7. VITU VINAVYOFANANA/ VITU VYA AINA MOJA.
Jiepushe na kununua vitu vinavyofanana au vitu vya aina moja. Mfano. Unanunua simu mbili za iPhone, au unanunua jezi mbili za Simba/ Yanga. Hayo ni matumizi mabaya ya hela.
8. USIDANGANYWE KUWEKA HELA YAKO KWENYE SIASA KAMA HUJAWAHI KUWA MWANASIASA.
Huu sio wakati wa kujifunza siasa na kuweka hela zako kwenye vyama za siasa. Wanaokushawishi ugombee wanataka tu kukulia pesa yako, ukianguka wakucheke.
9. USINUNUE NYUMBA KWASABABU NI NYUMBA, JIULIZE ITARUDISHA HIYO HELA BAADA YA MUDA GANI?
Biashara ya majengo (Real Estate) unaweza kufanya popote. Lakini kumbuka thamani ya ardhi imetofautiana kati ya eneo moja hadi nyingine, sababu ikiwa ni vigezo mbalimbali, miundombinu, usalama, neighbourhood na utamaduni wa eneo husika.
Ni ngumu kupata nyumba ya AIRBNB Vingunguti Kiembembuzi
1O. ACHA TABIA YA KUNUNULIA WATU POMBE.
Umeingia bar, kila mtu unamwagizia anachokunywa. Tabia ya kujenga heshima bar imekwisha pitwa na wakati. Hela zako tumia vizuri, saidia wahitaji waliopo kwenye jamii inayokuzunguka.
11. DALADALA, BAJAJ NA BODABODA NI BIASHARA PASUA KICHWA.
Hata kama watu wako wa karibu wamekushawishi ufanye biashara hii, jiulize mara mbili, je utaweza kukimbizana na watu wenye akili kumi? Avute bangi, anywe gambe, agonge mademu, aweke akiba na ale hapohapo .
Bora ununue trekta, biashara unaongea mwenyewe, dereva unampa posho tu na mafuta.
Enzi za ujana iliitwa FOMO, Fear Of Missing Out. Hii ilikuwa hofu ya kuonekana umeachwa nyuma na fasheni. Muda umeenda sasa, acha kuangalia wenzako watakuonajr,nunua kutokana na mahitaji yako.
14. EPUKA KUWATEMBELEA WATOTO WAKO NA KUKAA KWAO KWA MUDA WA SIKU NYINGI.
Ndio ni wanao, watembelee kaa siku mbili rudi kwako. Sio unaenda kwa watoto wako halafu unahamia huko..
Waswahili wanasema hata tamu hukinai. Na pia mwanasanaa mzuri ni yule anayetoka jukwaani wakati mashabiki wa sanaa yake wanaihitaji zaidi.
15 JIEPUSHE NA VISERENGETI BOY/ VIBENTEN.
VivuIana Vidogo havina na haviwezi kuwa na mapenzi ya dhati na mijishangazi, vinafuata tu utelezi na Hela. Akiona humpi anaweza hata kukuletea majambazi ndani.
16. ACHA KUNUNUA VITU UKIWA BAR
Zimepita sufuri umenunua, imekuja pasi unanunua. Kumbuka, ubora ni jambo la muhimu kuzingatia kabla hujanumua kitu.
Hii itakusaidia kuifanya nyumba yako kutokuwa na makorokoocho mengi yasiyo na kazi wala yasiyo na matumizi.
Sasa umri wako umeenda, acha kununua marundo ya vipodozi. Kuwa na vipodozi vyako vichache tu, vitakavyokufanya uonekane nadhifu na simply natural beauty