Alafu ulivokuwab
wewe utakuwa ni shoga tu. Ata kujieleza in summary umefeli.
MAFUNDISHO YA KANISA YALIYOZONGWA NA ULOFA WA KIFALSAFA, KISAYANSI NA KITEOLOJIA HAYANA NAFASI KATIKA KUTAKATIFUZA ULIMWENGU KWENYE MILENIA YA TATU: WAKUU WA KANISA KATOLIKI CHUKUENI HATUA ZA HARAKA
Mtumiaji wa akaunti ya jukwaa la JamiiForums.com yenye jina la
paqwa amekuwa na tabia ambayo nimeiona katika matukio kadhaa yanayowahusu Wakuu wa KANISA langu Katoliki kama ifuatavyo:
- Niliiona jambo hili, kwenye Kituo cha Hija cha Consolata, kule BUnju, Kinondoni, Mkoani Dar Es Salaam, wakati tunajadilia na kuandaa maoni ya CPT kwa ajili ya Tume ya Warioba ya Katiba Mpya.
- Nilishuhudiajambo hili kwenye mkutano wa Ex-seminarian pale Msimbazi, ulioandaliwa na Askofu Jude Thadeus Ruwaichi, wa JImbo Kuu la Dar Es Salaam.
- Jambo hili lilitokea tena wakati Padre Privatus Karugendo alipolazimishwa kuacha upadre kupitia Baraza la Kimahakama la Kanisa Katoliki. Kati ya mashtaka matano yaliyomkabili, mojawapo linahusu tuhuma kwamba alikuwa anahimiza watu kutumia kondomu kama kingamimba, kinyume cha msimamo rasmi wa Kanisa Katoliki, usemao kuwa kuhimiza matumizi ya kondomu ni sawa na kuhimiza ushoga.
- Na sasa tabia hiyo imejirudia kwa mtindo ule ule kupitia maoni ya mtumiaji wa akaunti ya paqwa. Kwa maoni yake, mtu yeyote anayesema kuwa hali ya ushoga (homosexual condition) na tabia ya kulawiti wanaume (homo-affective pedication) vinaweza, na vinapaswa kutenganishwa, kwa sababu hali ya ushoga ni sifa ya kimaumbile wakati tabia ya kulawiti wanaume ni zao la maamuzi binafsi, anakuwa ni shoga.
Mara zote hizi nimeona tabia ya aina hii: mtu anayepinga hoja rasmi ya Kanisa Katoliki, hata kama anazo sababu nzuri za kisayansi au kifalsafa, lazima anyamazishwe kwa mabavu, ama kwa kumvisha joho la ushoga au kuhamisha mada kwa kumwita mtetezi wa ushoga.
Katika hali ya sasa, tabia hii imegeuka kuwa umachiaveli wa kitaasisi ndani ya Kanisa Katoliki, maana inahusisha baadhi ya waseminari, baadhi ya mapadre na baadhi ya maaskofu.
Kwa sababu zote hizi, sasa nimeamua kujibu kwa ukamilifu, ili watu kama paqwa waelewe wapi wanachemka, na kama watapenda wajisahihishe. Naandika kupinga umachiaveli wa kitaasisi ndani na nje ya Kanisa Katoliki.
Kulingana na toleo jipya la Katekisimu ya Kanisa Katoliki (KKK 1750–1754), kila kitendo cha binadamu kinazo sehemu tatu: madhumuni, mbinu ya kufanikisha madhumuni hayo, na mazingira ya utekelezaji wa mbinu hiyo. Yaani,
the object, intention and circumstances.
Hizi zinaitwa fonti tatu za kimaadili. Kwa kutumia fonti hizi tatu, matendo yote ya watu yanaweza kugawanywa kwenye aina nane zifuatazo, aina ya kwanza pekee ikiwa ndiyo halali kimaadili:
Hivyo, sisi walei tunafundishwa na makuhani kuwa, kuna vigezo vitatu vya kupima uadilifu wa matendo ya wanadamu: malengo, mbinu na mazingira. Uadilifu wa tendo inapata dosari endapo kigezo chochote kati ya vigezo hivi vitatu kinafungamana na doa la uovu wa aina yoyote.
