Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu



kwa kuwa tafsiri yako ni ya 'haraka haraka', ngoja na mimi nisikupatie jibu haraka haraka.
 
Acha wivu nyambari kasaidia sana watu.. Nchi haina mitaala hii unataka watu asone nini?

Mh, ushahidi? Vitabu vyake vingi vinapotosha, kuanzia grammar hadi content. Halafu watoto ndo wanashindia kukariri, na attention zero kwa walimu madarasani. Pia baadhi ya walimu wanaviona kama misahafu, hakuna juhudi ya kutafuta vitabu vya ziada juu ya somo husika.
 
asa mliktaka wasome nini acha masihara vitabu vimewatoa wengi sana nchi....
 
hivyo ndivyo vilivyopo na vinapatikana ki urahisi
 
kasaidia sana,si umeona matokeo
vitabu vilikuwepo kabla ya mwaka huu tokea miaka ya 2000 iweje leo useme ndo sababu......chukua paper ya necta angalia asilimia maswali kibao yanatoka kwenye hivyo vitabu mnavyoviponda....mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..........letemni mbadala wa hivyo vitabu
 
Mtaala upo, na kama haupo wewe usingefaulu. Mtaala upo ila wanauficha. labda tuambiwe sababu za kufichwa kwa Mtaala wa Elimu yetu ni nini?
Mambo ya rushwa tu mkuu. naafiki hao makanjanja wanakoroga sana. kila mtu akiingia wizarani anakula deal na makanjanja wake sylabus inabadilishwa kuingiza vitabu mbadala.
 

Wengine tulitumia vitabu hivyo hivyo vya Nyambari na tulisoma shule za hizo hizo za ada ya elf 20 na tulifaulu?! Wazazi wangapi wanaweza kununua vitabu vya maana vya tsh 30,000 hadi 70,000?
Kama issue ni kufaulu tu na sio kuelewa muhimu kumtumia Nyambari aisee manake necta yenyewe hawana maswali mapya wana copy na kupaste ya mitihani ya nyuma.
Tatizo kubwa watoto hawasomi na wanao soma hawapo serious.
 
Acheni kumsingizia Nyambari hizo shule zenyewe nyingi hata ukiwaulizia vitabu vya huyo mwandishi
hawavijui,kwani hawana vitabu kabisa,na kwa taarifa yako uliza shule zilizofanya vizuri watakuambia
wanatumia vitabu hivyohivyo unavyoviponda" acha wivu tatueni migogoro ya waalimu"
 

Toa mfano kitabu gani?


Kuna mtu aliyesoma Geography hakusoma kitabu cha Msabila au Economics vya Ambilikile? ( Ambapo hao wote watu wa Nyambari.
 
Naunga mkono hoja,lakini inatubidi kama taifa tujikite katika mjadala mpana juu ya namna ya kuweza kutatu tatizo la elimu yetu kushuka.
 

Waulize swali wanafunzi wote wa sayansi mwaka huu kama wanajua vitabu vya Abbot na principal physics? Hakuna kitu! Wakati sisi ndo tulikuwa tunachimba humu heat na electricity kuanzia form one mpaka form four. Hivi vitabu vya sasa sijui hata ni summary ya nini kwani kwa somo havifai kabisa.
 
NITAKUWA TOFAUTI SANA.
1.si kweli nyambari nyangwine kubebeshwa zigo lote la lawama na vitabu vyake
2.vipo vitabu vizuri mfano kwa wale wanamahesabu Mathematics cha mwakamoga fm1,2,3&4 sponsored by nyangwine
3.vitabu vipya vya serikali ndio vibovu kabisa na havifai licha ya kutumia pesa nyingi ya walipa kodi
MFANO,angalia vitabu vyote vpya kwa mihutasar ya 2005 vilivyo chini ya wizara ya elimu BARA.kama kuna mtu anabisha angalia kimoja tu cha fm two maths topic ya logarithm(NI HATARI)
4.pia vitabu vya serikali havifanani mfano chukua physics cha zanziba USAID,NA physics cha BARA,vyote kwa syllabus ya 2005,UTAGUNDUA MAAJABU mana syllabus moja lakini idadi ya topic inatofautiana na hata mambo mengine yapo kwenye syllabus lakin kwenye vtabu hakuna
5.mwaka jana vitabu vya ZANZIBAR(USAID) vilisambazwa kila kona ya nchi na hivyo wengi zaid wamevitumia lakin vya nyambari ni wale tu wenye uwezo ndo wanavipata kwa wingi
6.mapungufu na makosa hata kwenye vile vya zanzibar ni MENGI,kuna v2 havtolew maelezo eg PHYISCS
 
Mtaala upo, na kama haupo wewe usingefaulu. Mtaala upo ila wanauficha. labda tuambiwe sababu za kufichwa kwa Mtaala wa Elimu yetu ni nini?

teh! teh! teh!....................arguments nyngne bana eh....................................
 

kwani kuna tofauti gani na Google, kama hutaki c unaacha!
 
