SINGULARITY
Member
- Jul 9, 2014
- 8
- 16
Analojia rahisi kwenye hili ni kufananisha Strait ya Hormuz kama mto mdogo wa kijijini ambao 30% ya maji tunapata hapo. Maji haya ndio kiungo muhimu katika shughuri za kila siku za kijiji chetu. Sasa, kuna bwana anyekaa huko kwenye chanzo cha mto aliweka bayana kabisa kuwa ataufunga mto kama Wachokonozi wake wataendelea kumchokonoa. Jirani huyu ni Iran ambaye tayari wahasimu wake Wamemchokonoa jana.
Bunge la Irani liliketi kuidhinisha kufungwa kwa straight ya Hormuz, kitu kinachoweza kuwa kigumu kutekelezeka lakini washirika wake wanavisrani na wanaweza kufanya hali isiwe shwali kabisa huko kwenye chanzo cha maji, hasa washirika wake kama Hezbollah watajaribu kuufunga mto huo. Wengi wanaweza kujiuliza kuwa Sisi Kiu tutaipata wapi wakati huu ugomvi hatuhusu?….
Ni wazi kuwa Tanzania, ni wanakijiji tunaoishi chini ya mto, hekaheka zozote kwenye chanzo lazima zitukoseshe usingizi. Kama unaweza kulala vizuri ukadhani mambo yako sawa, unapaswa kujitafakari.
Wachambuzi wa masoko ukipenda Wazee wa mahesabu, wanasema kama mto ukifungwa kabisa kwa wiki kadhaa, bei ya mafuta inaweza kupanda kati ya 103% hadi 373%. Hiyo ni kama lita moja ya mafuta, ambayo sasa ni Tsh 3,200, ikapanda hadi Tsh 6,400–15,000! Hapa ‘Hamza Kanuni’ lazima wataongezeka 😂😂 Na mapambano kwenye Daladala yatakuwa zaidi ya pale Sinza 😂.
Hata kama mto ukifungwa nusu tu, bei itapanda 7–22%, yaani Tsh 3,400–3,900 kwa lita. Shida inaweza kuletwa na makampuni ya bima, kama watondoa bima au watatoza gharama za ziada kwa meli zitakazo pita Hormuz ili kufidia au kukwepa harasara zinazoweza kuzuilikakutokana na hatari iliyopo, hivyo kufanya bei ya mafuta iwe iwe kichomi kwa wanakijiji wanaoishi chini ya mto.
Iran inaweza kufanya mashambulizi ya makombola na drones, hivyo kufanya maji yasinyweke kabisa. Aliyetuleta huku na huyu mzee wakijiji (Marekani) baada ya kutimia Gobore kwenye ugomvi wa fimbo. Njia pekee tunaweza kunusurika ni kama mzee wa kijiji atalinda mto kwa mslahi ya kijiji ili maji yaendelee kutiririka la sivyo Tutakufa ni Kiu.
Kufunga mto kabisa ni ngumu, lakini hata mgogoro mdogo kwenye mto, lazima utatibua maji na kuleta uhaba wa maji, Tunaokaa chini ya mto tunaweza kuanza kunywa maji machafu tena kwa bei ya juu, huku tukisubiri mvua ya miujiza (nishati mbadala) ambayo hatujawahi kuipanda.
Figures Sources
Euronews
Reuters
TheGuardian