[h=3]
VITAMBULISHO VYA TAIFA VYATENGEWA SH355BILLIONI WAKATI NCHI ZA WENZETU MPAKA PAKA NA MBWAA WANAVITAMBULISHO.[/h]
SERIKALI YA TANGANYIKA imesema itatumia
Sh355 bilioni kutengeneza vitambulisho vya taifa ambapo awamu ya kwanza itamalizika mwishoni mwa mwaka huu.Hayo yabainishwa na Waziri wa Fedha , Mustafa Mkulo jana alipokuwa akiwasilisha bajeti ya mwaka 2011/12 bungeni mjini Dodoma.
kabla hujatowa vitambulisho wajengeeni hawa watoto wa mabarabarani nyumba za kulala,skuli,maji,umeme,madawa wakiumwa,nguo,viatu,na wao wawe na maisha mazuri kama watoto wenu au mutaona raha nyinyi watoto wenu wawe kama hivi..?
Alisema kwa kutambua umuhimu wa vitambulisho vya taifa, serikali imekamilisha taratibu za kumpata mzabuni na kwamba tayari mkataba umekwisha sainiwa.Mradi huu utagharimu jumla ya
shilingi bilioni 355 mpaka utakapokamilika na awamu ya kwanza ya kutengeneza vitambulisho hivyo itakamilika mwishoni mwa mwaka
2011,alisema Mkulo.
ona mkulo utakubali baba yako au mama yako awe hivi na wewe unatowa pesa kutengeza vitambulisho au kwanza utamuwekea mahali paa kuishi kisha ndio uanzishe vitambulisho...?
Alisema katika awamu ya kwanza jumla ya
Sh70 bilioni zitatumika kuzalisha vitambulisho hivyo kama ilivyopangwa.Aliongeza kuwa mradi huo ukikamilika utawawezesha wananchi kuwa na utambulisho na hivyo kusaidia kuongeza wigo wa
ulipaji wa kodi pamoja na mambo mengine.
kwa hiyo ni vitambulisho vya kuzidi kuwabana watu ili mujuwe nani kalipa kodi na nani hajalipa kodi sasa ndio maendeleo hayo ya nchi au ndio munawamaliza wananchi..?
Pia alisema vitambulisho hivyo vitasaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha na kuwatambua wahamiaji haramu.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha alinukuliwa na vyombo vya habari akisema, utekelezaji wa mradi huo utakuwa mgumu kutokana na Tanzania kuwa na watu 26milioni wanaostahili kupata vitambulisho hivyo.Pia alisema vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa kwa
wanafunzi,wafanya biashara wakubwa,pamoja na wafanyakazi.
hichi ni kitambulisho cha mbwa hata sio binadamu ni mbwa nyinyi majuha munasema vitambulisho wapewe wanafunzi,wafanyakazi,na wafanya biashara wakubwa..?ujuha gani muliyokuwa nao nyinyi kama ni kitambulisho kila mtu anahaki yakuwa nacho ikiwa ni rai sio mwanafunzi,mfanyabiashara ona hapa mbwa mbwa anakitambulisho nyinyi viongozi au shahalabalah tuuuuuuuu..?
ona mbwa mbwa
ona mpaka paka pia kwasababu taarifa zao zinafahamika kwa urahisi. Nahodha alisema, vitambulisho hivyo vitatumika pia katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaostahili na kubainisha kuwa wapo wanafunzi wanaopewa mikopo huku wakiwa hawastahili
NYINYI VIONGOZI WACHENI UJINGA ULIMWENGU USHAMKA MUNACHEKWA NCHI ZA WATU WANAKUCHEKENI TENA SANA TU WANAKUONENI MAJUHA WA MWISHO KABISA ATI KWA SABABU TAARIFA ZAO ZINAFAHAMIKA KWA URAHISI SASA BINADAMU MWENGINE KAMA SIO MWANAFUNZI,MFANYABIASHARA MKUBWA NA MFANYAKAZI TAARIFA ZAO HAZIFAHAMIKI KWA URAHISI..?BASI NDIO PAKUWAPA VITAMBULISHO WOTE ILI WAFAHAMIKE NYINYI MAJUHA KWELI KWELI ONA NCHI ZA WATU MPAKA MBWA NA PAKA WANAFAHAMIKA NYINYI WANANCHI WENU WENYE HAMUWAFAHAMU SASA VIPI MUNAONGOZA NCHI NYINYI MAJUHA.....?