Kutumia hoja mbaya kufanikisha kengo zuri, la kupinga uovu wowote, kama vile ulawiti, uzinzi, uasherati, ubakaji, umalaya, hata kama hoja nzuri kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo hazipo, ni tabia ya umachiaveli.
Mfano hapa ni hoja zinazokiuka kanuni ya "NIFO (No-Is-From-Ought)" katika kusanifu hoja.
Mfano wa pili ni hoja zinazokiuka kanuni ya "NOFI (No-Ought-From-Is)" katika kusanifu hoja.
Mfano wa tatu ni hoja zinazokumbatia "type-token fallacy", ambayo sifa zinazohusu kundi la watu zinahamishiwa kwa kila mwanakundi, wakati baadhi ya wanakundi hawana sifa hizo.
Na mfano wa nne ni hoja zinazomshambulia mleta hoja badala ya kujielekeza kwenye hoka (attacking the arguer fallacy).
Hapa narejea tabia ya kujaribu kuficha ubaya wa hoja mbovu zinazotumika kupinga uovu kama vile ulawiti, kwa kuwaziba midomo wakosoaji wa hoja hiyo, tena kwa kuwachafua kwamba ama wao ni mashoga au watetezi wa ushoga.
Huu ni umachiaveli pia, ambao unafanywa na baadhi ya Mapadre na baadhi ya Maaskofu wangu Katoliki. Kwa hapa nahifadhi majina yao.
Katika muktadha huu, sasa hoja yangu ya msingi ni kama ifuatavyo:
1. KUna hoja kwamba, kwa kuwa muungano wa ngono ya jenitalia kwa jenitali kati ya mwanamke na mwanamume ni alama yenye maana ya ndoa; na kwa kuwa muungano wa ngono ya jenitalia kwa jenitali kati ya mwanamke na mwanamume ni alama yenye maana ya familia ya baba, mama na watoto wao wa damu; hivyo basi, kwa sababu hizo mbili, inafuata kimantiki kwamba, kuna muungano wa kudumu kati ya maana ya ndoa na maana ya familia. Lakini, hoja hii ingekuwa sahihi kimuundo na kimaudhui endapo: maana ya ndoa na maana ya familia ni semiotically inseparable, spatially inseparable, temporally inseparable, axiologically inseparable, causally inseparable, na theologically inseparable.
2. Lakini, tendo la ngono ya jenitalia kwa jenitalia kati ya mwanamke na mwanamume ni alama ambayo inabeba maana ya ndoa na maana ya familia, ambapo maana hizo mbili ni semiotically separable, spatially separable, temporally separable, axiologically separable, causally separable, na theologically separable. Yaani:
--
semiotically separable kwa sababu: tunapotumia neno lenye maana nyingi (polysemic signifier) kwenye sentensi kama vile, "nakupa mwili wangu ili uutumie kama njia ya kupata utulivu wa kimwili na kiakili (unitive meaning) kwa ajili kudumisha urafiki wetu (unitive meaning)" na "nakupa mwili wangu ili uutumie kama njia ya kupata mtoto atakayekuwa uzao wetu (procreative meaning)," tunakuwa tumechukua maana mojawapo katika sentensi husika na maana baki inawekwa kwenye mabano, yaani inawekwa kwenye "passive state" bila kuharibiwa, na hivyo kutenganisha maana hizo.
