Vitambulisho vya NIDA ni Siasa au hupewa watu maalum

Uongo
 
Uongo
 
Sasa inakuaje wakupe namba alafu hardcopy ya namba ambayo tayari wameshakupa ichukue miaka? Si Bora wakunyime namba ikiwa Bado uhakiki unaendelea!!

Nadhani ni uzembe tu wa maksudi Ili kutengeneza mazingira ya rushwa. Nakumbuka kipindi naanza mchakato cheti Cha kuzaliwa Kilikua na shida kidogo ya spellings za majina na waligoma kubadili!! Kuna ofisa Mmoja aliniambia Niandae laki 7 nitapata NIDA Ndani ya wiki Moja. Yaani malipo siku ananiletea NIDA!!

Sasa najiuliza tukihonga inakuaje kipatikane ilihali tukifuata process tukose? Sasa hizi tamaa za rushwa ndio zinatuchelewesha
 
Unachosema kaka hiyo kweli. Mchakato wa maombi ya Kitambulisho unahusisha watu wengi katika hatua mbalimbali zikiwemo pia taasisi nyingine. Unapataje kwa siku moja? Na kama kuhonga pesa utawapa wote hao?
Inawezekana sana tu, mbona namba ilikua inatoka siku hiyo hiyo Tena mtandaoni kinachobakia ni print version/hardcopy pekee. Binafsi nilipata namba siku hiyo hiyo ila tatizo ni hardcopy so kama Kuna process za vitengo vingine kivipi namba iwepo (mpaka unapata TIN,unafungua akaunti, unasajili line) alafu hardcopy ndio ichukue miaka?
 
Sasa inakuaje wakupe namba alafu hardcopy ya namba ambayo tayari wameshakupa ichukue miaka? Si Bora wakunyime namba ikiwa Bado uhakiki unaendelea!!
Hoja muruwa hii. Kama wamekupa namba inamaanisha uhakiki tayari umekamilika. Nini kinachelewesha kitambulisho kuchapwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…