Vitoto vya nyoka nyumbani kwangu

Vitoto vya nyoka nyumbani kwangu

Nyoka gani sasa huyo.Mnyoo huyo.
 
Huyo pichani ndo mwamba alofanya nilale bila kuoga,nisipate usingizi nibane haja ndogo kwa zaidi ya masaa manne.
Nyoka hagongi mtu Ila mtu ndio anagonga nyoka, sumu ya nyoka ni kwa ajili ya kuwindia kuua mawindo yake km panya sumu ya nyoka sio kwa ajili ya kupambana na adui mwingine Ila inapotokea kujihami basi uitumia sumu yake kumvamia adui, mara zote nyoka hukimbia kukwepa hatari iliyopo mbele yake na pia wapo baadhi ya nyoka hukuvamia kuendana na joto na mapigo yako ya moyo yanavyopanda unamtisha Ila ukirelax nyoka hana shida na wewe hujawahi ona mtoto anacheza na nyoka na hamdhuru hata kidogo ?
 
Yes I like to brag about my twins but english medium is nothing to brag about
Watu wengine si lazima uwajibu, Soma waache km walivyo uzuri story yako imeeleweka next time unajua una mwanaume hata ukivamiwa na Simba utamwita aje kuku-defend
 
Nyoka gani sasa huyo.Mnyoo huyo.
Nyoka wa chooni hao inaonekana anapoishi Kuna kamsitu pembeni ambapo ndio makazi ya kila nyoka especially weusi na wa kijani
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Alichokiona mtoa mada ni (Minyoo aina ya Earth Worms) na sio vitoto vya Nyoka... nyoka hutafuta sehemu ambazo zipo very comfortable kutaga na kutotoa watoto.. + urahisi wa kuwalisha.. mara nyingi huwa porini..
Mimi hiyo hali ilinitokea karibu mara tano naua vitu kama watoto wa nyoka... nikaanza kuhisi ninaishi na nyoka/ Ushirikina... kuna kijana alikua anachukua mchepuo wa sayansi.. PCB mdogo wangu ninakaa nae.. nilikua nimekiuA kimoja nikampa na yeye aone.. wakati nalalamika sana kuwa kuna nyoka wanatotoa vitoto bafuni kila mara..tulipovichinguza... akaja kubaini ni hao Earth worms.... minyoo... ambao wanasaidia kurutubisha udongo.. kwa watu waliosomea udongo na kilimo.. ukimuua huyo mnyoo wanaweza kutoa machozi.. kwa sababu wanajua umuhimu wake...
 
Mimi nikuoe niwe naua vinyoka tu basi. Okay chakufanya mwaga oil chafu au diesel Kila eneo Kwa masaa 36 watahama wenyewe. Sio umwage kama maji, unamwaga kwakuchora mistari mistari.

Vile vile nyoka huwa wanatembea wawili wawili, ukimuua mkubwa ndani ya kipindi Fulani atakuja mwingine kumtafuta mwenzake. Nyoka mdogo wa mwanzo mlimtupaje? Ilitakiwa aburuzwe kuzunguka nyumba na kuelekea eneo la pori na kumzika huko Ili akija mwenzake atazunguka na mwisho ataishia porini huko.

Hako katoto nistue kesho
Hii kweli mkuu Kuna siku mwenye nyumba alinita baada ya kukuta nyoka koridoni nyuma ya mlango mida ya 11 jioni nikamuua freshi tu kiroho Safi na tukaenda kutupa mbali ajabu night tumelala mida ya sa5 naona mwenye nyumba ananiamsha tena eneo lilelile Kuna nyoka mwingnine na ukubwa uleule niliua tena lkn ckulala kwa amani cku hyo
 
Anaishi juu ya Dari pia?
 
