Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Uko sahihi sana mkuu mimi ni mfugaji wa kuku chotara nauza mayai ya kuroiler.Pia kwasababu ya uhitaji wa mayai ya kisasa huwa nanunua kwa jumla trei 100 then nawauzia watu wa chips.Soko kubwa la mayai ni wauza CHIPS.

Na hao wadau wanaangalia vitu vitatu nitavipanga kulingana na umuhimu wake.

1.Bei
2.Size
3.Kiini cha njano

Sasa mayai ya chotara au kienyeji hayawezi kukidhi hivyo vigezo kwanza yanauzwa bei juu pili ni madogo kwa size kigezo cha tatu walau yanakidhi kuwa na kiini cha njano. Huwezi mueleza mtu wa chips Habari za mayai kuwa yana mbegu bla bla hizo hazina maana.
Mkuu hao kuloiler chakula unanunua au unatengeneza mwenyewe?
Maana nilikua na sasso wanataga sijui ata nmewakosea nini wamepunguza kabisa kutaga!
 
Natengeneza mwenyewe natumia formula za layers nilinunua k....poultry Farm moja ya shamba kubwa Shinyanga ni nzuri ila ni gharama maana imezingatia kanuni bora za chakula.

Yaani Metabolic energy, Crude protein,fiber.....lazima ziwe katika kiwango husika so pia nina excel sheet ninayoitumia ku balance chakula in case nikikosa ingredients moja wapo sokoni au bei ikiwa juu sana natafuta mbadala

Hiyo crude protein si mpaka upime? Unapimia wapi?
Na kwenye huo mchanganyiko vipi mashudu haya alizeti? Maana kuna mtu umeniambia tatizo mashudu
 
Hiyo crude protein si mpaka upime? Unapimia wapi?
Na kwenye huo mchanganyiko vipi mashudu haya alizeti? Maana kuna mtu umeniambia tatizo mashudu
Kuna namna fulani ya kukokotoa kujua kiwango cha crude protein yaani unakokotoa kwenye excel then unapima maabara.

Mashudu sio tatizo mkuu muhimu uweke kiwango kinachotakiwa.
 
Kuna namna fulani ya kukokotoa kujua kiwango cha crude protein yaani unakokotoa kwenye excel then unapima maabara.

Mashudu sio tatizo mkuu muhimu uweke kiwango kinachotakiwa.
Shukran mkuu
 
Feed formulation tunazitengeneza kwa kukokotoa kwenye kikokotoo then ndo inaenda kupimwa maabara maana formula inaweza kuwa nzuri ila isifanye vizuri katika utendaji.
 
Mkuu sikuwa karibu na docs za chakula....

Kuhusu suala la mashudu kwa formula ninayotumia naweka 90kg kwenye tani.

Changamoto ambayo wafugaji wengi wamekuwa wakihusisha mashudu na kuku kutotaga ni KUNENEPA. Hii ni sahihi kuna uzito ukizidi kuku hatagi hata ukipungua kuku hatagi pia....lakini tatizo la uzito sio mashudu ni chakula kwa ujumla yawezekana chakula chako umezidisha virutubisho.

Tena kwa sasso angalia uzito ikiwa wamenenepa sana hawataga.Pia sasso ni kuku ambaye anajenga nyama kwa haraka sana hivyo ni rahisi kuwa over weight
 
Wadau nivitu gan vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa muongozo wadau,Asanteni
 
- bei unayonunulia
- bei unayouzia
- soko la hayo mayai yako
- sehemu utakayouzia
- namna ambavyo utawafikia au wateja watakavyokufikia
- namna nzuri ya utunzaji hayo mayai ili yasiharibike au kuvunjika
- Nani atasimamia na kuuza Biashara yako
- ubunifu na mikakati ya kiushindani utakayokuwa nayo kuweza kuwafanya wateja waje kununua kwako na wasiende kwa wengine
- namna unavyojitangaza na kutunza brand yako
 
Back
Top Bottom