Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu


Ngw'anangwa ninaongeza moja kwenye hivyo vitabu vya maswali na majibu, majibu yaliyowekwa mengi yamekosewa. Hivi vitabu vipigwa marufuku immediately.

Nimesikia Mh Waziri TBC akisema wanaenda retreat kutafuta majibu. Nitafarijika ikiwa kuna mtu atamshahuri asihangaike na retreat anatuingiza gharama ya bure (maana najua watalipana posho kubwa). Sababu zinaeleweka na wala hazihitaji retreat. Lakini la kushangaza ni kwa nini alipinga hoja ya Mbatia ambayo ilikuwa inaomba kutafuta majibu ya matatizo haya na sasa anakuja na retreat. At least akiwa muungwana awaombe radhi watanzania.
 

kama hiyo picha kwenye avatar ni ya kwako basi umezawadiwa kiuno kizuri sana
 

Naungana na hoja yako, kwani hata mimi kuna baadhi ya mada nimejaribu kuzichunguza kwa makini katika masomo ya lugha na kugundua makosa yasiyosameheka, kunawakati katika kusomasoma kwangu nikagundua hawa jamaa hawatumii vichwa vyao katika utunzi wa vitabu bali wanacopy sana na kupaste kiasi wakati mwingine katika kufanya hivyo huwa hawafanyi analysis ya kina kwa kile wanachokicopy na kukipaste na kuishia kuandika makosa katika kazi zao.
 

Mkuu aina hii ya usomaji ( maswali na majibu bila kuwa na ziada yeyote) ni janga .Tatizo lilikuwa linakua taratibu nadhani sasa limefikia kilele watu wanashtuka. Mwanafunzi ahimizwe na azoeshwe kutafuta maarifa kwanza kupitia vitabu si maswali na majibu kuanzia form I! Nilifaulu kirahisi sana O-level kwa kusoma NELKON,ABOTT,TITCOMB and the like
 
Vitabu vyake ni bomu lakini vinapata ithibati. Wizara ya elimu ni ngoma nzito haichezeki!
 

Kusema uomgo ni dhambi! Huwezi kukuta kitabu jamii na N. Nyangwine n.k kwenye maktaba ya shule kama Kifungilo n.k.
Vitabu vilivyopo nchini (vya binafsi na serikali) vina mchango mkubwa kwenye uduni wa elimu. Mh. Mbatia alilalama juu ya ubovu wa vitabu (udhaifu unaoongelewa na walimu kila kona) watu wasema anatafuta umaarufu. Nchi hii haina vitabu vinavyoweza kumpa mwanafunzi uelewa sahihi. Ikiwa kama huamini, naomba unitajie vitabu vya Economics, Geography n.k tuvifanyie uchambuzi.
 
Kwa kweli suala la vitabu nchi hii ni tatizo kubwa sana. Walipoondoa jukumu hilo kwa Taasisi ya Elimu na kuanza soko huria imekuwa holela kweli
 

Naomba kutofautiana kidogo: Sidhani kama vitabu vina- violet mathematical priciples! Vitabu vyake vinalenga kumpa mtoto mazoezi kwa yale aliyoyasoma na kuyaelewa. Ukiona umesoma topic ya differentiation katika hesabu, ukashinwa kujibu maswali katika topic hiyo, ujue bado hujafikia kiwango. Inabidi uzame tena UELEWE. Vitabu vyake ni copy ya vitabu tulivyovisoma miaka ya 70! Kuna factors nyingi kushindwa kwa watoto. Moja kubwa among the major ones, watoto hawasomi! Tunao, tunaishi nao etc, tunawaona.
 

uhalisia ni kwamba mwananfunzi yeyote akipewa 'desa' huwa anabweteka na kuanza kumeza kilichoandikwa kwenye 'desa'. navitizama vitabu vya huyu jamaa kama madesa ambayo hayana msaada, sana sana yanaua kiwango cha ufikiri wa watoto wetu na kwa hiyo kuchangia katika matokeo mabovu ya mitihani ya mwisho.
 
Sasa tunajadili tatizo la elimu Tanzania ingiwa baadaye ingekuwa vizuri kuwa na mjadala wa wazi wa ukweli kuhusu haya mambo. Bila hivyo, Tanzania inapukutika kwa kukosa uzalendo.
 
Vitabu kama hivyo vilikuwapo miaka niliyoiasema (70s) vikijinadi kutoa elimu ya kiwango cha "cambridge" Title zake zilijinadi: cambridge History, Cambridge Biology etc. Vilikuwa kama vya Nyangwine ndio maana nasema ana-copy mfumo wa zamani, he did not invent anything. Hivyo kusema watoto wanalemaa si kweli mbona wa zamani hamsemi walilemaa , maana walikuwa na vitabu kama hivyo hasa wakati wa mkoloni na mwanzoni mwa uhuru!
 
sijakubishia kwamba vitabu hivyo ubora wake una walakini.......lakini sio kweli kwamba ndiyo sababu kubwa ya kuwafelisha wanafunzi.......kwa sababu product ya miaka ya 2000 wengi tumetumia sana vitabu hivi na kiukweli wengi vimetusaidia sana.......hivyo vitabu unavyovitaja vinatumika hadi leo lakini katika baadhi ya shule tena zile za zamani tena vimebaki vichache sana kwa sababu serikali haijajisumbua kununua vingine na kuweka maktaba na mbaya zaidi shule nyingi hazina hata hizo maktaba........kununua Abbot, Lambert si mchezo.......wisho wa siku tunasema serikali yetu haijali elimu ya watu wa chini..........shule zote za serikali zinapotea kwenye ramani kiasi kwamba watu siku hawajali hata watoto wao wakichaguliwa mzumbe,ilboru,kilakala,pugu,tosamaganga,ndanda,galanos, kwiro, mpwapwa,moshi tech,tanga tech,tabora boys,msalato,..........n.k......siku hizi shule hizi zimechoka kama nini nyingi hazitamaniki......serikali inachezea elimu yetu......
 
Mfumo wa elimu wa Tanzania unahitaji postmortem
 
Hivyo vitabu vinalenga kujenga uwezo wa kukariri tu havimjengei mwanafunzi maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…