Siku basha fulani likija kuleta mahari kwa ajili ya mwanao wa kiume na kujitambulisha kuwa ni mchumba wake wa muda mrefu, ndipo utakapokuja kutambua ukubwa wa tatizo la ushoga hapa nchini.
Licha ya tatizo la ajira kwa vijana wengi hapa nchini, wewe unakenua tu meno kwa kuwa mwanao ana bahati ya mtende ya kubadilisha kazi jinsi atakavyo, na ni mwenye juhudi ya kufanya uwekezaji licha ya umri wake mdogo, kumbe hujui kitu chochote kile nyuma ya pazia. Tatizo la ushoga lipo na tena limepiga hodi katika familia nyingi sana hapa nchini, ama kwa kujua ama kutokujua.
Usalama wa watoto ni mdogo sana. Si makanisani, misikitini, sunday schools, madrassa, kwa waganga wa kienyej, kwenye tution, katika school bus, ndani ya nyumba zetu, kwa bodaboda, kwa majirani, na kila mahali.
Ni lazima ufunge na kuomba kwa Mungu, ili familia yako isiwe muhanga wa tatizo hili.