Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Kama nimeelewa vizuri, cha msingi na muhimu zaidi, mtu kuwa na wazo la biashara lenye tija au kuwa na biashara inayoendelea inayohitani kuongeza mtaji ili ikue au kuboresha huduma.

Unapopewa mkopo huku, kunakuwa na nafasi ya majadiliano kuangalia kwamba faida inapatikana vipi, kiasi gani na endapo mtu atawekeza, kukopesha, mtagawana vipi hiyo faida?

Hii ni tofauti na riba za sehem nyingine, wao ukichukua pesa, iwe ni matibabu, au kumidhi shida yeyote ile hata kama sio biashara, wameshaweka riba iko palepale haujadiliani nao.

Nafikiri hii kwa ufupi ndio tafsiri ya mkopo bila riba, hapo mwalimu wangu wa muda wote FaizaFoxy atanisahihisha na kuongezea mapungufu.
 
Nami nahitaji kujiunga
 
Nami nahitaji kujiunga
Karibu sana.

Kujiunga nasi unatutumia kiingilio cha Shillingi 10,000 kupitia namba 0756803528 au 0656399856

Na majina yako kamili (matatu). Tunakuingiza kwenye register yetu na kukuunga kwenye WhatsApp group ya Vitendo SACCOS ambapo utashiriki kikamilifu kama sisi sote.
 
*Tangazo la Kujiunga VTS Training Forum*
VTS Training Forum inatangaza nafasi za kazi za kujitolea katika Kada mbali Mbali. Hii ni kutokana na uhitaji wa VTS kupata wataalam ambao tutasaidiana katika kutatua changamoto zinazotukabili katika ushirika wetu. Katika kufanikisha malengo yetu tunaomba wataalamu wenye taaluma zifuatazo watume majina yao. High involvement and commitment inahitajika ili tuweze kufikia malengo...
*Wenye taaluma zifuatazo mnakaribishwa sana:*
1.Kilimo
2.Apiculture/beekeeping
3. Setting up greenhouse
4. Mifugo
5. Food scientists
6.Hydroponic
7.Aquaculture
8.Aquaponics
9. Horticulture
10. Handicrafts
11. Basket weaving
12. Cooperative
13. Islamic finance
14. Project write up
15. Entrepreneurial skills
*_Na kwa yoyote ambaye taaluma yake haikutajwa asisite kuwasiliana nasi_*
*Tafadhali wasiliana na mratibu wa mafunzo Bi Asha kwa maelezo zaidi.*
*VTS...KWA MAENDELEO YETU*
Ahsanteni na karibuni sana. Kwa maelezo zaidi WhatsApp 0625249605
 
Wana VTS,

KUMEKUCHA!

Kila mwana VTS hapa jukwaani anaombwa aandike mradi au biashara yake ya kila siku ambayo kwayo ataombea mkopo vitendo saccos: (Kama mtaji wako unazidi milioni mbili; Tuma mchanganuo jukwaa la vitendo biashara; Hapa watume wale wenye michanganuo chini ya milioni mbili) Ajibu maswali yafuatayo: 1.Jina la biashara
2.Eneo unalofanyia
3.mauzo au mapato kwa siku ni kiasi gani?
4. matumizi ya biashara kwa siku ni kiasi gani
4.Una watu wangapi wanakutegemea?
5.unahisi mkopo wa kiasi gani utakuza biashara yako?
6. Elezea matumizi na mapato ya mkopo huo?
7.Una muda gani tangu uanze biashara hiyo?
8. Ukipewa mkopo utaihakikishia vipi VTS kuwa utaurudisha mkopo?

9. Utakuwa tayari kamati ya saccos kutembelea biashara yako, kukupa ushauri wa kitaalaamu, kukupa mafunzo ya ziada kuhusu ujasiriamali?
10.Upo tayari kuwa mbia na saccos katika biashara kipindi chote cha mkopo mpaka utakapomaliza deni?
11. Una madeni mengine nje ya saccos yanayohusiana na biashara yako?
 
kila post naona namba za simu kwa kutumia whasap sasa wasio na hzo simu mnawasaidiaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…