residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Akhsante sana, umekuja nilipokuwa napataka kwa swali hili la "Mtu akizungumza mpira huku anafanya shughuli zake, tatizo linakua wapi?".Hayo mazao unayonunua anakua amewalimia nani?
Hivi kwanini mnatamani kila mtu awaze mnavyowaza nyinyi?
Mtu akizungumza mpira huku anafanya shughuli zake, tatizo linakua wapi?
Jibu lake ni kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa taratibu za kazi yangu, nimepanga muda wa kukamilika kuwa saa nne.
Wao wanapokuwa wanabishana kuhusu mpira wa miguu, kwa kuongea huku umesimama na kuchezesha mikono, miguu na kichwa, maana yake muda wa kuimaliza ile kazi ya saa nne utaongezeka kwani muda mwingine utapotea kwa kutumia mikono, miguu na kichwa kuonyesha kwa vitendo namna mpira ulivyokuwa au ulivyo.
Ninalazimika kufukuza watu wengi kila leo na kunilazimu kuleta watu toka mbali na hapo ninapofanyia shughuli zangu kitu kinachopelekea kuwalipa kiwango cha chini kinachopelekea ile "multiplier effects" na "money circulation" kuwa ndogo.
Msimu ujao wa ununuzi korosho nina mpango wa kutembea na "hidden camera" inayorekodi live kila tukio na muda wake linapotokea.