Vitu vingine vinafikirisha sana

Vitu vingine vinafikirisha sana

Sawa Mkuu maisha ya kisiwani yanaemdeshwa na ushirikina hivyo unabidi kujizatiti
Kwani hapi kulikuwa na ushirikina ndo maana nikapewa hiyo mbinu? Mi lilijua ni ugonjwa tu na tiba yake ni hiyo. Kwkigupi nilichukulia kuwa ni ugonjwa wa huku na dawa ndo hiyo.
 
ee mkuu m ni wa kagera
Basi sawa ila sisi huku visiwani tunayaita tu mwalilo ndo jina linalijulikana huku. Mi niko pale rwamishenye mtaa unaitwa migera. Nimepanga huko unavuka tu shule ya rwamishasha daraja la chuma unafika ninapoishi kwa sasa
 
Utotoni niliwahi kutokewa na kiupele kwenye paji la uso kadri siku zinavokwenda kikazidi kukua, nikapelekwa hospitali wakanipa dawa za kumeza na sindano ila bado hakikukauka. Nakumbuka kuna siku nimeagizwa jembe kwa bibi flani alikuwa jirani yetu alivoniona akaniuliza ulikuwaje usoni nikamuelezea na namna kiupele kilivoshindwa kupona. Alichoomba ni mama aninulie sindano ya kushona nguo tumpelekee yule bibi tukakuta ametafuta matunda pori flani yanakuwa kama nyanya ndogo yakiiva yanakuwa ya njano. Akachukua sindano akaigusisha kwenye kidonda halafu akaichomeka kwenye lile tunda akaviweka kwenye uchanja wake wa kutunzia kuni juu ya jiko lake la kuni. Cha ajabu ni kwamba kadri lile tunda lilivokua likinyauka na kukauka ndivyo na hiki kipele kilivokuwa kinakauka. Baadae nikapona kabisa. So haya mambo yapo
 
Back
Top Bottom