Vituko na vioja vya wadada wa benki

Vituko na vioja vya wadada wa benki

Watanzania wengi hatujawa vizuri katika biashara ya huduma,,kiasi unaweza kuhisi mtu yupo pale si kwa ujuzi wake bali sura yake. Tusipobadilika wakenya nawachina watachukua ajira zote huku tukibadilisha vyama kila siku na katiba kila wiki..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika mkuu,

Unakuta mtu sawa amesomea kazi anayoifanya lakini customer care haipo kichwani mwake, ndomana dharau haziishi majivuno mengii,hawalijui kuwa wewe mteja ndio sababu ya wao kuwa pale WTF

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Hii kazi ya kushikashika mahela inataka moyo sana, yaani job unashika manoti, ukirudi home watoto wanakula tembele!..kwa kweli tuwavumilie tu..
 
Pamoja na huduma mbovu za baadhi ya wafanyakazi wa benki labda wateja wengine nao wana matatizo. Au wengine mnaenda benki tofauti kila siku?
Benki yako(yaani una akaunti hapo muda mrefu) lazima utakuwa unajulikana na wahudumu wengi tu na mnaweza kuwa marafiki kitu ambacho kitakusaidia kupata huduma nzuri ambayo unastahili kuipata hata ukiwa huna rafiki.
Mimi ninapo-bank nawajua wahudumu wote hadi branch manager kwa sababu hii labda ndio maana napata first class service,wafanyakazi wote wa bank hadi walinzi wa security company wananifahamu na ni 'marafiki'
Habari ya kuibiwa hela na teller ukishafahamiana na hawa watu haipo,tena muda mwingine unakuta foleni kubwa au system down unamuachia hela anakugongea tu muhuri system ikiwa fresh anamalizia transaction.
Tuwaheshimu wengine na sisi watatuheshimu.
Umeshasema unawafahamu

Sie tusiependa mazoea na wahudumu hatustahili huduma nzuri?

post using my macbook air using jamiiforums app
 
Customer care ni mbovu kila sehemu Tanzania
Sio kwa mwanamke au mwanaume
Labda uwe hotel za 5 star ndio watakufanyia vyema ila pengine sijui airport mmmmmh
 
MKUU WAKATI MWINGNE DHARAU ZNATOKANA NA AKAUNT INAVYOSOMA, KAMA BALANCE NI M 5 WANAKUONA KAPUKU TU

ILA AKAUNTI INA M 100 NA KUENDELEA HUKO, OH, MBNA HATA KWENYE CM ATAKUWA ANAKUTAFUTA NA HUDUMA UTAPEWA KWA SAUT YA MAPENZ NA MACHO YA KULEGEA.

hakuna teller au bank officer anaekuona kapuku kwa balance milion 5... labda uwe umekopa.. mimi kazi yangu naprint tshirt tu nina ofisi yangu kkoo... bank yangu nmb na crdb... sijawai kuwa na hela nyingi sana kwenye account mara nyingi m 3 to 5m tu....ila sijawai kunyanyaswa na staff wa bank.. na tip nawapaga mara moja moja buku 5 au 10 siku nikiwa nimepiga hela nzuri
 
Kuibua ngano za ajabu juu ya binadamu wenzetu wanaojitahidi kutekeleza majukumu sehemu zao za kazi si kitendo cha kiutu.

Watumishi wengi katika sekta ya benki wanajitahidi,wasichana wakiwemo.Tatizo la wengi wetu tunapenda kuheshimiwa na wengine wakati wenyewe hatujiheshimu wala kuheshimu wengine.
 
Wakuu za mida hii?

Leo nimeona tuwaangazie hawa dada zetu wa benki ambao baadhi yao wanadharau sana kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi zako.

Kuna kipindi rafiki yangu alienda benki moja kuulizia wamefikia wapi mchakato wa kuwaita kwenye " interview " cha ajabu yule dada akamjibu nanukuu " unadhani ukijipitisha hapa ndio utaonewa huruma" .

Mimi pia kuna dada benki teller alinidharau wakati ananihidumia nikamuangalia tu.

Je wewe umekutana na lipi kutoka kwa hawa Maofisa wa kike wa benki?

Nawasilisha.
Wana stress za maisha. Wanashuka miliins of money per day lakini mwisho wa mwezi wanalipwa laki 4 na 50

Sent using Jamii Forums mobile app
 
***** mmenikumbusha miaka ya nyuma hivi.

Niliingia benki moja nikaenda kwenye dirisha la maulizo,
Mungu wangu nilivojibiwa kuhusu kufungua akaunti, niliambiwa subiri, kweli asee ilikuwa subiri ya maana.

Nikasema poa na utu uzima wangu huu huyu mtoto ananichezea akili??
Nikachukua ki begi nikaingia kwa meneja, nikamwambia bwana nina vijihela hapa, nataka kufungua akaunti,
Akaniambia umeenda maulizo??
Nikamjibu ndio toka saa tatu mpaka sasa saa sita nimeambiwa nisyubiri au kwa kuwa mi sina suti??

Asee meneja akanifungulia nikaweka mzigo wangu, mwisho akaniahidi atalifanyia kazi na aliniomba radhi kiukweli.

Nilichoshangaa siku moja yule dada alinikuta offucine anatafuta kazi akanipa nyaraka zake, nikaamuambia nitampa taarifa aje kwenye usaili

Mungu anisamehe nilimpa taarifa kuwa anatakiwa aje kwenye usaili siku mbili baada ya usaili wenyewe.

Aliumia mnoo lakini nilishatubu asee, mi hata madirishani siku hizi siingii aseee
 
mm naona kama wanastress sana ndio maana wanakuwa na hasira , maana unashika hela nyingi halafu wewe mwenyewe hauna salio mfukoni mwisho wa siku unakuwa na mahasira kwa wateja ambayo hayana hata maana.....

tuwasameeni bureeeeee jamani
 
Sasa unafikiri kila mtu ana muda wa "kufahamiana" na mtoa huduma wa ofisi wa kila taasisi anayopita? Wengine muda ni mali na tunazo ofisi zetu pia nazo zina viyoyozi kama za hao bank tellers wenye nyodo na hata kama hazina viyoyozi zinalipa vyema kuliko visenti vyao uchwara na bado tunawaletea biashara na hatuna nyodo. By the way ni miongozo ya bank gani inaagiza ili upate huduma nzuri (ambayo ni haki yako) ni lazima uwe na urafiki na hao mahousegirl wao (bank tellers sijui)? Nakosa muda hata wa kumpigia mama mzazi nianze kupoteza muda kujipendekeza kwa KIMA ambaye hana adabu na bila mimi hana sababu ya kuwepo hapo alipo? Wajiheshimu na kuheshimu wateja bhana, heshima kitu cha bure na kwenye kazi kama zao ni kitu cha LAZIMA hata kama ana ugomvi na bwana wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya upuuuuz ambao toka niijue hela ni kutafuta marafiki kwa kujipendekeza.

Eti na utu uzima huu mtu nilazimishe urafiki kisa huduma??

Meneja wao wenyewe tukikutana ni kunihudumia tuu ujinga na mazoea nao mi sipendi yeye atapita benki na account yangu vitadumu milele
 
Back
Top Bottom