Sijui kama ni tatizo au siyo tatizo. Ila inaaffect performance ya engine. Japo siyo kwa kiwango kikubwa. Ila wewe jua tu as long as uzito unaongezeka kwenye gari basi lazima fuel economy izidi kuwa bad.
Hii haina utofauti sana na wale wanaosema AC inakula mafuta. Actually AC kama AC haitumii mafuta. Ila unapowasha AC maana yake pump ya AC itaanza kufanya kazi na itachukua power from engine hivyo kupelekea kuongezeka kwa engine load. Na engine load ikishaongezeka lazima mafuta yatumike mengi.
Yaani mpaka upigaji wa rangi kwenye gari unaaffect fuel economy.