Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba


Ukopeshaji wetu ni tofauti.

Tunakopesha kwenye mradi tu ambao nasi tunakuwa wabia. Kwa maana hiyo faida na hasara ni kwa wote.

Pia kwa wanachama tunakopesha mikopo ya dharura zilizoainishwa. Bila riba.

Nakuhakikishia VTS hatuna riba.
 
Ukopeshaji wetu ni tofauti.

Tunakopesha kwenye mradi tu ambao nasi tunakuwa wabia. Kwa maana hiyo faida na hasara ni kwa wote.

Pia kwa wanachama tunakopesha mikopo ya dharura zilizoainishwa. Bila riba.

Nakuhakikishia VTS hatuna riba.
Bi Mrembo, Mzee Abdul akianza kukusanya pesa za mradi wa excavator nijulishe, maana nategemea kusafiri kiduuuchu, ntakuwa kwenye simu sipatikani. Email me.
 
Fursa ya kuwekeza kwa Mtanzania yeyote aliopo ndani na nje ya Tanzania.

Sasa unaweza kuwasiliana na waliokwisha wekeza kwetu na kujipatia majibu mubashara.

Kidole kimoja hakivunji chawa.

Hii nimeipenda.

Mimi shahidi wa kwanza. Nimewekeza miradi yako yote. Wa kwanza ulikuwa wa sand mining nikapata ntaji wangu na 50% faida ndani ya miezi miwili.

Mradi mwengine ni wa bodaboda, nashukuru pesa nilizowekeza zimerudi na sasa nasubiri faida ule wa pili. Ule wa kwanza na kula faida.

Mradi wa sand mining wa pili pia nimewekeza na napata malipo mara kwa mara.

Nnatumai wapo wengine waliowekeza na wapo humu JF wajitokeza waelezee ukweli.

Hongera sana Mzee Abdul kwa kuwa yu muwazi na mkweli naahidi hata pesa yangu ya mwisho ntawekeza kwake.

Ahsante sana Bi Zainab Tamim, keep up the good work ya kum keep busy huyo mzee, day and night. Kwi kwi kwi teh teh teh.
 

Asante kwa kujitokeza.

We kiajuza huachi ukware, hiyo day and night inahusu nini. Pambaf.
 
Update...

Wadau,

Kwanza tunashukuru AlhamduliLlah mkutano umeenda vizuri na umeisha salama.
Tunafuraha kuwafahamisha wadau wote kuwa mkutano umeenda vizuri kabisa na umefana sana.

Tulianza kwa kukaribishwa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vitendo...

Kisha nikaongea kidogo mimi kuwakaribisha wajumbe wote...

Baada ya hapo ikaanza semina ya ushirika iliotolewa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Kibaha, Bwana Msangi. Semina ilikuwa ndefu kidogo lakini ilitoa mwangaza mpana wa nini SACCOS, vipi iongozwe, nini haki za Wana SACCOS na vipi haki zao zinalindwa na kusimamiwa na sheria rasmi za vyama vya ushirika na vipi serikali inasimamia vyama vya ushirika.

Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha.

Kamati hio ya muda ikamteua Katibu wa kwanza wa muda wa Vitendo SACCOS Ltd., chini ya usimamizia wa Afisa Ushirika wilaya ya Kiabaha.


Mambo yote hayo yapo kwenye video na picha. Zitakapokuwa tayari, tutapandisha video YouTube na kwenye tovuti yetu (inayoanadaliwa kwa sasa) tutapandisha video na picha.

Tunakaribisha maswali.

Asanteni na karibuni kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. kwa faida ya wengi.

Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Mobile / Whats-app 0625249605
 
Wanachama na Wana hisa wa Vitendo SACCOS wanategemea kuzindua na kuanza kazi miradi yao mitatu mipya hivi karibuni.

Miradi hiyo mitatu yote iliyo nje ya Vitendo SACCOS lakini imebuniwa na Wana VTS na itaendeshwa kwa njia ya kuchangiana mitaji na kugawana faida kwa muda maalum.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni, mradi wa ukumbi wa sinema na mikutano, unaoweza kukaa watu 100, unatambulika kama mradi wa Vitendo Cinema Hall. Huu ni mradi wa muda mfupi kwa waliowekeza. Inatarajiwa kuwa mara tu utakapoanza hivi karibuni, wote waliowekeza kwenye mradi huu kuanza kupata mafao yao na faida ndani ya miezi sita.

Mradi mwingi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni unaojulikana kwa jina la Vitendo Bricks, mradi huu ni wa muda wa kati. Mradi huu utajumuisha utengenezaji wa matofali ya aina tofauti tofauti na pia kwa siku za mwanzoni unatarajiwa kuwa na bidhaa tofauti zinazotokana na mchanga, kokoto na simenti.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa zote za ujenzi zinazotokana na simenti, kokoto na michanga.

Mradi mwengine kuanza hivi karibuni ni mradi wa kijiko (excavator) ya kuchimba na kupakilia mchanga. Mradi huu upo kwenye matayarisho ya mwisho na unategemewa kuanza hivi karibuni. Huu ni mradi unaotarajiwa kuanza kulipa mafao ya wawekezaji na kukamilika ndani ya siku 365 za kazi.

Tunawakaribisha nyote kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. Kwa faida ya wengi.

Vitendo SACCOS imedhamiria kufanya mabadiliko ya uwekezaji Tanzania. Na sasa unaweza kuanza kuwekeza na VTS kwa kuanzia Shillingi 10,000 tu.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu au whatsapp namba 0625249605.

Ahsanteni sana.
 
Vitendo SACCOS inaendeleaje?

[emoji252] [emoji479]
 
Wish I was with you guys.

Nililiona pilau kwenye picha kwenye group. Count me in Zainab, nitilie pesa za membership, sina access ya account ya Mpesa wala Tigo for now.

Will talk to you on the phone.

Keep it up.
Una updates za hii kitu?
 
mambo yakoke huko aisee ?

Inaendelea ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…