geek01
Senior Member
- Jul 11, 2017
- 143
- 267
kama great thinker nimebuni iv apa dsm mayai najumua 7000 kila trei af nauza 9000 mana saiv DSM mayai yamepanda kidogo alaf napita katika vijiwe vya chipsi mbalimbali vingine ambavyo vipo mbali na masoko kabisa naingia ob na watu nakua nakupa trei mbili au moja alaf nakuja kuchukua pesa baada ya siku mbili nakua napata faida ya 2000 mara 40 ndan ya siku mbili inakua 80000 na mtaj wa trei 40 ni 280000 kwa mwez ni 1200000 ndan ya mwaka ni milionaire....na usafiri kuna mchiz ananiuzia lipikipik
Sent using Jamii Forums mobile app
Sikuvunji moyo ila umeongea kirahisi sana, umeassume kama hamna changamoto yoyote katika hizo siku mbili upate hiyo 80,000.
1) Hiyo pikipiki unauziwa bei gani? Maan hujaweka kwenye mtaji ina maana hii biznez ni nzuri kwa mtu mwenye pikipiki tayari. Na kama ni kukodi Kwa kawaida hesabu za pikipiki ni kurudisha elf 8 hadi 10 kwa boss kwa siku, hujaweka hii.
2) Hayo mayai ya 7000 kwa trey unapata wapi kila siku? Believe me kuna kipindi mayai yanaisha kwa supplier wako na inabidi utafute sehemu nyingine na bei inakuwa tofauti, ukipata kwa lets say 8000 kwa trey kwa siku mbili au tatu ujue ni faida nusu tayari.
3) Hakuna kitu kibaya kama kumuachia muuza chips hela kwa siku mbili, kibanda cha chips faida yake ni ndogo na boss anachukua almost kila siku hivyo kurudi baada ya siku mbili na kudai hela ya juzi mtaanza kutafutana lawana. Ukipigwa kalendar hata siku moja tu deni linakuwa kubwa na inazidi kuwa ngumu kulipa, ushauri hapa ni kupita kila siku kesho yake kuchukua hela ya jana. Na je what if hayakuisha atakuwa tayari kulipa yote na kuchukua tena mzigo? Wewe unasema 80,000 faida siku mbili..[emoji58]
4) Umesema unategemea kuzungusha kama trey 40 kwa siku hizo mbili ili upate faida ya hiyo 80,000. Na pikipiki yako unazungukaje na trey 20 za mayai? Au utakuwa unaenda na kurudi kila saa, hivyo vibanda havipo mtaa mmoja hivyo utakuwa unapeleka vipi hizo trey 40 zote kwa hizo siku mbili kwa pikipiki? Kama unabeba kidogokidogo je vipi kuhusu mafuta(petrol).
5) .......
-Wengi tunakimbiliaga tu kwenye faida(sijui milion ngapi kwa mwezi) na tunasahau changamoto zake, ukianza biashara baada ya week mbili tu unaacha na unakuwa umepoteza muda na hela. Tuache ndoto za kina forever living kuwa ukialika tu watu watano na hao wakaalika wengine basi unakuwa milionea. Nijibu kwa hoja hizo changamoto hapo juu ili tusaidiane kujikwamua.
Big up sana kwa hii idea nzuri !