Mimi nawaweka mashoga makundi haya:
1. Waliozaliwa na hali hiyo
2. Waliojiingiza
Hawa wa aina ya pili, sitapenda kuwaongelea sana kwa sababu ni suala la kujitakia. Wengi wao ni tamaa za kifedha na hawa wengi ni wale wanajiona wana miili ya kuvutia lakini mifukoni na vichwani ni watupu.
Kuna wengine wanaingia si kwa sababu ya fedha lakini tu kashawishiwa na kajiingiza na kanogewa, hawa wengi ni watu wasomi na wana kazi na familia zao pia. Pia sitawaongelea sana, wamejitakia.
Ila kuna hawa wa kundi la kwanza, waliozaliwa hivyo, hawa wanahitaji kupewa jicho la pekee, kwa sababu wao wakidhibitiwa ni rahisi kupunguza tatizo.
Hawa huonyesha dalili mapema, ni wale watoto tangu wadogo wanakuwa na tabia tofauti na zile za kawaida za watoto wa kiume, michezo yao ni tofauti na mara nyingi hupendelea kukaa na watoto wa kike, dada na Mama zao. Huwakwepa kaka na baba zao.
Wanajiona hawako daraja moja na watoto wengine wakiume. Hizi dalili huwa tunaziona lakini zinapuuzwa, kumbe ni wakati muafaka kuzifanyia kazi.
Huyu akiwa kijana anajikuta hatamani wanawake, hana swaga za wakiume, haelewi hisia zake, ndio msongo wa mawazo huanza na kujitenga. Bahati mbaya sisi huwa tunawasema vibaya, hivyo amani wanaipata kwa kukaa na wasichana, na ndio wanazidi.
Ni rahisi kumsema na kumtukana akiwa wa watu ila akiwa kwenye familia yako ni kitu tofauti. Hakuna namna utamuondosha katika familia, ila akipata msaada anaweza kusaidika.
Wakina baba wanaweza kusaidia kiasi kikubwa, kuwa mtoto akionesha dalili tofauti wawe wanakaa nao mara nyingi, itasaidia mtoto kupambana na ile hali anayohisi...
Afundishwe kukubali kuwa hata walemavu wameumbwa na Mungu, lakini hapaswi kujisusa, zaidi kukaa karibu na Mungu na kupambana.
Hivi anaweza kushinda hisia, na hatimae akawa ni kijana wa kiume kawaida.
Kosa kubwa tunalifanya ni kusemea hivi vitu kwa ushabiki bila hata kuelewa, ila tunapaswa kurudi kwenye ngazi ya familia kupambana na hii hali.