--
spatially separable kwa sababu: Tukio la kujamiiana (lenye kubeba maana ya ndoa) linatokea kwenye mwili wa mwanamke katika kituo kinachoitwa mfereji wa ngono/uzazi ndani ya uke (vagina), wakati tukio la kurutubishwa kwa yai (lenye kubeba maana ya familia) linatokea kwenye mwili wa mwanamke katika kituo kingine kinachoitwa mrija wa falopia (fallopian tube), ambapo kuna umbali ambao ni zaidi ya sentimeta saba kati ya vituo hivi viwili ndani ya mwili wa mwanamke.
--
temporally separable kwa sababu: Tukio la kujamiiana (lenye kubeba maana ya ndoa) linatokea kwenye mwili wa mwanamke katika kituo kinachoitwa mfereji wa ngono/uzazi kwenye muda T1, wakati tukio la kurutubishwa kwa yai (lenye kubeba maana ya familia) linatokea kwenye mwili wa mwanamke katika kituo kinachoitwa mfereji wa fallopia (fallopian tube) kwenye muda T2, ambapo kuna tofauti ya kimajira iliyo sawa na tofauti kati ya muda T1 na muda T2, yaani T2-T1, ambapo tofauti hiyo haiwezi kuwa sawa na dakika zero.
--
axiologically separable kwa sababu: Tunu ya ndoa, kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, tunu ya familia, sio tunu za msingi (basic human goods) mara zote. Bali ni tunu elekezi (instrumental goods) mara nyingine. Tunu elekezi zinaweza kudhoofishwa, kupuuzwa na kukiukwa bila kufanya kosa la kimaadili, endapo kufanya hivyo kunaleta matunda yenye thamani kubwa zaidi kwenye ustawi wa wahusika. Kujamiiana ni mchakato unaozalisha gameti za kiume zenye uwezo wa kurutubisha gameti za kike, na hivyo kuanzisha mchakato wa kuzaliana. Katika hali hii, kuzaliana ni mchakato unaohusisha msafara wa uhai kutoka kwa wazazi kwenda kwenye mimba ya mtoto. Lakini, uhai wa gameti ni tofauti na uhai wa mimba. Gamri ni sehemu ya mwili wa wazazi, wakati mimba ni misuli ambayo ni sehemu ya mwili wa kiumbe kipya. Hivyo, ni makosa kisayansi na kifalsafa kufikiri kuwa uhai wa gameti (sperm and ovum) unayo thamani sawa na uhai wa mimba. Yaani, "
respect for embryo does not entail respect for gametes." Kwa sababu hizi zote, kuzuia mchakato wa kuzaliana unaoweza kuhitimishwa kwa kuzalisha mimba unaweza kuwa ni uovu kwa sababu za kimazingira. Yaani "
contraception is extrinsically evil". Kwa sababu hii, waandishi wa
Vatican Minority Report (1966) walikosea wakati waandishi wa
Vatican Majority Report (1966) walipatia.
--
causally separable kwa sababu: Binadamu ni kiumbe mwenye akili ya kupanga, utashi wa kuchagua na uhai wa kimwili unaomwezesha kutekeleza matendo huru. Anaweza kuchagua kutobeba mimba kwa kuacha kufanya tendo la ngono au kwa kufanya tendo la ngono kwa kuzuia ujio wa mimba mpya. Anaweza kuzuia mimba kwa sababu mchakato wa kutungwa kwa mimba unazuilika kwa kutumia juhudi binafsi za kibinadamiu kupitia matendo ya kimwili. Matendo haya ni rahisi kufanyika kuliko jaribio la kubeba jiwe lenye kilo 1,000 kwa kutumia mikono yake pekee.
--
theologically separable kwa sababu: Under thick inseparability thesis which combines the good of procreation with the good of matrimonial union, hakuna maandiko kwenye misahafu yote ya Kikristo, Kiislamu, Kibuda, na vinginevyo, inayosema, na kutafsiriwa kwa kauli moja yenye kuonyesha kwamba, umoja wa wanandoa unapaswa kudumu, kila mahali, kila wakati na kwa kila jozi, hadi kifo kiwatenganishe. Hivyo, fundisho la thick inseparability thesis linabaki kuwa ni sera ya kisekta inayowahusu waumini wa madhehebu maalum pekee na Mungu wao.
