Vituko na vioja vya wadada wa benki

Hakika mkuu,

Unakuta mtu sawa amesomea kazi anayoifanya lakini customer care haipo kichwani mwake, ndomana dharau haziishi majivuno mengii,hawalijui kuwa wewe mteja ndio sababu ya wao kuwa pale WTF

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Hii kazi ya kushikashika mahela inataka moyo sana, yaani job unashika manoti, ukirudi home watoto wanakula tembele!..kwa kweli tuwavumilie tu..
 
Umeshasema unawafahamu

Sie tusiependa mazoea na wahudumu hatustahili huduma nzuri?

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Customer care ni mbovu kila sehemu Tanzania
Sio kwa mwanamke au mwanaume
Labda uwe hotel za 5 star ndio watakufanyia vyema ila pengine sijui airport mmmmmh
 
MKUU WAKATI MWINGNE DHARAU ZNATOKANA NA AKAUNT INAVYOSOMA, KAMA BALANCE NI M 5 WANAKUONA KAPUKU TU

ILA AKAUNTI INA M 100 NA KUENDELEA HUKO, OH, MBNA HATA KWENYE CM ATAKUWA ANAKUTAFUTA NA HUDUMA UTAPEWA KWA SAUT YA MAPENZ NA MACHO YA KULEGEA.

hakuna teller au bank officer anaekuona kapuku kwa balance milion 5... labda uwe umekopa.. mimi kazi yangu naprint tshirt tu nina ofisi yangu kkoo... bank yangu nmb na crdb... sijawai kuwa na hela nyingi sana kwenye account mara nyingi m 3 to 5m tu....ila sijawai kunyanyaswa na staff wa bank.. na tip nawapaga mara moja moja buku 5 au 10 siku nikiwa nimepiga hela nzuri
 
Kuibua ngano za ajabu juu ya binadamu wenzetu wanaojitahidi kutekeleza majukumu sehemu zao za kazi si kitendo cha kiutu.

Watumishi wengi katika sekta ya benki wanajitahidi,wasichana wakiwemo.Tatizo la wengi wetu tunapenda kuheshimiwa na wengine wakati wenyewe hatujiheshimu wala kuheshimu wengine.
 
Wana stress za maisha. Wanashuka miliins of money per day lakini mwisho wa mwezi wanalipwa laki 4 na 50

Sent using Jamii Forums mobile app
 
***** mmenikumbusha miaka ya nyuma hivi.

Niliingia benki moja nikaenda kwenye dirisha la maulizo,
Mungu wangu nilivojibiwa kuhusu kufungua akaunti, niliambiwa subiri, kweli asee ilikuwa subiri ya maana.

Nikasema poa na utu uzima wangu huu huyu mtoto ananichezea akili??
Nikachukua ki begi nikaingia kwa meneja, nikamwambia bwana nina vijihela hapa, nataka kufungua akaunti,
Akaniambia umeenda maulizo??
Nikamjibu ndio toka saa tatu mpaka sasa saa sita nimeambiwa nisyubiri au kwa kuwa mi sina suti??

Asee meneja akanifungulia nikaweka mzigo wangu, mwisho akaniahidi atalifanyia kazi na aliniomba radhi kiukweli.

Nilichoshangaa siku moja yule dada alinikuta offucine anatafuta kazi akanipa nyaraka zake, nikaamuambia nitampa taarifa aje kwenye usaili

Mungu anisamehe nilimpa taarifa kuwa anatakiwa aje kwenye usaili siku mbili baada ya usaili wenyewe.

Aliumia mnoo lakini nilishatubu asee, mi hata madirishani siku hizi siingii aseee
 
mm naona kama wanastress sana ndio maana wanakuwa na hasira , maana unashika hela nyingi halafu wewe mwenyewe hauna salio mfukoni mwisho wa siku unakuwa na mahasira kwa wateja ambayo hayana hata maana.....

tuwasameeni bureeeeee jamani
 
Moja ya upuuuuz ambao toka niijue hela ni kutafuta marafiki kwa kujipendekeza.

Eti na utu uzima huu mtu nilazimishe urafiki kisa huduma??

Meneja wao wenyewe tukikutana ni kunihudumia tuu ujinga na mazoea nao mi sipendi yeye atapita benki na account yangu vitadumu milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…