Zainab Tamim
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 1,293
- 583
- Thread starter
-
- #201
Sawa kabisa, tumeiona.Nimetuma kwenye Namba ya tigo sasa hivi
naona majina ya ki-islam tu, je ni saccos ya misingi ya kiislamu ama?
ungeweka vigezo vya mtu kuja kupata mkopo maana mwisho wa yote ni,mtu kuja kupata mkopo maana leo naweza nikajiunga mwisho wa siku kumbe sina vigezo vya kupata mkopo.
so nivyema ungeeleza hafa vigezo vichache vya mtu kupata mkopo.
members wake ni watu wenye sifa gani?Islamic finance system. Bila riba.
Naweza kujiunga na ii saccoss ata sio diaspora je VP kuhusu taratibu za kujiunga!?
Nmefuatilia mjadala huu kwa mda kidogo ili kujiridhisha,nmekuwa interested sn,pls dada zainabu bado nafasi za kujiunga zpo?nami nijumuike.
members wake ni watu wenye sifa gani?
Kasome vizuri post namba moja.members wake ni watu wenye sifa gani?
Yale yale tu mkuu, mnazunguka zunguka tu lakn kuna riba tusidanganyane. Mm nahitaji gari linalouzwa milioni kumi sasa ivi ww unaenda kuninunulia alafu unanidai milion 12 alafu uniambie hakuna riba? Mm nataka nikikopa 10m nirejeshe 10m baada ya mwaka au zaidi, kinyume na hapo tusidanganyaneSio yale yale, ktk mfumo wa kiislamu mnaelewana wakt mifumo mingine unakuta mashart tayar. Pia mifumo mingne shart kubwa ni riba wakt huku hakuna riba.
Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.Yale yale tu mkuu, mnazunguka zunguka tu lakn kuna riba tusidanganyane. Mm nahitaji gari linalouzwa milioni kumi sasa ivi ww unaenda kuninunulia alafu unanidai milion 12 alafu uniambie hakuna riba? Mm nataka nikikopa 10m nirejeshe 10m baada ya mwaka au zaidi, kinyume na hapo tusidanganyane
Na hakuna mtu anayeweza kukupa milioni alafu ukamrudishia milioni baada ya mwaka labda ajazie pesa toka chanzo kingine kisichojulikana.Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.
Hakuna duniani atakaefanya biashara ya kukuuzia gari kwa bei aliyonunulia labda liwe bovu.
Kasome vizuri post namba moja.
Nimeipenda Sana.
Ninavyofahamu mimi na nilivyosoma kuhusu (mortgage) za bila riba, ni kuwa aidha kuna nyumba unaitaka kununua na hauna pesa za kutosha za mara moja basi financers wanainunua na kukukodisha (Ijara). Au kama unataka kujenga nyumba mpya basi unajengewa nyumba uitakayo na wenye kutoa mkopo lakini hiyo nyumba inakuwa ni ya wanaotoa mkopo na wewe wanakukodisha kwa kipindi mlichoelewana, na hiyo kodi kila inavyolipwa ndiyo unalipia na ununuzi wa hiyo nyumba (hire purchase).
Naomba upitie hapa: Ijara Canada - ijaraCDC
Suala la kununuliwa vifaa vya kujengea kwa hapa kwetu nadhani pia linawezekana na ni namna mtakavyojipanga watoaji mkopo, kwani hapo mnaweza kuwa ni retailers wa vifaa vya ujenzi ambavyo mnawauzia wakopaji wenu na wao wanalipa kama wamenunua duka la retail (hii ni kwa banks).
Njia nzuri nionavyo na yenye usalama kwa wote ni kuwa kama sisi tunaotaka kuanzisha kikundi cha wawekezaji ambae kila mkopaji atakuwa ni mwanachama wa hicho kikundi na moja ya miradi ni vifaa vya ujenzi kwa reja reja ambapo faida zitakuwa mara mmbili, faida ya kuuza vifaa vya ujenzi itarudi kwenye kikundi na faida ya wana kikundi kuweza kukopa bila riba.
Ni mjadala unaendelea na hayo ya mwisho ni mawazo tu yangu sio final say.
Napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa wote waliochangia mada hii hapa na wale wote wengine walioona wawasiliane nasi kwa kutupigia simu na wengine kwa whatsapp.
Uamuzi tuliofikia ni kuwa tunaanzisha haraka iwezekanavyo, saccos ambayo itasajiliwa kisheria na kanununi zote za nchi kuhusu vyama vya ushirika kuzingatiwa. Saccos yetu itakuwa ni wazi kwa wote watakao kujiunga pia tutahamasisha zaidi Watanzania wa diaspora kujiunga na saacos hii mpya.
Saccos itaendeshwa kwa kuwekeza kwenye vitu vinavyokubalika kihalali na pia saccos haitatoza riba kwa wanachama wake pindi watakapohitaji mikopo.
Kutakuwa na kamati ya awali ya uaunzilishi wa saccos, kikao cha kwanza kitafanyika tarehe 1 May 2017 hapa kwetu Kibaha, Misugusugu, mtaa wa vitendo.
Wale wote waliojiunga na group yetu ya Vitendo Action Group wamekaribishwa rasmi.
Siku ya mkutano huo wa awali kutakuwa na agenda zifatazo:
Introduction
- Kujulishana na kujuana wote, nani ni nani.
- kutambulisha miradi iliyopo na inavyoendelea.
- kutambulisha sabuni mpya zilizotengenezwa kwa udongo wa Aunt Zainab's Natural Super Clay.
- maswali na majibu.
Saccos
- Kuongolea saccos mpya itayoanzishwa na kutengeneza njia (road map) ya kuianzisha.
- maswali na majibu.
Uwekezaji
- kuelezea uwekezaji mpya unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
- maswali na majibi.
Lunch
- Chakula cha mchana kimeandaliwa, tutakula saa saba kamili.
Tunaomba wote wanaohusika wafike mapema, maongezi yetu ya maendeleo yaanze saa nne kamili.
Asanteni.
Abdul
Tumekuelewa vizuri sana.Ufafanuzi wako ni wa kisomi.Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.
Hakuna duniani atakaefanya biashara ya kukuuzia gari kwa bei aliyonunulia labda liwe bovu.
Tumekuelewa vizuri sana.Ufafanuzi wako ni wa kisomi.
Na hakuna mtu anayeweza kukupa milioni alafu ukamrudishia milioni baada ya mwaka labda ajazie pesa toka chanzo kingine kisichojulikana.