3. Kwa hiyo, tamko kwamba, tendo la ngono ya jenitalia kwa jenitalia kati ya mwanamume na mwanamke ni alama ya ndoa na alama ya familia kwa mpigo, kiasi kwamba, maana hizi mbili zinatengeneza muungano usiopaswa kutenganishwa na mtu yeyote, mahali popote na wakati wowote, ni tamko batili semiotically, spatially, temporally, axiologically, practically, na theologically.
4. Wanateolojia wengi walioko kwenye Kambi ya Kanisa Katoliki hujenga hoja zao kupinga matumizi ya vizuia mimba, vizuia magonjwa ya kingono, ulawiti, mapenzi ya mdomo, mapenzi ya mapajani, mapenzi ya kwapani, kupiga punyeto, na matendo ya ngono baki yanayohitimishwa Kwa kumwaga manii nje ya jenitalia ya kike, Kwa kuanzia kwenye kanuni ya muungano wa kudumu kati ya maana ya ndoa na maana ya familia, zilizojadiliwa hapo juu.
5. Kwa hiyo, hoja hizi za wanateolojia walioko kwenye Kambi ya Kanisa Katoliki ni hoja batili kimaudhui, japo zinao muundo sahihi kimantiki.
6. Lakini, Kuna hoja mbadala, chini ya nadharia mamboleo ya maadili asilia zinazoweza na zinazopaswa kutumika kuthibitisha uharamu wa kimaadili wa baadhi ya matendo ya ngono kama vile tendo la ulawiti, bila kujali kama anayelawitiwa ni mwanamke au mwanamume, tena bila kufanya uhuni wa kushambulia haiba za wanazuoni wanaofanya kazi nzuri ya kufichua ubovu wa kinachoitwa kanuni ya umoja na uzazi katika Kila tendo la kutombana. Yaani, the principle of inseparability between the unitive and procreative significances of truly human sexual acts.
7. HIVYO, Maaskofu, mapadre, mafrateli na ex-seminarian Katoliki wanapaswa kuacha uhuni wa kushambulia waleta hoja na kujielekeza kwenye hoja zenye mashiko kimantiki, kiepiatemolojia na kimetafizikia katika kutajatifuza Ulimwengu.
(NB: Hata Mimi ni ex-seminarian, na nimeyajua haya yote Kwa sababu ya historia yangu hiyo)
WITO:
Hivyo, natoa wito maalum Kwa maaskofu na mapadre wenye medulla oblangata zilizotulia, kama vile Dr. Ruwaichi,.
Wanapaswa kuchukua hatua za haraka kuliokoa Kanisa Katoliki dhidi ya tishio la taasisi hii kugeuka jumuiya ya kishirikina, kwa sababu tu ya kulinda disputed traditional continuity.
Tabia ya kufikiri, kuhukumu na kutenda kana kwamba madili ya ngono ndio alfa na omega ya Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Muundo na Maisha ya Jamii inapaswa kufa.
Lakini sio hivyo tu. Mafundisho ya Kanisa yanapaswa kuborsehwa kwa kufanya mambo mawili yafuatayo:
1. Kuingiza fasili ya maneno "society" na "community" kwa mtazamo wa Kanisa Katoliki. Haiwezekani Kubuni Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Jamii bila kueleza Jamii inayokudusiwa ni Kitu gani na Sio Kitu gano. Ombwe hili lizibwe.
2. Kuboresha fasili ya maneno "society" na "community" inayotumika kwenye matini ya seminari Kuu. Fasili za sasa haziwapi nafasi mafrateri wetu kuelea maana ya neno dola. Semonari Kuu wanatumia fasili ya Austin Fagothey wakati huku uraiani tunatumia fasili ya Max Weber. Fasili ya Weber inao ubora fulani dhidi ya Fasili ya Fagothey kwa sababu inatofautisha "means" na "ends" katika kuongelea maisha ya kijamii.
