Mapenzi ya Jinsia moja ni jambo linalokemewa kwa Nguvu zote hapa Nchini, lakini bado linaendelea kushamiri kwakua wanaofanya ni kwa utashi wao na hakuna anayewakagua kujua kama wameanza kushiriki au La. Juzi nilikua natoka Mwanza mjini nikielekea Kwangu Mkolani, Nilishuka Nyegezi Stendi kisha nikachukua Bodaboda kwenda Majengo Mapya.. Wakati tunaelekea huko nikampa stori dereva yule, Baadaye akanisimulia kisa ambacho kiliniacha Mdomo wazi.
ni kwamba kuna siku moja alikua alimpakia kijana Lijali kwenye pikipiki yake akitokea Nyegezi Stendi kwenda Nyegezi Kona, wakati wakiwa njiani Yule kijana akaanza kumkumbatia bodaboda, akaanza kumtomasa.. Dereva mpaka akashindwa kuendesha bodaboda akasimama baada ya kusimama Kijana yule akatoa Burungutu la Fedha akampa huyo Bodaboda akimshawishi kwenda kumfanyia hicho kitendo.. Huyo Bodaboda kwa Maelezo yake alichukua Pesa akaondoa Pikipiki yake kwa kasi na akatokomkea, sasa najiuliza ni vijana wangapi wenye tamaa ya pesa wanaopewa na kujihusisha na mapenzi haya Haramu? iko haja kwa Elimu kutolewa kwa makundi haya Maalumu ili tusipoteze hiki kizazi.