Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,267
- 29,917
Welcome back
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1] [emoji1]Nina usingizi balaaa
welcome back we missed you Mrs jrKwanza jaman Niliwamiss sana Demiss miye mama ntilieee miyeeee .
Kabla ya yote shukrani kwa member hawa Mwifwa Zero IQ Samweli faraj mmepambana sana kunirudisha jf mungu awabariki sana japo najua wengi wanataman kujua kwann nilipotea ila mambo mengine ni vyema kukaa kimya ili maisha yaendelee bila hivyo tutaonana wa ajabu bure.
Leo wacha niwape kituko kimoja ambacho mpaka leo najiuliza yawezekana nisingekuwa mama ntilie ningekuwa gereza la keko.
Nakumbuka nikiwa form 3 mwaka 201- ktk shule moja Dar nilikuwa na rafiki yangu Apple tumekaa tunawaza wapi tupate pocket money kwa ajili ya kula kachori canteen.
Aisee nikawa nimepata wazo la kuiba sadaka kanisani Mungu anisamehe tu kwa kweli.
Shule niliyosoma mm siku ya Jumapili tulikuwa tunaruhusiwa kutoka nje ya Shule kwenda kusali kanisani kila jumapili.
Siku ya tukio ikafika mimi na Apple tumeshapanga mpango wa jinsi ya kwenda kuiba sadaka kanisani tukaamka mapema tukavaa nguo haoo asubuhi tukatoka kuelekea kanisani tukawahi nafasi zetu kusubiria muda wa mashambulizi.
Hatimaye muda ukawadia wa kutoa sadaka na unajua makanisa makubwa watu huwa wanatoa elf 10 kama sadaka hapo sasa tukasema sisi tutakuwa wa mwisho.
Unajua kwanini?
Watu wanavyotoa sadaka huwa wanakunja mikono kama ngumi[emoji109][emoji109] na ndani yake kunakuwa na pesaa.
Na makanisa mengi wanaweka vikapu na kuvifunika na kitambaa hivyo unaingiza mkono unaweka hela ndani ya kikapu.
Baada ya watu kupungua mimi na Apple tukainuka tukiwa tumekunja mikono yetu kama ngumi[emoji109][emoji109]ikiwa haina kitu mpaka kwenye kapu la sadaka.
Nilivyofika pale nikadumbukiza mkono na kuokota hela yani unacheza Biko hujui unaokota sh ngap?
Nikatoa mkono nikiwa nimekunja ngumi vile vile ndani kuna hela nimeshaichukua nikarudi mpaka kwenye kiti changu nikafungua kipochi changu nikaidumbukiza laahaulaa!!nikaona kitu cha msimbazi elf 10.
Muda kidogo Apple naye akafika akachukua pochi yake akadumbukiza mkono kumbe alichukua hela mbili moja elf 5 nyingine elf 2 .
Tulivyotoka kanisani tukasema mungu tusamehe hatukuwa na jinsi.
Najua wengi mtashangaa sana ila ilikuwa ni mojawapo ya maisha ambayo ni lazima ningepitia ili nifike hapa nilipo wengi wameshaiba ila wanaona aibu kusimulia mimi sinaga aibu huwa nasema tu si yalishapita bhn au?
Mama ntilie Demiss.
yaa naonaMama ntilie wa Digital
me moreeeMiss u shem baeeee
[emoji119]Love mingiii mingiiii
Unataka kunipikaaaa