Vitambulisho vya NIDA ni Siasa au hupewa watu maalum

Vitambulisho vya NIDA ni Siasa au hupewa watu maalum

Jamani tuwe wakweli, hakuna siasa yeyote dhamira ni njema Vitambulisho vinatolewa kwa wote na si viongozi tu ingawa inaweza kuwa si kwa kasi tuliyotarajia. Namba ni nyingi mno zilizotolwwa na uzuri wameweka utaratibu wa huduma kutolewa kwa wenye namba kama ilivyonkwa wenye vitambulisho. Ukitazama kasi ya nida kwa sasa katika kuzalisha vitambulisho imeongezeka sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Nadhani tusilaumu tu lakini pia ni vema kupongeza kwa juhudi zinazofanyika binafsi naamini wote ambao hawajapata ambao nilisikia ikielezwa ni asilimia 50 ya walioandikishwa watapata.
Uongo
 
Ninavyojia mimi mchakato wa Kitambulisho cha Taifa ni mrefu kidogo kutokana na unyeti ID hiyo kwani uhakiki wa maombi hayo unahusisha taasisi nyingine pia na si nida pekee. Taasisi nyingine kama Uhamiaji, Tamisemi kupitia Serikali za mitaa n.k zina sehemu ya kujiridhisha pia. Hivyo si sahihi sana kulinganisha ID hiyo na kadi au document nyingine. ID ya nida ina beba dhamana ya usalama wa nchi, usalama wa mwombaji binafsi nk.

Sasa inakuaje wakupe namba alafu hardcopy ya namba ambayo tayari wameshakupa ichukue miaka? Si Bora wakunyime namba ikiwa Bado uhakiki unaendelea!!

Nadhani ni uzembe tu wa maksudi Ili kutengeneza mazingira ya rushwa. Nakumbuka kipindi naanza mchakato cheti Cha kuzaliwa Kilikua na shida kidogo ya spellings za majina na waligoma kubadili!! Kuna ofisa Mmoja aliniambia Niandae laki 7 nitapata NIDA Ndani ya wiki Moja. Yaani malipo siku ananiletea NIDA!!

Sasa najiuliza tukihonga inakuaje kipatikane ilihali tukifuata process tukose? Sasa hizi tamaa za rushwa ndio zinatuchelewesha
 
Unachosema kaka hiyo kweli. Mchakato wa maombi ya Kitambulisho unahusisha watu wengi katika hatua mbalimbali zikiwemo pia taasisi nyingine. Unapataje kwa siku moja? Na kama kuhonga pesa utawapa wote hao?
Inawezekana sana tu, mbona namba ilikua inatoka siku hiyo hiyo Tena mtandaoni kinachobakia ni print version/hardcopy pekee. Binafsi nilipata namba siku hiyo hiyo ila tatizo ni hardcopy so kama Kuna process za vitengo vingine kivipi namba iwepo (mpaka unapata TIN,unafungua akaunti, unasajili line) alafu hardcopy ndio ichukue miaka?
 
Sasa inakuaje wakupe namba alafu hardcopy ya namba ambayo tayari wameshakupa ichukue miaka? Si Bora wakunyime namba ikiwa Bado uhakiki unaendelea!!
Hoja muruwa hii. Kama wamekupa namba inamaanisha uhakiki tayari umekamilika. Nini kinachelewesha kitambulisho kuchapwa?
 
Back
Top Bottom