Vitu 15+ unavyotakiwa kuacha kununua unapotimiza miaka 50

19. ACHA KUNUNUA MAGARI MAKUUKUU AMBAYO YATAKUMALIZIA HELA, MUDA NA FURAHA YAKO.
Magari makuu kuu na machakavu.a.k.a spana mkononi hayakufahi kwa muda huu. Magari haya yanapoteza muda mwingi garage na yanamaliza pesa na furaha yako.
 
20. JIEPUSHE NA KUNUNUA VIATU VYENYE SOLI NDEFU

Mifupa imekomaa, nyama za mwilini zimeanza kulegea na uzuri wa mwilini unakupa mkono wa kwaheri.

Ukiteguka ama kuvunjika katika umri huu, mifupa haiungi kwa urahisi. Viatu virefu vinakuweka kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kuanguka
 
Na mimi babu nisipite bila kuacha neno,
"Penda kujipa furaha kula kwa kiasi, punguza kula nyama zidisha matunda, maziwa, lewa pombe kila weekend, acha kunywa bia mbili za kila siku mfululizo hizi ndizo zinazotuua wajukuu zangu. 49yrs old kipisi cha mtu."
 

Waswahili wanasema uzee ni jalala....

Uzee ni jungu kuu...

Ila jungu kuu halikosi ukoko....

Nashukuru mengi ya aliyoandika mleta uzi nilianza kuyafanyia kazi nikiwa na miaka 38 huko, kuja kufika 50 haikunipa shida niliona ni maisha yaleyale, hakuna jipya.

Ila uzee ni kama balehe...

Kuna wanaowahi, kuna wanaochelewa..

Kuna wanaopata changamoto flani flani wakiingia uzee...
Kuna wanao ona kawaida tuu kama anaenda dukani na kurudi.

Kikubwa omba uzee ukukute na afya njema na uwe unajiweza na kujimudu kihali na mali.

Bi Kasinde πŸ˜‰.
 
Unadate na Shimba ya Buyenze mkuu πŸ€”
 
Uzuri wa fake ids.Wengine watajiweka kundi la vijana wadogo.Wengine watajiweka umri wa kati katikati.Na wale palee,watajijumuisha uzeeni.Yote kheri.
NB:Siku angalau moja tu,tuweke ids zetu wazi ili tugundue masufuria ya plastiki.A mere joke!πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Wazee tupendane, tuachane na ben10 hawa wanatunyonya tu uchumi wetu na wapenda dezo! πŸ˜‚
Wazee tujilinde tuvae vizuri, shughuli zote za kuumiza vichwa tupa mbali, kama unakinanda piga imba nyimbo nzuri upendazo huku ukiwa na juice yako fresh!
Hata hivyo at 50 huwa sio mzee japo tunajaa woga! Maana wapo wenye 65+na wako vizuri sana kuliko hata mwenye 35+,kimwonekano na kiafya.
 
Tamko jema sana hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…