Kwanza awali ya yote nipongeze jitihada ya ya kila Mwanachama ambaye anapinga kwa vitengo vya ushoga kwa nguvu kubwa na ninawaomba nguvu ya kufanya hivyo,lakini pia nawaombea wale wanaobeZa jitihada hizo na Mungu awape uongofu.
Nakumbuka nilipokuwa mwaka wa 2 katika chuo kikuu cha Dar es salaam nilisoma somo la Ethics ambayo nadharia mbalimbali zipo kwa ajili ya kuguide Maamuzi ya watumishi Nadharia ya "Utalitarism" ambayo imetokana na neno Utility (Matumizi) ambapo lengo la kuwepo nadharia hii ni kutaka kujua usahihi au uhalali wa maamuzi ambayo unachukuliwa katika sehemu tofauti za serikali au mtu yeyote,nadharia inasema ukitaka kujua jambo ni sahihi unatakiwa kuangalia matokeo (consequence) kama maamuzi yamewapa furaha watu wengi basi maamuzi hayo ni sahihi na kinyume chake ni dhambi kwa wote.
Ushoga na usagaji siyo jambo jipya kwenye masikio yetu hata kwenye vitabu vya dini wameonesha kuwapo kwa watu ambao walishafanya sana(watu wa mtume Nuhu) dhambi hiyo ambapo matokeo yao yalikuwa mabaya kwao kwa kupokea adhabu kubwa ya kupinduliwa ardhi.
Katika jamii yetu suala hili la ushoga limekuwa ni lenye majuto na kuibua hasira kwa watu wengi sana kwani jambo hilo ni chukizo kwa kila Imani (Rejea Hadithi ya mtume Nuhu) na hata pia katika vitabu vitakatifu vimebainisha kuwa ni katazo kwa kila Mwanamke na Mwanaume(78:8 Qur'an).
SUALA la ushoga si la kulifumbia macho mamlaka inatakiwa kulizibiti kabla halijawa kubwa na,jukumu letu wengine kulikema kwa moyo mmoja,Yapo Maamuzi magumu yanahitajika katika serikali kutumika (authoritative desicison) sababu ni kama serikali ikitumia njia ya Demokrasia itaendelea kudharauliwa hivyo nazani njia sahihi ni serikali kutumia mamlaka na nguvu katika kuondosha matatizo haya.
Mabepari wanatakiwa kujua kuwaka mstari wa kubainisha Value (maadili) na Rights(haki) kwamba vyote ni muhimu katika jamii ila kitu pekee kinachofanya jamii iweze kuishi ni maadili siyo haki ambazo zinaenda kupoteza utu wa kila mmoja wetu pamoja na kupotza sifa za Taifa kwa ujumla.
MADHARA
Kupotea kwa Maadili na Silka za Tamaduni zetu,tunapoteza kabisa uhalisia/bendera au uhuru wetu.
Kupoteauvu kazi ya Taifa,fikra,maono na weledi katika majumu unapungua kutokana na athari za saikolojia ya mapenzi ya jinsia moja.
Uvunjifu wa katiba ya jamuhuri ya muungano,Nembo ya Rais ni ishara ya kuwepo kwa jinsia tofauti ambazo zinalijenga Taifa