Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Nimetuma kwenye Namba ya tigo sasa hivi
Sawa kabisa, tumeiona.

Tunaomba tutumie majina yako matatu kwa WhatsApp 0625249605 tukuweke kwenye register na kukuunga kwenye group letu la WhatsApp ambapo utashiriki kikamilifu kuunda ushirika wetu.
 
ungeweka vigezo vya mtu kuja kupata mkopo maana mwisho wa yote ni,mtu kuja kupata mkopo maana leo naweza nikajiunga mwisho wa siku kumbe sina vigezo vya kupata mkopo.
so nivyema ungeeleza hafa vigezo vichache vya mtu kupata mkopo.
 
Falsafa yetu ni kuwezeshana.

Mikopo kwa kuanzia itakuwa ya aina mbili, mikopo ya maendeleo na mikopo ya dharura.

Masharti ndio wanachama waliojiunga wanayapanga hivi sasa.
 
Rozella ipo Dodoma, bei 6,500/= kwa kilo.

IMG-20170607-WA0016.jpg
 
Nmefuatilia mjadala huu kwa mda kidogo ili kujiridhisha,nmekuwa interested sn,pls dada zainabu bado nafasi za kujiunga zpo?nami nijumuike.
 
Ndugu @content manager au Moderator ku merge uzi huu wa kuanzisha SACCOS na ule wa biashara za wana saccoss tunaona si sawa kwani ni nyuzi mbili tofauti zenye maudhui mawili tafauti. Tunauomba uongozi wa JF uzi unmerge kama zilivyokuwa mwanzo kwa faida ya wengi.

Asante.
 
Nmefuatilia mjadala huu kwa mda kidogo ili kujiridhisha,nmekuwa interested sn,pls dada zainabu bado nafasi za kujiunga zpo?nami nijumuike.

Karibu sana, bado unaweza kujiunga nasi.

Kwa maelezo zaidi WhatsApp 0625249605.
 
Wadau,

Tuna furaha kubwa kuwajulisha kuwa leo tumeanza rasmi kuvuna zao la Azolla ambalo sisi wa Vitendo SACCOS tunallita zao mkombozi.

Azolla ni 100% asilia na ni lishe ya mifugp yote, yenye ubora kuliko lishe yoyote ya mifugo ya nafaka au ya kiwandani, ni 100% chemical free.

Sasa utaalamu wa Azolla unapatikana Vitendo SACCOS na tumedhamiria kulifanyia kazi zao hili kuwa ni mkombozi wa wafugaji na wakulima. Azolla licha ya kuwa ni lishe ya mifugo pia ni mbolea nzuri sana ya asilia.

Azolla inapunguza gharama za lishe kwa mifugo, kwa uchache, kwa asilimia hamsini na zaidi ukilinganisha na lishe za viwandani na ni asilia 100%.

Kwa maelezo zaidi...
IMG-20170525-WA0028.jpg

Faida kwa wengi.

Whatsapp 0625249605
 
Sio yale yale, ktk mfumo wa kiislamu mnaelewana wakt mifumo mingine unakuta mashart tayar. Pia mifumo mingne shart kubwa ni riba wakt huku hakuna riba.
Yale yale tu mkuu, mnazunguka zunguka tu lakn kuna riba tusidanganyane. Mm nahitaji gari linalouzwa milioni kumi sasa ivi ww unaenda kuninunulia alafu unanidai milion 12 alafu uniambie hakuna riba? Mm nataka nikikopa 10m nirejeshe 10m baada ya mwaka au zaidi, kinyume na hapo tusidanganyane
 
Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.

Hakuna duniani atakaefanya biashara ya kukuuzia gari kwa bei aliyonunulia labda liwe bovu.
 
Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.

Hakuna duniani atakaefanya biashara ya kukuuzia gari kwa bei aliyonunulia labda liwe bovu.
Na hakuna mtu anayeweza kukupa milioni alafu ukamrudishia milioni baada ya mwaka labda ajazie pesa toka chanzo kingine kisichojulikana.
 
Nimeipenda Sana.

