Vituko jikoni, Let us share and have fun

sikumoja home nliunga harage nazi. kumbe kuna kitunguusaum hakikusagika. baba kakutananacho akanirudishia,'' kieke upikie tena kesho''

Hahahaha lol nimecheka...

Mie sipendi kukiona kitunguu maji kwenye mchuzi
 
Ha ha h ha ha mbona uongeza wingi wa mboga!mwisho wasiku ndio unkuwa mpishi mzuri
 
mm nakumbuka nkiwa 11 nliambiwa nipike uji ,Unga nliouweka ni shidah kila nikikoroga uji unazid kuwa mzito yani kama ugali nlichofanya haraka haraka nlipunguza nkamwagia mbali afu uliobakia kidogo nkaongeza maji sana basi ukarudi normal,,ni shidahh
:laugh:
 
huhu niliachwa hom...jikon palikuwa na wali.... ndo ulikuwa ktk kukauka bibi kapunguza moto katoka.... mimi kuingia...nikakuta moto mdogo....nikaongeza kuni....mmmm nikaskia harufu ya kuunguza si nikaweka maji.....huuuu. bibi alivyorudi.... nikampokea na maneno......'ungeunguza chakula...' wakati mm ndo meunguza ulilika lkn.....
 

Pole sana. Nina braza angu alikuwa mtu wa home tu sasa wakamtafutia eneo la garage angalau ajifunze ufundi wa magari. Akaanza siku ya kwanza katika kuzoea eneo akakutana na dumu jipya jipya kuangalia ndani akakuta mafuta kuangalia yanafanana na ya pamba ya kupikia. Akarudi home direct kwa mother na kumtonya kuwa kule kazini kakuta dumu la mafuta ya kupitia kazini kwao yapo yapo tu akamuhaidi siku inayofuatia atawaomba na kuyaleta skani ili yasaidie siku ikafika mama akaahidi kuja na mpunga kilo tatu ili ukaangwe na mafuta mapya jioni bro huyo na galoni liko nusu tukashangilia kuwa yalikuwa mengi ukapikwa wali na mafuta kuwekwa duu!. Mother asistukie hapo bweche linatokota na kutoa harufu kali ya oil tena ya gari. Mother kasara mbaya likatengwa fugo la ugali wacha tucheke wengine tulikuwa wadogo tukagoma kula ugali tunataka wali mama akatwambia ni sumu tutakufa tukagwaya asubuhi yake bweche lote kilo mbili likamwagwa jalalani bro akairudisha oil ilikotoka sitokaa nisahau hii kamwe. Du!.
 
hahaaaaaa,you have made my evening! loh1 hiyo ilikuwa kali.
 
Nilikuwa na kosana na mama mchaga kila nikipika ndizi nyama lazima akosoe loo
 
Mara ya kwanza kuandaa na kuchoma samosa

Nilivyoweka kwenye mafuta zikawa zinafunguka.... Hahaha mchanganyiko wote ukawa umesambaa
Kuumbe ile chapati na uji wa ngano ulikua mzitoo, loh
Nilichekwa sana ila "kukosea njia ndo kujua njia "
Chocs umenikumbusha nilipika samosa na haraka zangu sikuweka ile pastry kwenye friji wala kufunika na kitambaa ili isipoteza unyevu ,kwenda kukaanga ikawa kama ngozi ya mamba juu.
 
Last edited by a moderator:
Chocs umenikumbusha nilipika samosa na haraka zangu sikuweka ile pastry kwenye friji wala kufunika na kitambaa ili isipoteza unyevu ,kwenda kukaanga ikawa kama ngozi ya mamba juu.


Ahaha.... Yani jikon kunakuaga na vimbwanga acha tu
Mtu asione kishaandaliwa mezani, dah
 
Last edited by a moderator:

Hahahahaaaaa...hadi nimecheka kwa nguvu...

Hiyo ya ugenini nliwahi kuweka chumvi nyingi kwenye msosi...wakati wa kula nikazuga kwetu ndo tumezoea chumvi nyingiii...walijibebaa...
 
hahahahaaaaa...hadi nimecheka kwa nguvu...

Hiyo ya ugenini nliwahi kuweka chumvi nyingi kwenye msosi...wakati wa kula nikazuga kwetu ndo tumezoea chumvi nyingiii...walijibebaa...
basi chakula bora hata kiwe na chumvi kidogo watu wataongeza kuliko kuzidi inakua noumer.

Mara unaambiwa umepandisha watu presha. Lol
 
basi chakula bora hata kiwe na chumvi kidogo watu wataongeza kuliko kuzidi inakua noumer.

Mara unaambiwa umepandisha watu presha. Lol

Yaani hili lilikuwa tatizo langu kubwa kuzidisha chumvi ili nimeli-control kwa kuweka kidogo sawa wacha waongeze wenyewe
 
Nimewahi kuunga majani ya chai badala ya chumvi kwenye mboga kwa kuchanganya makopo ya viungo

hii ilinikuta mimi nikiwa napika wali na umeme umekatika ghafla kabla sijaweka mafuta, kushikashika kwenye giza nikadhani ni kopo la mafuta kumbe majani ya chai. nikawa na wasiwasi na nilichotia kwenye wali, nikatafuta karatasi ili niwashe nichungulie nilichotia, loooh! kumbe majani ya chai. nilichukua sifuria faster nikamwaga wali wote chooni kabla mama hajanikuta nikaanza upya na uzuri wake mchele upo ndani. Loh!
 


Angel umeolewa?
 
Wiki moja iliyopita nilipatwa na homa, Mimi ndo mpishi home...bahati nzuri Kaka yangu alichukua likizo ya wiki kazini so akaja home....Akakaimu nafasi yangu jikoni....sasa kuna siku akapika chuzi hilo sijawahi ona....yani kachukua nyanya maji (tungule), nyanya chungu, bamia kavitia kwenye Brenda kasaga pamoja...ndo vikapikiwa samaki....

Duh....nlichokaaaa.....!
 


Hahaha rosti la kusaga lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…