Vitu vinatukwamisha Taifa kusonga mbele, bali yakipungua mambo haya Tanzania ingekuwa tupo mbali mno

Uingereza hawazungumzii Man U, Liverpool, Newcastle, Aston Villa tangu asubuhi mpaka jioni.
Nimeishi huko.

Mwaka huu most watched TV programme on TV semi final England v Netherlands (watched by 20.4 million people).


Siku ya uchaguzi wao accumulation ya TV zote watu waliokuwa wanaangalia ni 7.3 million. Na Election debate ilikuwa na 3.2 million views


Uchaguzi ulioisha ni nusu tu ya watu wenye sifa ya kupiga kura ndio waliojitokeza.


Match of the day ambayo inaonyeshwa jumamosi usiku (saa nne) muda ambao vijana na watu wengi wanaenda night out inaangaliwa na 4 million people kila week kwa hao waliopo nyumbani tu.

Nenda kutafute talksports radio siku nzima mpira (ukitaka kucheka itafute leo baada ya premiership games, usikie povu la mashabiki hasa wa team zitakazo fungwa). Au ingia kwenye social media zao uone mapovu huko hasa leo jioni.

Ushabiki wa mpira uingereza ni balaa watu ninao wajua mimi mida hii wanajipanga kuelekea pubs na hao wabongo tu.
 
Hajui kitu huyo analopoka tu
 
KWa hiyo unaona hisani sio ? Kujengewa barabara ujinga ni mzigo
 
Shukuru kuna Yanga na Simba watu wanapata outlet ya kutoa stress zao ama sivyo sasa hivi hapo ulipo huenda ungehitaji kuwa na panga au silaha ili wananchi wasichukue chochote ulichonacho...

Acha kabisa mkuu kinacholeta shida nchi hii ni siasa chafu na uongozi mbaya (ingawa hivyo pia sio hatari kama corruption na watu kwenye nafasi kutumikia matumbo yao)..., Pesa zinazokusanywa zingeweza kufanya mambo maradufu bila kutembeza bakuli wala mikopo...
 
Ili uweze kupiga hatua ujanja ni kufanya kazi kwa bidii, haya mengine ni siasa za kimaskini, hayana ukweli wowote.
 
Umaskini wetu ni uvivu wetu hivi vingine ni visingizio tu.

Simba na Yanga unaweza kuzilinganisha na Al Ahly, Pyramids au Zamalek?

Unaweza kuzilinganisha na Esperance, Wydad Casablanca na Raja Casablanca?,

Mbona Misri na Morocco hawazilalamikii timu zao ambazo ni kubwa kuliko hizi mbili za kariakoo?.

Tuache kuwa na mawazo ya kipuuzi, hayatusaidii chochote.

Kiswahili ndio kimerahisisha hata uwepo wa umoja na amani vitu ambavyo mataifa mengine ya afrika hawana.
 
Umaskini wetu ni uvivu wetu hivi vingine ni visingizio tu.
Uvivu wa Nani ?
  • Hivi unaweza kumuita mkulima ni mvivu wakati amelima na serikali ndio imeshindwa kutafuta masoko ?
  • Hivi unaweza kumuita mtu aliyehitimu utabibu aliyepo mataani eti hana kazi wakati tunahitahi watabibu (hawatoshi) na tumetumia gharama za kutosha kuwasomesha ?
  • Hivi unaweza kumuita msanii ni mvivu wakati anakesha kila siku kutunga nyimbo zinazopendwa na UMMA lakini anaishia kushindwa kupata ujira wowote kutokana na kwamba watu hawana buying power kutokana na kwamba watumishi tuliowapa kazi ya kutunga sera wameshindwa kazi ?
 
Yanga na simba wala hawahusiki, huwezi zuia mtu kufuata burudani kisha kushabikia vyaĺma vya siasa au wanasia wasio na misimimamo na hawajui nini hasa taifa linataka au watanzania wanataka. Upinzani ukiwa imara na ukaeleweka automatically mabadiliko yatatokea ndio 2015 uchaguzi ulikuwa na mvuto kutokana na upinzani ulikuwa imara ila baada ya kupelekwa puta na kazi safi za JPM wakaanza kupoteza uelekeo. Hivi unawezaje kumuamini mpinzani ambaye familia yake ipo Ulaya are we serious? Mpinzani ambaye akipata shutba kidogo anakimbia uhamishoni are serious ukombozi ndio unatafutwa hivyo? Wakina Mandela wangekimbia nchi zao zingepata uhuru. Kati ya wapinzani wote angalau Mbowe na Mwabukusi wanachembe ya uzalendo wengine wapo kwa maslahi yao binafsi.
 
H
 
Mpira wetu bado haujakua, kuna muda utafika huko mikoani kutakuwa na shule za kukuzia vipaji kila mkoa, sijui mlalamikaji atasema nini ukifika wakati huo?.

Hawa Yanga na Simba bado hawajutumia vizuri mashabiki wao kama mtaji wao wa uhakika, wanaweza kuwa matajiri kuliko walipo hivi sasa, je tutasemaje wakishafikia viwango vya kina Mamelodi kwa utajiri.

Tuchape kazi kwa bidii, kwa kuwa wabunifu, pia tusisahau kuupitia upya mfumo wa elimu.

Mchina anakwenda kuishi sehemu yoyote duniani na kile anachokizalisha kwenye soko la nchi hiyo kinamuwezesha kuishi vyema, elimu zao zimejaa ubunifu zinafungua kichwa cha mtoto mpaka akiwa mtu mzima hapati taabu maishani.
 
Shida ya huyo uliyemjibu yuko na narrow view ya namna uchumi unvyojengwa! Hafahamu ushiriki wa watu katika maendeleo.
 
Kwenye maofisi,mashule,vyuo na vijiwe nchini Uingereza hawana ujuha wa kuongelea mpira wa miguu tangu asubuhi mpaka jioni/usiku.

Kuangalia TV programu ya saa mbili haiwezi halalisha kuwq wanatumia muda mwingi kwenye kujadili mpira wa miguu.
 
Ni wapi hapa Tanzania watu huzungumza mpira asubuhi hadi jioni?
Mimi ni mfanyaji wa kilimo na biashara ya korosho na ufuta huko Kusini, (Kuanzia Mkuranga, Rufiji mpaka Newala).

Yaani unasimamia mavuno au manunuzi,unasikia tangu asubuhi watu wanaongela mpira wa miguu mpaka jua linazama.
 
Mimi ni mfanyaji wa kilimo na biashara ya korosho na ufuta huko Kusini, (Kuanzia Mkuranga, Rufiji mpaka Newala).

Yaani unasimamia mavuno au manunuzi,unasikia tangu asubuhi watu wanaongela mpira wa miguu mpaka jua linazama.
Hayo mazao unayonunua anakua amewalimia nani?

Hivi kwanini mnatamani kila mtu awaze mnavyowaza nyinyi?

Mtu akizungumza mpira huku anafanya shughuli zake, tatizo linakua wapi?
 
UCHAWA NI NAMBA MOJA, UTAKUTA WAGANGA WAKUU, MAAFISA ELIMU WA WILAYA NA MIKOA NI MACHAWA HASWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…