Ninavyofahamu mimi na nilivyosoma kuhusu (mortgage) za bila riba, ni kuwa aidha kuna nyumba unaitaka kununua na hauna pesa za kutosha za mara moja basi financers wanainunua na kukukodisha (Ijara). Au kama unataka kujenga nyumba mpya basi unajengewa nyumba uitakayo na wenye kutoa mkopo lakini hiyo nyumba inakuwa ni ya wanaotoa mkopo na wewe wanakukodisha kwa kipindi mlichoelewana, na hiyo kodi kila inavyolipwa ndiyo unalipia na ununuzi wa hiyo nyumba (hire purchase).

Naomba upitie hapa: Ijara Canada - ijaraCDC

Suala la kununuliwa vifaa vya kujengea kwa hapa kwetu nadhani pia linawezekana na ni namna mtakavyojipanga watoaji mkopo, kwani hapo mnaweza kuwa ni retailers wa vifaa vya ujenzi ambavyo mnawauzia wakopaji wenu na wao wanalipa kama wamenunua duka la retail (hii ni kwa banks).

Njia nzuri nionavyo na yenye usalama kwa wote ni kuwa kama sisi tunaotaka kuanzisha kikundi cha wawekezaji ambae kila mkopaji atakuwa ni mwanachama wa hicho kikundi na moja ya miradi ni vifaa vya ujenzi kwa reja reja ambapo faida zitakuwa mara mmbili, faida ya kuuza vifaa vya ujenzi itarudi kwenye kikundi na faida ya wana kikundi kuweza kukopa bila riba.

Ni mjadala unaendelea na hayo ya mwisho ni mawazo tu yangu sio final say.

Napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa wote waliochangia mada hii hapa na wale wote wengine walioona wawasiliane nasi kwa kutupigia simu na wengine kwa whatsapp.

Uamuzi tuliofikia ni kuwa tunaanzisha haraka iwezekanavyo, saccos ambayo itasajiliwa kisheria na kanununi zote za nchi kuhusu vyama vya ushirika kuzingatiwa. Saccos yetu itakuwa ni wazi kwa wote watakao kujiunga pia tutahamasisha zaidi Watanzania wa diaspora kujiunga na saacos hii mpya.

Saccos itaendeshwa kwa kuwekeza kwenye vitu vinavyokubalika kihalali na pia saccos haitatoza riba kwa wanachama wake pindi watakapohitaji mikopo.

Kutakuwa na kamati ya awali ya uaunzilishi wa saccos, kikao cha kwanza kitafanyika tarehe 1 May 2017 hapa kwetu Kibaha, Misugusugu, mtaa wa vitendo.

Wale wote waliojiunga na group yetu ya Vitendo Action Group wamekaribishwa rasmi.

Siku ya mkutano huo wa awali kutakuwa na agenda zifatazo:

Introduction
- Kujulishana na kujuana wote, nani ni nani.
- kutambulisha miradi iliyopo na inavyoendelea.
- kutambulisha sabuni mpya zilizotengenezwa kwa udongo wa Aunt Zainab's Natural Super Clay.
- maswali na majibu.

Saccos
- Kuongolea saccos mpya itayoanzishwa na kutengeneza njia (road map) ya kuianzisha.
- maswali na majibu.

Uwekezaji
- kuelezea uwekezaji mpya unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
- maswali na majibi.

Lunch
- Chakula cha mchana kimeandaliwa, tutakula saa saba kamili.

Tunaomba wote wanaohusika wafike mapema, maongezi yetu ya maendeleo yaanze saa nne kamili.

Asanteni.

Abdul

Hiyo ni biashara si riba kwa vigezo vyovyote vile.

Hakuna duniani atakaefanya biashara ya kukuuzia gari kwa bei aliyonunulia labda liwe bovu.
Tumekuelewa vizuri sana.Ufafanuzi wako ni wa kisomi.
 
Na hakuna mtu anayeweza kukupa milioni alafu ukamrudishia milioni baada ya mwaka labda ajazie pesa toka chanzo kingine kisichojulikana.

Tena mpango wa kukopa bila riba unaweza kuhitahiji kukopa million kumi ukaishia kukopa million tano tu kwani anaekukopesha ataingia ubia na wewe kwa kukupa million 5 deni na kuwekeza million tano mgawane faida mpaka utapomaliza deni.

Hapo utaona raha ya mikopo bila riba.

Kwanza ulitaka burden ya kukopa 10m imekuondokea na umeishia kukopa tano tu. Na unailipa bila riba hata senti tano.

Hilo sijui kama unalielewa.
 
Back
Top Bottom