Kama unafanya biashara,naamini hakuna kitu unachokipenda kama mauzo na wateja.
Kama unafanya biashara na hutamani kupata wateja zaidi au mauzo zaidi,unaweza ishia hapa kusoma.
But kama tunaendelea pamoja,hongera sana.
Leo utaenda kujifunza ni vitu gani vitakusaidia kutimiza lengo lako la kupata wateja zaidi na mauzo zaidi.
Biashara kama biashara ina mambo mengi,inahitaji uwekezaji wa kutosha (muda na pesa zako) ili iweze kusimama na kuleta mafanikio.
Sometimes unaweza ukakosa direction,ni wapi uwekeze nguvu zako,resources zako ili ziweze kuleta mafanikio.
Leo nakupatia vitu hivi 3,
No matter what,ukiwekeza katika vitu hivi lazima utaona impact yake ktk biashara.
Tena utaona matokeo mazuri,kama ukiwekeza ktk vyote 3 na sio kimoja kimoja Kama wengi wanavyofanya.
Twende pamoja
1. BRANDING
Yes,tunaanzia hapa hapa ambapo waswahili wanaelewa vizuri,wao wanaita kuji-brand.
Swali la kujiuliza hapa ni moja
Je,Wateja wako (au watu wanaoweza kuwa wateja wako )wanaichukuliaje biashara yako??
Jibu utakalolipata ndio BRAND YAKO.
Je, umeridhika na namna wanavyokuona na kukuchukulia (online na offline?)
Vipi ungependa kubadilisha muonekano wa biashara yako,na jinsi wanavyokuchukulia??
Hiyo sasa ndo tunaita Branding.
Unashape namna ambavyo wateja wako wanatakiwa wakuchukulie, KWA MFANO
-Kuanzia muonekano wa account yako ya insta,Design ya posts zako,Matangazo yako...mpaka Duka lako linavyoonekana,customer service,delivery nk.
- Asikwambie mtu, BRAND na BRANDING zina nguvu Sana, within seconds mtu anaweza kukuchukulia poa au akakuweka matawi ya juu.
Ndio maana watu wengi leo wanawekeza ktk kudesign na kubrand frames zao mfano mzuri Maduka ya Iphone Makumbusho na Frames za Sinza.
HOWEVER,
Branding haiishii nje ktk frames tu,inaenda mpaka online na kiufupi inagusa mchakato mzima wa biashara yako.
Invest here
#More lessons za brand and Branding zitakuepo,stay tuned
2. MARKETING
Kama unafanya biashara,Bila shaka umewahi kuskia neno hili mara nyingi "Marketing"
Je, ushawahi kulizingatia ktk biashara yako?
Marketing ina definitions nyingi sana, lakini hapa hatupo shule,kudefine na kupata marks.
Lengo ni kujifunza na kuapply kile tulichojifunza ktk biashara ili uweze kupata impact yake.
Naweza kusema kwa ufupi,marketing inahusisha shughuli zote unazofanya ili kuweza kutambua mahitaji na wateja (needs) na kuweza kuwahudumia (satisfying them).
Wengi wakiskia marketing,wanawaza matangazo tu,hapana.
Matangazo ni sehemu tu ya marketing,
That's's why unapoweka marketing budget (for companies example)...lazima uiassign ktk vitu vingi mbali na matangazo tu.
Kuna aina nyingi za marketing mfano Digital Marketing, Content Marketing,Social Media Marketing,E-mail Marketing,Influencer Marketing nk
Hopefully tutajifunza na hizo pia,stay tuned kwa siku zijazo
Invest in your marketing
3. ADVERTISING
Japokuwa ni part ya marketing,nimeiweka katika section yake kwa sababu maalum.
Advertising/Matangazo ni kitu ambacho wafanyabiashara wengi wanakifahamu kwamba kina potential ya kuwaletea wateja wengi
Lakini wanaowekeza ktk matangazo ni wachache, kwanini?
Kwa sababu either wanakosa taarifa sahihi au msaada kuhusu namna matangazo yanavyofanya kazi,hivyo wanaona kama watapoteza fedha zao.
Wengine labda ni ubize wa kuendesha biashara,Uoga wa kuanza matangazo na mara chache sana kukosa funds??
($1 kwa siku?? Kweli)
Anyway,Long story short...kama ambavyo ili kitu chochote kifanikiwe kinaitaji maandaliz na mipango madhubuti.
Ukitaka kufanikiwa ktk matangazo unahitaji strategy nzuri pamoja na maandalizi mazuri.....Kabla hujaweka hata senti tano yako kulipia matangazo.
Na hapa naongelea matangazo yote, Kuanzia TVCs, Radio, Vipeperushi mpaka kwenye matangazo ya online (sponsored ads).
Kama unahitaji ushauri na msaada ktk kutengeneza au kuendesha matangazo,usisite kuwasiliana nasi.
(USHAURI NI BURE).
And Yes,usisahau kauli hii "BIASHARA NI MATANGAZO"
Conclusion
Leo tunaishia hapa,
Running a business tough ,running a successful business is even tougher.
Vutia wateja zaidi na itangaze biashara yako izidi kujulikana kwa kuwekeza vizuri ktk vitu hivyo 3.
Na ukiona unakwama sehemu,usisite kutafuta msaada.
Tukutane kesho kwa next lesson.
Cc:NYUMBANI DIGITAL AGENCY
We help to Market,Advertise and Brand Your Business
Text/Call/WhatsApp 0752226475
Join our FREE TRAINING WhatsApp Group
Send "ADD ME" to 0752226475