Tatizo humu JF ulikokuja kuomba ushauri kumejaa Vijana lojolojo wa Dar, na wao wanaogopa nyoka.
Nakumbuka nikiwa na miaka 14 nikiwa Kwa Bibi kijijin huko Ndani ndani Bariadi siku Moja tukawa tunasikia Mbuzi analia Sanaa meeee meeeee meeeee
Mida hiyo Asubuh nilikuwepo Mimi na Mtoto mwenzangu tulikua tunaringana umri.
Aisee tukakimbilia kunakotoka sauti, kufika huyo Chatu, walalalala wosashashaa chatu huyo .
Sijui hata ilikuaje, nilijikuta nimemkamata shingo yule chatu ,huku namuambia mwenzangu ampige Kwa mpini ulikua pemben.
Yule Chatu akamuachia Mbuzi, Dogo akaendelea kutia kipondo tuu, Tulimuaa!!.