Bila kuchukua hatua za kuhuisha Mafundishio ya Kanisa Kuhusu Muundo na Maisha ya Kijamii, tuhuma kama zile zilizotolewa na Rais SSH dhidi ya TEC, siku alipoongea na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 2 Desemba 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), zinaweza kuonekana za kweli siku moja.
Bahati nzuri ni kwamba, katika matamko 10 aliyoyarejea sijaona mahali walipoongelea "the principle of inseparability".
Kanisa Katoliki linaweza Kuwaburuza watu wote, wakiwemi wanasayansi na wanafalsafa uchwara, kwa muda mchache;
Kanisa Katoliki linaweza Kuwaburuza watu wachache, wakiwemi wanasayansi na wanafalsafa uchwara wa muda wote;
Lakini Kanisa Katoliki haliwezi Kuwaburuza watu wote, wakiwemo wananasayansi na wanafalsafa makini, Kwa muda wote.
Kwa ufupi: niseme kidogo kuhusu thin principle of inseparability dhidi ya thick principle of inseparability.
Kanuni ya umoja-na-uzazi Inaitwa "kanuni nyembamba" kwa sababu inajielekeza katika
kila tendo moja moja la ngono (act-by-act analysis).
Chini ya kanuni hii, kila tendo la ngono lazima libaki wazi kwa ajili ya kuruhusu uzazi na wakati huo huo kueleza muungano wa upendo. Kuzuia uzazi kwa kutumia njia za kisasa (vidonge, kondomu) katika tendo lolote lile kunavunja kanuni hii na kuchukuliwa kuwa ni dhambi.
Kanuni ya umoja-na-uzazi Inaitwa "kanuni nene" kwa sababu inajielekeza katika muktadha mzima wa maisha ya ndoa (totality or relational context) badala ya tendo moja moja.
Hapa, maana ya umoja na uzazi hazitakiwi kutenganishwa katika
ujumla wa maisha ya wapenzi. Hii inamaanisha kuwa kwa ujumla wake mahusiano ya kimapenzi lazima yawe ya upendo na yenye nia ya kuleta uzazi duniani.
Lakini haina maana kwamba kila tendo la ngono lazima liwe na sifa zote mbili kwa pamoja. Kwa hiyo, wapenzi wanaweza kutumia uzazi wa mpango wa kisasa kwa sababu halali bila kuharibu sifa ya msingi ya urafiki wao.
Baada ya kuweka bayana tofauti hizi bado nasisitiza kuwa:
1. The thin principle of inseparability between the unitive significance and procreative significance of truly hman sexual acts is indefensible under the natural moral theory
2. Similarly, the thick principle of inseparability between the unitive significance and procreative significance of truly human sexual acts is indefensible under the natural moral law theory, save under the sectarian theological moral theory as taught by the catholic church, and not otherwise.
It's time to think big outside the old catholic box by updating major seminary curricula and the catechism of the Catholic church to eliminate superstition- laden doctrines.
MAREJEO
Kwa ajili ya kuwafikia kirahisi wasomaji wa lugha ya iingereza, nimetafsiri makala haya kwenye lugha ya Kiingereza na kuiambatanisha kama nakala hapa chini pia.
Ndani yake kuna viambatanisho vya "working papers" kumi na tatu, kama marejeo maalum wakati wa kuandaa chapisho hili. Zinawafaa wasomaji wenye kipaji cha kusoma bila kuchoka, na hasa wale wanaoamini katka kanuni ya uekumene wenye msingi wake katika maadili asilia (natural alw based ecumenism).
.
Makala hizo kumi na moja naziambatanisha hapa kwa ajili ya wale wenye muda na ubavu wa kusoma kila kitu.