Ninavyofahamu mimi na nilivyosoma kuhusu (mortgage) za bila riba, ni kuwa aidha kuna nyumba unaitaka kununua na hauna pesa za kutosha za mara moja basi financers wanainunua na kukukodisha (Ijara). Au kama unataka kujenga nyumba mpya basi unajengewa nyumba uitakayo na wenye kutoa mkopo lakini hiyo nyumba inakuwa ni ya wanaotoa mkopo na wewe wanakukodisha kwa kipindi mlichoelewana, na hiyo kodi kila inavyolipwa ndiyo unalipia na ununuzi wa hiyo nyumba (hire purchase).
Naomba upitie hapa:
Ijara Canada - ijaraCDC
Suala la kununuliwa vifaa vya kujengea kwa hapa kwetu nadhani pia linawezekana na ni namna mtakavyojipanga watoaji mkopo, kwani hapo mnaweza kuwa ni retailers wa vifaa vya ujenzi ambavyo mnawauzia wakopaji wenu na wao wanalipa kama wamenunua duka la retail (hii ni kwa banks).
Njia nzuri nionavyo na yenye usalama kwa wote ni kuwa kama sisi tunaotaka kuanzisha kikundi cha wawekezaji ambae kila mkopaji atakuwa ni mwanachama wa hicho kikundi na moja ya miradi ni vifaa vya ujenzi kwa reja reja ambapo faida zitakuwa mara mmbili, faida ya kuuza vifaa vya ujenzi itarudi kwenye kikundi na faida ya wana kikundi kuweza kukopa bila riba.
Ni mjadala unaendelea na hayo ya mwisho ni mawazo tu yangu sio final say.