Vitendo vya Ushoga vinaongezeka kwa kasi sana

Sababu kuu ni kwa sababu mataifa hayo yana mtazamo tofauti kuhusu masuala ya ushoga na masuala ya haki za binadamu. Katika mataifa mengi ya Magharibi, ushoga unatambulika kama haki ya kibinadamu na uhuru wa kujieleza kwa mtu binafsi. Kwa hiyo, serikali, mashirika na watu binafsi wanaweza kusaidia kukuza uelewa wa umma kuhusu ushoga, pamoja na kutoa ushauri, ushawishi na rasilimali zinazohitajika kwa watu wenye mwelekeo wa kimapenzi wa jinsia moja.

Mbali na haki za binadamu, kuna pia sababu nyingine ambazo zinachangia kuwepo kwa uhamasishaji na matangazo ya ushoga katika mataifa ya Magharibi. Kwa mfano, kuna baadhi ya watu ambao wanapenda kutumia masuala kama hayo kama zana za kisiasa kwa lengo la kuwagawa watu na kuunda kundi la wafuasi wanaoshiriki mtazamo wao. Aidha, kuna watu ambao wanapenda kufanya biashara kwa kutumia masuala haya kama vile kuuza bidhaa au kufanya kazi katika sekta ya burudani.

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kwamba, hali ya kuwepo kwa ushoga katika jamii zote haina ushawishi mkubwa kutoka mataifa ya Magharibi. Ushoga umekuwa sehemu ya tamaduni za binadamu kwa karne nyingi, na unaendelea kuwepo katika jamii zote duniani
 
Hayo mambo yanapata njia yakuenea kwetu kwasababu ya ujinga wetu wenyewe.Ukiona mtu amekwambia ufanye jambo la kijinga nikwasababu kakuona akili zako zinaweza zikakubali kuufanya.Kwahiyo kama unashawishiwa kufanya ujinga nawewe ukashawishika kuufanya mwenye kosa hapo niyule aliyekubali kufanya ujinga.Tungekua na akili timamu hakuna ujinga ambao ungepata nafasi.Hao wanaoleta huo ujinga wanaleta kwasababu wanajua udhaifu wetu ulipo.
 
hili litawaathiri wao kwa kasi zaidi kama ambavyo iliwatokea canada hadi kuishiwa na nguvu kazi ya taifa.
 
So sad. People of color are the major target. Depopulate black people. Lakini watu weusi wenyewe wako gizani.
 
Ujinga ndo unatufanya tuombe
 
Nasikia tu kuwa kuna muimbaji na mtangazaji wa redio hapo kwa Mwamposa ni shoga.

Naendelea kufuatilia kujua ukweli kama bulldozer anapinga ushoga kwa kumaanisha au anawaajili mashoga ila haungi mkono ushoga.
 
Huyo mchungaji anaishi dunia gani ina maana hajui kama hivi sasa watu wanawasha umeme kwa hasi kwa hasi na chanya kwa chanya!
 
WAAMINI WAASWA KUBOREHSA MALEZI ILI KUKOMESHA USHOGA NA USAGAJI.
Wakristo wakatoliki duniani leo tarehe 02/04/2023 wameadhimisha sikukuu ya matawi ikiwa ni mwanzo wa wiki ya kumbukumbu ya mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo (juma takatifu), sambamba na hili waamini wa kanisa katoliki jimboni Njombe (parokia ya Njombe Mjini) wameaswa kuboresha malezi kwa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya kikatili (ushoga na usagaji)

Akizungumza wakati wa adhimisho la misa takatifu ya matawi, Paroko wa parokia ya Njombe mjini pd. Francisco Changula amewahimiza wazazi kujenga urafiki na watoto wao, watenge muda wa kuzungumza na watoto wao badala ya kuwapa uhuru wa kutazama Tv hasa maudhui ambayo yanachochea vitendo viovu.
"Wazazi acheni kuwaruhusu watoto wabaki majumbani peke yao wakitazama Tv na michezo isiyo ya maadili kwa kigezo cha kuonesha kuwajali kwa kuwanunulia vitu vya thamani kama TV ,SIMU na kuwapa muda mwingi wawe peke yao".

Amewahimiza pia kuepuka mazoea ya kuwaachia wafanyakazi wa ndani yaani house-girls majukumu ya kuwalea watoto, "Wazazi acheni kuwapa majukumu ya malezi wafanyakazi wa dani yaani dada wa kazi, unauhakika gani kama anaakili timamu, je amepimwa milembe?" Aidha amewasihi wazazi watenge muda wa kukaa na watoto wao ili wazungumze bao wajue nini kinawakabili au nini kinaendelea kati yao.
"Watu wa Njombe mnatumia muda mwingi kutafuta pesa na kuacha Tv zizungumze na watoto wenu hampati muda wa kukaa na watoto kujua changamoto zinazo wakabili, mwishoni watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na wanashindwa kwa kusemea, wakizoea vitendo hivyo wanaona ni vya kawaida."

