Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Akavunjwa vidole vyote ila bado akaweza kupiga risasi kwa kutumia karoti

Alaf pale yupo angan na parashut eti akawaua majambaz wote huko angani kafika chini kakuta maiti
 
Hiyo movie niliona kipande kwa mshikaji aisee nilicheka mpaka nilipaliwa[emoji23][emoji23]
 
Daah ,,kwakweli ni shidah[emoji16][emoji16]
 
kwenye hobbs n shaws watu wanapigana kuanzia usiku hadi asubuhi hadi usiku tena!
Ile inauongo mwingi mpaka kero sasa.
Nilishtushwa sana na ile scene ya mr hobbs kupita chini ya uvungu wa semi akiwa anaride pikipiki[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]washaona watizamaji ni wajinga sana
 
Na star wa muvi hata awe kijana mdogo mwanafunzi wa chuo, ila lazima ukute anajua kuendesha kila aina ya usafiri kuanzia gari, pikipiki, boti, edikopta, treni.... yaani hata umpe kifaru anagonga gia...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
hebu tazama hii uone vituko humo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni kweli mkuu lakini wangepunguza uongo kidogo. Nyingine ni ile eti unakuta maadui kama 10 wanapigana na Jet Li ila wanaenda mmoja mmoja anawapiga mpaka wanaisha [emoji23] Sasa si wamrukie wote kwa pamoja mbona easy wangeshammaliza [emoji23][emoji23]
Mkuu achana na ngumi za kiswahili za kurukiana, kiuhalisi kama hamna ujuzi wa mapambano mkajifanya kumrukia mtu mwenye ujuzi kwa pamoja mnaweza isha kirahisi sana
 
Nafikiri baadhi ya watu hatujui nini maana ya Sci-Fi (Science Fiction)! Hizo movies mnazosema ni uongo nyingi zinaangukia katika hilo kundi nililotaja hapo juu!

Neno Science wote tunajua maana yake na Fiction ni jambo la kutunga ambalo mara nyingi huwa la kufirika! Sasa mtu ameshakuambia hiki kitu ni Science Fiction wewe bado unataka kiwe na ukweli na uhalisia na ndiyo maana zikaitwa movies jamani hebu tuweni waelewa!
 
Kwaupande mwingine upo sahihi[emoji5]
 
Hahahaha we unashangaa hilo tafuta muvi za Steven siga yule jomba hajawahi kupigwa wala kupata mchubuko wa risasi hata kwa bahati mbaya tu kuanzia muvi inaanza mpaka inaishia
Muvi zake binfsi huwa zinanikera sana, hazina uhalisia hata kidogo. Jamaa hana mvuto wa kucheza muvi labda aende kwenye mieleka.
 
Minimecheka hiyo ya kupigana juu ya train[emoji3][emoji3][emoji3]
Siyo juu ya train, juu ya train inayotembea,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wakati wengine hata kulala tu hawezi labda afungwe na mpira achilia mbali kusimama.
 
Muvi zake binfsi huwa zinanikera sana, hazina uhalisi hata kidogo. Jamaa hana mvuto wa kucheza muvi labda aende kwenye mieleka.
Kabisa kazidi sana kwa kweli hapendezi kabisa kuwa main character
 
Mkuu achana na ngumi za kiswahili za kurukiana, kiuhalisi kama hamna ujuzi wa mapambano mkajifanya kumrukia mtu mwenye ujuzi kwa pamoja mnaweza isha kirahisi sana
Mkuu hata mtu awe na ujuzi wa kupigana kiasi gani, binadamu ni binadamu na uwezo wake una limit. kuna idadi ya raia wakikuvamia kwa pamoja huchomoki. Ila wakija mmoja mmoja kama kwenye muvi ndio unawachakaza. Ndio maana hata wajuzi hua lazima wasome upepo kwanza watu wakishakua wengi cha maana ni kutoka nduki tu 😀
 
Tunaelewa maana ya fiction, ila hii haitunyimi kujadili uongo wa wazi kabisa uliopo kwenye hizo fiction movies. Wote tunajua kwamba movie ni uongo ila sasa hata huo uongo unatakiwa ukushawishi sio unaona kabisa hapa hawa jamaa wananionaje kuweka kitu kama hiki? Ndio hapo hasira zetu zinapoanzia. Tunapinga kuonekana maboya 💪
 
Na ikitokea akapata mimba ni siku hiyohiyo tayari tumbo linakua kubwa mtu hawezi kutembea na kiuno kinamuuma. [emoji3]
Na akiwa na mimba hana mamuudi ya kununa nuna kama mama athumani au jamila mititi
Na akiwa na mimba hawatemi mate wala hawatoki machunusi kama yule "juliana"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…