ONYO: MAKALA HII ISOMWE NA WAPENDA KUSHUGHULISHA AKILI NA SIO WANAOONGOZWA NA HISIA KUHOJI MAMBO
Jinsi tunavyouona ushoga jinsi ulivyouchafu, tunavyoupinga na kuukataa ndivyo wazee wetu walivyokuwa wakiiona dini ya Kikristo Wakati imeletwa.
Wazee wetu walipambana vilivyo wengine mpaka kupoteza Maisha ATI kisa kuukataa Ukristo. Afrika tulikuwa na Dini na miungu yetu. Tulikauwa na Mila na desturi zetu.
Ujio wa wazungu ilikuwa vita ya kihistoria ambayo imeacha mabadiliko makubwa mpaka hivi leo.
Ukristo haukuwa na uzuri wowote Mbele ya wazee wetu, Ukristo ulikuwa ni balaa kubwa.
Lakini wazungu walivipiga vita mpaka wakashinda, Mababu zetu wakasalimu amri wakiwa wamegaragazwa vibaya Kwa Hoja au Kwa viboko.
Vivyohivyo Kwa Uislam. Hakuna Mzee yeyote hata mmoja aliyeukubali uislam, ilikuwa ni vita naam Zama za vita, damu na Roho viliwatoka wengi.
Sasa Sisi ni kizazi cha nne tangu Ukristo umeingia Afrika,
Kwa sasa Ukristo ni Wimbo mtamu midomoni MWA Watu wengi.
Ingawaje Kwa Mababu zetu ulikuwa ni Wimbo wa maombolezo, kilio na Ole.
Zamu yetu imefika, tupo katika pambano Dogo Mno, wala Hii sio Vita Kwa sababu vita walipigana Mababu zetu. Kizazi cha nne hakitaweza kupigana vita tena na Mzungu. Kwani vita ilishakwisha, Kwa sasa ni mapambano madogo madogo.
Tupo katika pambano la kuukataa ushoga ambao katika jamii zetu sio Mila wala sio desturi.
Lakini hatuna hoja hata zenye mantiki za kukataa ushoga Kwa sababu kama tumeukubali Ukristo kama Dini licha ya kuwa hakuna Mila na desturi zetu za kiafrika zinazokubaliana na Ukristo.
Ikiwa Watu wameukubali Ukristo na NI waafrika Kwa nini Waafrika haohao wakatae ushoga?
Utagundua ni kuwa Hii sio Vita Bali kapambano kadogo tuu ambako Wazungu wameshinda mapema Kabla pambano halijaanza.
Mashoga wanaweza kuanzisha dini Yao na kujiita dini ya mashoga, mtawazuia Kwa kigezo kipi?
Mkisema sio utamaduni WA muafrika watawaambia kwani Ukristo au uislam ni utamaduni WA muafrika?
Kufikia hapo watakuwa wameshinda mapema Kabla hata kipenga cha pambano hakijapulizwa.
Ni unafiki na upunguani kupinga ushoga alafu muda huohuo kuukumbatia Ukristo na uislam,
Wazee wetu waliolala katika Ardhi yetu, licha ya kuwa walipoteza vita Ile na Wazungu lakini watabaki kuwa mashujaa WA Wakati wote Kwa kuupinga uzungu na mambo yake yote.
Nina uhakika, kama Ukristo ulikuwa unakataliwa na kupingwa na Wazee wetu kipindi unaletwa na Wazungu lakini Kwa sasa Watu wanachekelea kuwa Wakristo ndivyo hivyohivyo Ushoga utakavyokuwa Kwa Karne moja inayokuja.
Itakuwa NI kawaida, itakuwa NI dini kama dini zingine.
Na kama kuna Haki ya kuabudu dini yoyote Ile basi hatuna mamlaka ya kuwazuia watakaoamini katika ushoga.
Taikon kama Kuhani, msimamo wangu ni kuwa kama Watu wako Serious na kupigana vita vya Ushoga basi waanzie kwenye kuondoa Ukristo na Uislam Kwanza, wakiweza hapo basi kuundoa ushoga ni dakika moja tuu.
Hakuna Watu wanaofuata mambo ya utamaduni, Mila na desturi ambao watajiingiza kwenye ushoga Dunia ingalipo.
Ila wale wafuata Dini, Mila na desturi za kigeni kama Ukristo, uislam ni rahisi kuwa mashoga au kuzaa Watoto mashoga.
Pinga na kataa Ukristo na uislam, ili kuondoa Ushoga na matabia mengine ya kigeni.
Mbali na Hivyo kinachoendelea ni unafiki tuu! Na pambano hilo tumeshashindwa MAPEMA.
Nimemaliza