Pd. Chengula pia amkemea vikali baadhi ya imani za kishirikina hasa kujitafutia utajiri na kupewa masharti ya kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto. "Hakuna kanuni ya kiuchumi duniani inayo sema utatajirika kupitia kwa mganga wa kienyeji, tafuteni wataalamu wa uchumi wawaelekezeni njia halali za kukuza uchumi na siyo waganga wa kienyeji wanaotoa masharti ya kufanya vitendo viovu ambavyo ni chukizo kwa Mungu na kwa jamii".
Kuna baadhi ya mashoga wanazalishwa ama kutengenezwa kupitia imani za kishirikina na baadae wataona ni halali kufanya na kufanyiwa hivyo. "Mkoa wa njombe ni mkoa mchanga sana lakini unajulikana kwa matukio na takwimu mbaya, ni mkoa ambao una miaka 11 tangu uzaliwe lakini ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya mashoga." Amesema Padre Chengula

Aidha katika adhimisho la misa takatifu jeshi la polisi kupitia Dawati la jinsia limekemea vikali baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi pindi uhalifu unapotokea.
Jeshi la polisi pia limewaasa wananchi kufichua vitendo vya ushoga ili kubaini vyanzo vya matatizo hayo.

Jeshi hilo la polisi kupitia dawati la jinsia wilaya ya Njombe, limesema takwimu za vitendo vya ulawiti kwa wilaya ya Njombe siyo nzuri zinaharibu taswira ya mkoa wetu.
"Inawezekana ndani ya miaka 10 ijayo Njombe tutakuwa na wanaume wavaa suruali ili hali na wao wanatumika kama wanawake na wanaume wenzao" limesema jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia.

Na
Karisto Mwinuka
Njombe 02.04.2023
 
Watanzania haipiti siku bila kuzungumzia Ushoga....

Jamii forums hazipiti dakika kumi bila uzi wenye neno "shoga" kuanzishwa.
 
Nabii Mkuu Geor Davie yeye kwake poa wanaume kubinjuana na wanaume wenzao
 
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Kwanza kabisa nikupongeze na kukushukuru kwa ujasiri wako wa kupigana vita ambayo wote tunajua si rahisi.Unajua kabisa vita hii itakuletea maadui na utahatarisha maisha ila hujajali umejitosa na unapambana.Mungu akulinde kila uingiapo na utokapo baba yetu.

Mh. Mwakyembe mimi ni mzazi niliyejaliwa mtoto mmoja tu wa kiume na kama ilivyo kwa wazazi wote siku alipozaliwa nilimshukuru Mungu kunibariki dume la mbegu lakini kwa jinsi hali ilivyo mbaya nchini mwetu kwa sasa natamani angekua wa kike.Najiuliza nitalilinda vipi dume langu la mbegu lisiharibike kama watoto wengine wengi wa kitanzania wanavyoharibika.Eeh Mungu okoa vizazi vyetu.

Hata hivyo mkuu kukaa na kuogopa na kusikitika na kumuachia Mungu sio suluhisho.Suluhisho litapatikana kwa sisi watanzania wenzako kukupa support katika vita uliyoianza.

Mimi kama kama mtanzania,kama mzazi na kama mpinga ushoga ninakuandikia kwa kujiamini ya kwamba Mh. naomba unitafute ninalijua chimbuko la kweli na suluhisho la kweli la huu ushoga uliovamia jamii yetu.

Mh.Mwakyembe samahani kama nitakukwaza ila hao wazungu ni wahalifu ila sio waanzilishi wala sio waenezi wa ushoga katika jamii yetu.

Vijana wanaofanya huo uchafu na huyo mzungu wengi wao wanakua tayari walishayaanza hayo mambo.Sio rahisi kijana asiye shoga mwenye maadili yake akakubali kufanyiwa hivyo vitendo na huyo mzungu hata aahidiwe fedha kiasi gani.

Mh.Mwakyembe naomba uniamini baba yangu,kuna kitu huwa kinafanyika katika jamii yetu kilianza kama miaka 10 hivi iliyopita na huu ushoga mnaouona leo mimi niliuona ten years ago.(Sio maono ya kidini.Ni real life thing)

Mh. Mwakyembe,nakumbuka miaka 10 iliyopita kwa masikitiko sana nilikua nawaambia watu ya kwamba miaka 10 ijayo Tanzania itakua na Bisexual wengi sana ila hawakuniamini.Leo hii kuna wanaokumbuka nilichowaambia na wanasema "aisee ulisemaga hii kitu hatukukuamini".

Mh. Mwakyembe kisipofanyika kinachotakiwa kufanyika labda kwa miujiza ya Mungu tu ila miaka 10 ijayo mashoga watakua wengi sana hapa Tanzania na watakua na haki zao kama ilivyo huko ulaya na Marekani.

Wazungu hawasambazi ushoga bali wanataka mashoga ambao tayari tumewatengeneza wenyewe wapate haki za kuishi bila kunyanyasika,wawe na haki za kuoana na kuheshimiwa kama binadamu wengine.Yaani hapa namaanisha sisi tunawatengeneza halafu tunawakataa then mzungu anakuja kuwatetea kuwa tusiwanyanye.Sasa mzungu anapotaka waishi bila kubaguliwa ndipo tunaposema anatuletea ushoga nchini kwetu.

Mh.Mwakyembe mashoga wanatengenezwa nchini kila siku ,kila mahali mbele ya macho yetu kila mtu akiona.

Bila nguvu kubwa kuwekwa katika nitakachokuambia iwapo nitapata nafasi ya kuongea na wewe, basi tufanyayo ni sawa na kutibu homa bila kutokomeza kinachosababisha homa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kwanza huu uzi ufutwe maana hauna mantiki zaidi ya kuongeza content za vinyeo mtandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…