kufaulu mtihani wa Form Four ni rahisi sana kama ukisoma matirio sahihi kwa muda muafaka.
Sasa kama unaambiwa na NECTA wanatumia hayo madesa ya Nyangwine unategemea mwanafunzi akijibu kwa usahihi atafauru !?
 

mkuu, mimi ni product ya mwaka 1996-1999. nilisoma shule combination moja tu...PCM. lugha ilikuwa ni Abbot, Lambert, Fundamentals of Engineering Science, Nelkon, you name it. Ukienda Kiingereza unakula vitu vya Oxford, Things Fall Apart, na vitu vyote vya maana vya kupasuwa vichwa. Enzi zile ukiwa unajuwa unajuwa kweli, si lelemama.

asa leo hii unauziwa kitabu pembezoni mwa barabara kama karanga, afu mnategemea tutatoka kweli?


Somo moja, kidato kimoja, vitabu tofauti, waandishi tofauti, contents tofauti.

Watoto wenyewe hawa wanamaliza form four na miaka 17, unamuandaa kuhitimu kwa kutumia varieties za vitabu zaidi ya tano, kwa somo moja. na waandishi wenyewe ndo hawa wanagombea milingoti ya bendera.

Elimu hii ni janga sasa. ila kwa kuwa wabongo hampendi ukweli, basi, mshaanza ku-personalize hii ishu.

Nipo kitaifa zaidi.
 

Nilishangaa sana niliposkia vitabu vya shaaban Robert vimefutwa Kusadikika na vyengine vimefutwa. Nikajiuliza kulikon? Nikawahi kuuliza ndugu wanafunzi jee Song of Lawino and Ocol- wakanijib hawakijui hicho kitabu. Nikamuuliza ndugu yangu ambae siishi nae pamoja ambae alikuwa form IV, hebu niambie umesoma vitabu vingapi na kuhakiki kwa upand wa kiswahili na kiingereza. Jibu alilonipa nilishangaa sana! yaani hajui hata kitabu kimoja. Alinivunja moyo sana kwani nilikuwa nikimlipia mpaka tuition. Kwa bahati nzuri kuna siku nikamfuma na vitabu, nikamuuliza kitbu gani hicho akanijibu Nyambari, kutizama ndani nakuta majibu matupu ya historia.
Mimi nimuumini wa Physics chem, Math na Biology tangu nasoma Form I-IV na FIV PCM ndio masomo yangu mama lakini vitbu vyote ambavo tuliambiwa tusome o-level tulisoma na mpaka leo vingine navikumbuka kama Mfame juha,Malenga wapya, kusadikika, mashairi ya kandoro-japokuwa kilifutwa lakini nilikuwa nacho na nakisoma. Vya english navyo tulisoma- No longer it easy, beautiful one not born yet, Great Ponds, Lawino and Okol nk.
Wanafunzi wa leo ni wavivu ile mbaya, mtu akichukua masomo ya art eti ya sayansi hayataki na wa sayansi eti wa art hayataki, huu ni upumbavu wa hali ya juu. Matokeo yake ukiwa umefanya masomo 4 na yule aliefanya 7 kiwiano anaibuka kidedea aliefanya 7 na hapo ndio chanzo cha kufeli watoto wengi. Utashangaa mtu anafanyia mtihani masomo 3 tu lakini kila mwaka anafeli.
Siku hizi kuna mtandao na facebook, kila mwanafunzi utamkuta yupo huko ni kuchat tuu, akirudi nyumbani TV hana mda.
USHAURI KWA SERIKALI
1. Vitabu ivipige marufuku na tuje na sera mpya ya elimu
2. Serikali itangaze zawadi nono kwa wanafunzi ili iwafichue wezi wa mitihani pamoja na wale wa mtandao wizari ambao wanawatengenezea vyeti vya credit kwa wanafunzi waliofeli ili watu wapige dili. Huu mtandao upo na ndalichako na wenzake wanaujua.
3. Ijenge vyuo vya amali ili waliofeli waweze kujiendeleza zaid
 
kusema ukweli nyangwine analemaza wanafunzi wetu,ila nakumbuka shule niliyokua nasoma walimu walikua wanatuonya kabsa kabla ya mitihani kwamba tusijisumbue kusoma kitabu cha nyangwine kwani hakuna swali hata moja litakalotoka humo kwenye mtihani na ,shule yetu ilikua ukifeli lazima urudie darasa na kwel wale waliojisumbua kuvisoma walichemka na wengine tuliokazana kwenye notes na vitabu vya kiada na ziada tulikua tunafanya vema hiyo ilisaidia kudiscourage na hata mwalimu alikua akitoa swali kutoka kwenye hivyo vitabu alikua anahakikisha kama kitabu kinatoa majibu 5 basi yeye anataka 10 na in details
 

Vitabu vya Nyangwine ni kama vile vitabu vinachapishwaga CBS Publishers & Distributors ... New Delhi, Bangalore.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…