Shirki hii Mkuu 😂😂
 
Hii kweli mkuu Kuna siku mwenye nyumba alinita baada ya kukuta nyoka koridoni nyuma ya mlango mida ya 11 jioni nikamuua freshi tu kiroho Safi na tukaenda kutupa mbali ajabu night tumelala mida ya sa5 naona mwenye nyumba ananiamsha tena eneo lilelile Kuna nyoka mwingnine na ukubwa uleule niliua tena lkn ckulala kwa amani cku hyo
Wanyama hasa nyoka hata ukipita mwezi yaani atamtafuta mwenzake Kwa kupita njia Ile Ile hivyo ukiua mmoja unatakiwa kuharibu parten ya njia Kwa kumzungusha mfu hovyo hovyo na kumwelekeza porini.
Mwanzo watu walikua wanahisi nyoka anafufuka kumbe ni mwingine anaemtafuta mwenzake. Ukiua wawili basi endelea kuishi Kwa Amani.
 
Hello people.
Naandika hapa nikiwa natetemeka jamani niko ndani ya neti naogopa kushusha miguu chini na nimebanwa na haja lakini naogopa kwenda chooni.😭

Ni hivi,nilikua naenda kuoga bafuni ile kuwasha taa nikaona kitoto cha nyoka cheusi kinatembea kwenye maungio ya tiles.

Nilivyokiona tu kile kinyoka akili ikanambia mama yake hayuko mbali.Nikajikuta natengeneza picha ya mama yake na kwa jinsi ninavyoogopa nyoka nikajikuta napiga yowe moja kali nikageuka fasta kurud chumban na ku dive kitandani na kuchomekea neti.Moyo unadunda nataman kulia na sitapata usingizi leo.

Two weeks ago niliona tena kitoto cha nyoka kama hichi cha leo ila kilikua kimekufa na kwa vile mazingira yalisafishwa na kilikua kimekufa sikujali.

Hichi cha leo kimenitia presha sikuwahi kuwaza nitaona nyoka ndani ya nyumba yangu.Yesu nitetee mimi jamani😭.

Nahisi tu kuna wazazi wao somewhere nyumban kwangu wanazaliana tu jamani😭.Sijui wako mvunguni,sijui wako chini ya bathtub,sijui wako kabatin,sijui wako kwenye moja ya mapoch yangu.

Sitakua tena na amani na hii nyumba,ingekua ugenin kesho ningeaga ila hapa ni kwangu na mbaya nyumba ni kubwa na kila room imejaa vitu.Hata nikitafute mtu anisaidie kuwatafuta awaue ataanzia wapi aishie wapi?

Mlinzi kaja dirishan anauliza madam vp mbona mayowe?Namwambia kuna nyoka bafuni kwangu.Anauliza mkubwa kias gani?Namwambia ni kitoto kama kile tulichoona kimekufa siku ile.Baada ya kumjibu hivyo namsikia anafyonza huko nje then anawasha kiredio chake anaondoka.Namwambia sasa unanisaidiaje?Anasema huyo ni kama mjusi tu we lala then namsikia mwenzie anacheka hlf anamwambia mwambie ni kama mnyoo au hujui kuna siku huyo alishavunja mguu kwa kuogopa mjusi.?

Anyways.Wakuu naomba mnisaidie mawazo ya nini kifanyike kuhakikisha hawa viumbe kama wanaishi humu ndani wanatoka na kufa kabisa.

Hivi hakuna dawa ya ku spray nipulize nyumba nzima kama wapo wafe?

Pia naomba kujuzwa,hivi ukiona vitoto si ni ishara kuwa wazazi wao wapo around eeh?

UPDATE: Vitoto vya nyoka nyumbani kwangu

Mlinzi wako anakusonya?
 
Nimechekeshwa na huyo mlinzi wako aliyefyonnya na kuwasha kiredio chake.
 
Nunua Rungu zile spray, ukipulizia akiwa mkubwa au mdogo ukiwapulizia tu wanaishiwa nguvu then wanakufa.
 
Back
Top Bottom