyo unavyoviponda" acha wivu tatueni migogoro ya waalimu"

Kusema uomgo ni dhambi! Huwezi kukuta kitabu jamii na N. Nyangwine n.k kwenye maktaba ya shule kama Kifungilo n.k.
Vitabu vilivyopo nchini (vya binafsi na serikali) vina mchango mkubwa kwenye uduni wa elimu. Mh. Mbatia alilalama juu ya ubovu wa vitabu (udhaifu unaoongelewa na walimu kila kona) watu wasema anatafuta umaarufu. Nchi hii haina vitabu vinavyoweza kumpa mwanafunzi uelewa sahihi. Ikiwa kama huamini, naomba unitajie vitabu vya Economics, Geography n.k tuvifanyie uchambuzi.
 
Kwa kweli suala la vitabu nchi hii ni tatizo kubwa sana. Walipoondoa jukumu hilo kwa Taasisi ya Elimu na kuanza soko huria imekuwa holela kweli
 
Nimesononeshwa sana na matokeo ya mitihani Kidato cha Nne ya Mwaka huu. Ni dhahiri kwamba kila mwaka kunakuwa na wanafunzi wanaofeli, lakini hili la 66% ya watahiniwa kufeli (kupata Division Zero) limeniuma sana.

Kuna sababu nyingi.....

kuanzia migomo ya walimu, watumishi wa umma kutishiwa nyau na serikali dhaifu, kiasi hata wengine kung'olewa meno. siasa kwenye elimu, hasa mijadala ya kishabiki ya wabunge wa ccm wanapokuwa bungeni kwa kuwa na tabia ya kusifia kila kitu kwa kauli za kijuha za 'kiwango cha ufaulu kimeongezeka ...tunaipongeza serikali' mambo yote ya namna hiyo.

lakini baya zaidi ni hili la utitiri wa vitabu vya rejea.

wakati siye tukisoma O'Level kulikuwa na vitabu dizaini moja tu. Vitabu vya Taasisi zetu adhimu...Taasisi ya Elimu Tanzania na Taasisi ya Kukuza Mitaala Tanzania. baada ya utandawazi na ubinafsishaji na nyonyaji na soko huria kumeibuka makanjanja wanaojifanya wanaandika vitabu vya maswali na majibu...moja wapo ni huyu jamaa anajiita Nyambari Nyangwine. Namshukuru Mungu sikuwahi kusoma vitabu vyake na hakika sitakuja kumshauri mtu avinunuwe. Haiwezekani kitabu kikawa na maswali na majibu tu halafu ukategemea kikusaidie kufaulu. hata kama utafaulu utakuwa bogazi tu kwa sababu huna maarifa kichwani.

Kwa kuwa waTZ tupo kama tumerogwa, basi hatuna budi tuchezee madini, tuchezee oembe za ndovu, tuchezee kila kitu, lakini TUSICHEZEE ELIMU.

vitabu vya Nyambari na makanjanja wenzake vipigwe marufuku. Walimu wapewe staha zao. Turudi kwenye mstari. Vinginevyo tunatia aibu, dunia ya leo kuwa kuzalisha wahitimu ambapo idadi ya waliofeli ni kubwa kuliko waliofaulu.

Naomba kutofautiana kidogo: Sidhani kama vitabu vina- violet mathematical priciples! Vitabu vyake vinalenga kumpa mtoto mazoezi kwa yale aliyoyasoma na kuyaelewa. Ukiona umesoma topic ya differentiation katika hesabu, ukashinwa kujibu maswali katika topic hiyo, ujue bado hujafikia kiwango. Inabidi uzame tena UELEWE. Vitabu vyake ni copy ya vitabu tulivyovisoma miaka ya 70! Kuna factors nyingi kushindwa kwa watoto. Moja kubwa among the major ones, watoto hawasomi! Tunao, tunaishi nao etc, tunawaona.
 
uhalisia ni kwamba mwananfunzi yeyote akipewa 'desa' huwa anabweteka na kuanza kumeza kilichoandikwa kwenye 'desa'. navitizama vitabu vya huyu jamaa kama madesa ambayo hayana msaada, sana sana yanaua kiwango cha ufikiri wa watoto wetu na kwa hiyo kuchangia katika matokeo mabovu ya mitihani ya mwisho.
 
Sasa tunajadili tatizo la elimu Tanzania ingiwa baadaye ingekuwa vizuri kuwa na mjadala wa wazi wa ukweli kuhusu haya mambo. Bila hivyo, Tanzania inapukutika kwa kukosa uzalendo.
 
Vitabu kama hivyo vilikuwapo miaka niliyoiasema (70s) vikijinadi kutoa elimu ya kiwango cha "cambridge" Title zake zilijinadi: cambridge History, Cambridge Biology etc. Vilikuwa kama vya Nyangwine ndio maana nasema ana-copy mfumo wa zamani, he did not invent anything. Hivyo kusema watoto wanalemaa si kweli mbona wa zamani hamsemi walilemaa , maana walikuwa na vitabu kama hivyo hasa wakati wa mkoloni na mwanzoni mwa uhuru!
 
mkuu, mimi ni product ya mwaka 1996-1999. nilisoma shule combination moja tu...PCM. lugha ilikuwa ni Abbot, Lambert, Fundamentals of Engineering Science, Nelkon, you name it. Ukienda Kiingereza unakula vitu vya Oxford, Things Fall Apart, na vitu vyote vya maana vya kupasuwa vichwa. Enzi zile ukiwa unajuwa unajuwa kweli, si lelemama.

asa leo hii unauziwa kitabu pembezoni mwa barabara kama karanga, afu mnategemea tutatoka kweli?

Somo moja, kidato kimoja, vitabu tofauti, waandishi tofauti, contents tofauti.

Watoto wenyewe hawa wanamaliza form four na miaka 17, unamuandaa kuhitimu kwa kutumia varieties za vitabu zaidi ya tano, kwa somo moja. na waandishi wenyewe ndo hawa wanagombea milingoti ya bendera.

Elimu hii ni janga sasa. ila kwa kuwa wabongo hampendi ukweli, basi, mshaanza ku-personalize hii ishu.

Nipo kitaifa zaidi.
sijakubishia kwamba vitabu hivyo ubora wake una walakini.......lakini sio kweli kwamba ndiyo sababu kubwa ya kuwafelisha wanafunzi.......kwa sababu product ya miaka ya 2000 wengi tumetumia sana vitabu hivi na kiukweli wengi vimetusaidia sana.......hivyo vitabu unavyovitaja vinatumika hadi leo lakini katika baadhi ya shule tena zile za zamani tena vimebaki vichache sana kwa sababu serikali haijajisumbua kununua vingine na kuweka maktaba na mbaya zaidi shule nyingi hazina hata hizo maktaba........kununua Abbot, Lambert si mchezo.......wisho wa siku tunasema serikali yetu haijali elimu ya watu wa chini..........shule zote za serikali zinapotea kwenye ramani kiasi kwamba watu siku hawajali hata watoto wao wakichaguliwa mzumbe,ilboru,kilakala,pugu,tosamaganga,ndanda,galanos, kwiro, mpwapwa,moshi tech,tanga tech,tabora boys,msalato,..........n.k......siku hizi shule hizi zimechoka kama nini nyingi hazitamaniki......serikali inachezea elimu yetu......
 
Mfumo wa elimu wa Tanzania unahitaji postmortem
 
Hivyo vitabu vinalenga kujenga uwezo wa kukariri tu havimjengei mwanafunzi maarifa
 
Back
Top Bottom